Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Bahati Alikata Kiu
Bahati Alikata Kiu
Bahati Alikata Kiu
Ebook101 pages2 hours

Bahati Alikata Kiu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Bahati Alikata Kiu ni hadithi fupi iliyoendelezwa kutokana na riwaya Kiu.
Bahati, kinyume na waliowengi waliomwona kauawa na Idi, alipona na aliishi maisha ya fanaka.

LanguageKiswahili
Release dateJun 14, 2014
ISBN9781311986818
Bahati Alikata Kiu
Author

James Kemoli Amata

I am a retired secondary school teacher of Kiswahili (and Christian Religious Education) and an excited preventive healthcare marketer with Green World Health Products Company.I am a 1976 University of Nairobi Bachelor of Education [Arts (Hons)] graduate and a freelance content writer with a passion for writing and indeed I am a farmer-like author with many titles.I published my first book in 1985, by traditional publishing. I have tried self-publishing and now I am in great heat to explore E-publishing.However, I will never forget my Taaluma ya Ushairi (with Kitula King’ei) from which the publisher ate fat alone, and happens to be an E-book without my knowledge.As I do my business, I worship God in African Kenya Sabcrynnsk of Soi (Prayer and Healing) Church.

Read more from James Kemoli Amata

Related to Bahati Alikata Kiu

Related ebooks

Reviews for Bahati Alikata Kiu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Bahati Alikata Kiu - James Kemoli Amata

    Bahati Alikata Kiu

    Iwapo ilisoma Kiu, Mohamed Suleiman Mohamed, Longhorn Publishers, 1972, Idi alimfisha Bahati, halafu iweje amehuishwa?

    James Kemoli Amata

    Anwani ya Mahali:

    Tiens Specialty Shop

    KVDA Plaza, Mezzanine Floor

    Eldoret

    Kenya

    Anwani ya Posta:

    PO Box 2-30105

    Soy

    Kenya

    Rununu: +254 721 720 699/+254 734 720 699

    B-Pepe: kemoli2003@yahoo.com

    Toleo la Smashwords.com

    Bahati Alikata Kiu

    © James Kemoli Amata, 2006

    Maelezo ya Idhini ya Toleo la Smashwords

    Kitabu hiki cha kielektroniki kimeidhinishwa kwa raha na furaha yako peke yako ya kibinafsi. Usikiuze tena wala usiwape watu wengine. Ukitaka kutumia pamoja na mtu mwingine, tafadhali nunua nakala ya ziada kwa kila mtumizi. Iwapo unakisoma kitabu hiki lakini hukukinunua au hakikununuliwa kwa matumizi yako wewe peke yako, hivyo basi kirudishe kwa Smashwords.com na ununue nakala yako mwenyewe. Asante kwa kuiheshimu kazi ngumu ya mtunzi huyu.

    Kimetangazwa kwanza na

    James Kemoli Amata, Jumatano, Mei 07, 2014

    Mtabaruku

    Mabinti zangu wapenzi Jemimah Kang’alika, Annet Kalenya na Juliet Minage.

    Shukrani

    Mungu Baba yetu aliye mbinguni. Amenipa uhai wa bure, bila malipo.

    Margaret M’mbone. Yeye ni mke wangu na mama ya wana wangu na mabinti zangu.

    Jeniffer Chepkirui, Modern Professionals Worldwide. Bila yeye nisingeweza kukiandika kitabu hiki.

    Usanii wa jalada na James Kemoli Amata

    Lugha zilizotumika ni Swahili and Ullogoli

    ***

    Bahati Alikata Kiu

    James Kemoli Amata

    ***

    1

    KINARANI palikuwa kimya. Ndege ndio walioonekana wakirejea viotani. Kabla Idi afike fikira haikumjia Bahati binti Cheusi kuwa pahali pale palikuwa na hatari yoyote. Alikuwa ametulia rohoni huku akitembeatembea, mara akienda mbele mara akirudi. Saa kumi na moja u nusu ilifika ikapita. Akitaka kukata tamaa alizuiwa na kumbukumbu subira yavuta heri. Mara likatokea gari alilolifahamu barabara. Gari la Idi. Kweli. Mgaagaa na upwa haondokei patupu.

    Moyo ulimdundadunda Bahati. Atakubali kunigawia nusu bin nusu au atanirejesha nyumbani au atakana kabisa. Pengine atanirejesha nyumbani na aniambie, 'Chochote nilicho nacho ni chako wewe; bila wewe mimi sina kitu, na hata uhai nilio nao kutoka kwa Mwenyezi-Mungu utanitoka ----' Fikira za Bahati zilikuwa chunguchungu. Kimwana yule akawa sawa na mwehu.

    Idi alisimamisha gari karibu na Bahati akakitokeza kichwa nje kupitia dirishani. Alionekana mchangamfu ila mwenye hofu ya kutaka msaada ambao hakuwa na imani angeupata.

    Tafadhali Bahati, karibu ndani tuongee. Tulizungumzie lile jambo na tulimalize kabisa kabisa.

    Bahati aliamini wema ulikuwa mbele yake. Alijitia moyo thabiti kujikwaa si kuanguka na kuanguka si kufa. Akiwa bado anampenda Idi alijiambia, 'Hakika siwezi kukubali Idi wangu kapoteza ladha kama mate yaliyotemwa.' Hakusita kuingia garini. Kwa sauti ya mtu mwenye utu Idi alimkaribisha.

    Tufumbe macho tuombe, Idi aliomba ombi la ajabu. Bahati alitaka kucheka kicheko cha furaha ila akahofu kumbughudhi na kumghadhabisha Idi wake. Alijikakamua na kujizuia kikamilifu.

    Naam ---- Bahati alitamka kwa sauti ya unyenyekevu, yenye mnato wa kuinata hata roho ya Izraili isipokuwa alishindwa ahitimishe usemi wake kwa 'bwana' au 'mume wangu'.

    Ewe Mola Muumba, Mola wa kusamehe dhambi ndogondogo, mwenye kusamehe dhambi kubwakubwa, tuepushe na maovu na athari za madhambi yaliyopita ----

    Idi alimnyoshea Bahati mkono. Hiyo ilikuwa ajabu nyingine katika muhula wa miaka mingi. Bahati alipata matumaini mapya. Ikamwingia fikira ya imani na amani, 'Huyu Idi, hakika Idi ametubu na ushetani wote umemhama.'

    "Masalkheri Bibi binti Cheusi."

    "Alkheri Bwana."

    Idi alikuwa na uhuru wa kumwita Bahati binti Cheusi au kumtajia mke wangu. Lakini hakufanya hivyo. Alihiari amwite binti Cheusi. Katika desturi za Kiislamu mke aliyeolewa, tangu jadi ana uhuru wa kulitumia jina la mzazi wake na la mume wake au lile alilochagua. Miongoni mwa watu wa magharibi ya ulimwengu ni jambo la fedheha kwa mke kujiita jina la baba au mama yake. Bwana mmoja aliwahi kumtaliki mkewe, sababu mojawapo ikiwa, 'Yeye hulitumia jina la baba yake mara kwa mara akinifedhehesha na kunitweza."

    Idi aliendelea, Nimekuita ufike hapa ili tusawazishe yaliyopotoka. Mimi unionavyo, Kimwana Bahati binti Cheusi, roho yangu kwako, safi sana. Sina nia yoyote ya kukudhulumu. Siwezi kukuhini nafasi yako, wallahi kama Mola bado amenipa uhai. Unanielewa?

    Naam -

    Mbona unasita kama kwamba huniamini? Unashuku jambo lolote lile?

    Sisiti -

    Una wasiwasi lakini? Sivyo?

    Sina -

    Mimi naomba jambo moja tu. Kama Mwenyezi-Mungu angehiari akufunulie roho yangu. Uangaze ndani uone jinsi nilivyo na nia safi, nia safi sana kwako, Bahati, Kimwana Bahati binti Cheusi. Alirai Idi.

    Basi sema ulichoniitia hapa. Mahali hapa panitisha ambavyo hapana watu wengi.

    Watu wana haja gani katika mazungumzo yetu? Mimi lengo langu ni kukutimizia haki. Nataka nikufanyie insafu.

    Wewe unaona msitu ndio huu hapa karibu na watu hawapo. Mafisi yatokee yaje yanimalize.

    Fisi wa wapi?

    Fisi wa siku hizi. Si kama wa zamani. Watakutafuna mzimamzima bila kungoja zikutoke pumzi.

    Huo ni upuuzi ambao haunihusu ndewe wala sikio.

    Basi, wacha hilo lipite hivyo basi.

    "Tuongee juu ya haki yako. Nataka upige hesabu yako sasa hivi na uniambie thamani yako katika dunia hii ni nini? How much are you worth? Utalijibu hilo swali. Nakupa muda."

    Hilo ni swali gumu. Swala la thamani ya mtu linahitaji mashauriano.

    Sikubaliani nawe wala sitakubaliana nawe. Ukidai haki yako, ulitaka kiasi gani, la si hivyo univue zotezote nibaki wa mnyama?

    Nikuvue nini?

    Kimwana Bahati binti Cheusi, Idi aliongea kwa sauti nyororo thabiti, tafadhali tusizungushane juu ya haki yako. Nimehiari nikupe haki yako. Nimekubali nikupe haki yako bila kukuhini hata senti moja. Haki yako na itoke mdomoni mwako.

    Nipe muda basi.

    Muda kuutaka una maana ukidai haki hiyo kwa kitisho cha kuniweka wazi uchi wangu ulishauriwa ndipo wataka muda uweze kushauriana?

    Haki yangu - kudai haki yangu - sikushauriwa.

    Utasema ukweli ndipo hesabu iweze kufanyika. Nitakusaidia kuifanya.

    Siku zote nimekufanya kama paka. Mnyama wa kukaa miguuni pa mtu kujifurahisha.

    Umeanza tena kunitukana?

    Sikutukani. Kwa ufupi wewe si paka tena. Wewe ni kimwana. Kimwana, mtoto wa watu. Wewe ni wadinasi. Kimwana Bahati binti Cheusi. Na ndio maana nipo tuzungumzie haki yako bila kukuhini hata senti moja.

    Bahati na Idi waliongea kwa muda mrefu. Haja kubwa aliyokuwa nayo Idi ilikuwa avumbue asili ya Bahati kutaka haki yake. Idi aliamini ya kuwa kulikuwepo na mtu wa tatu na pengine hata wa nne aliyemshawishi Bahati adai haki yake. Haki ambayo Idi hakuitambua wala kuifikiria.

    Bahati naye kwa upande wa pili alitaka sana

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1