Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Nyayo Za Obama
Nyayo Za Obama
Nyayo Za Obama
Ebook279 pages12 hours

Nyayo Za Obama

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

"Nyayo Za Obama" ni kati ya vitabu vichache vilivyoandikwa kwa Kiswahili sanifu ambavyo vinazingatia historia ya ya Marekani, raia zake, uchumi na majukumu yake ya uongozi katika dunia ya utandawazi.Kati ya uongozi wake muhimu ni ule wa taasisi za kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Taasisi za Bretonwoods kama vile Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), nk. KIkifuatilia maisha ya rais wa 44 wa Marekani kuanzia nasaba yake ya Kiafrika, hadi alikofikia kwenye kilele cha siasa ya Marekani, kinaeleza kinaganaga jinsi Barack Obama alivyoanza amali yake ya siasa, mbinu alizotumia kupiku wapinzani wake wakubwa hasa katika kampeni za kinyang'anyiro cha urais hadi kwenye tamati ya ushindi wake wa kihistoria. KItabu hiki kimeandaliwa kwa wasomaji wale wenye ujuzi wa lugha nyingine hasa Kiingereza, ili kuweza kujieleza vizuri kwa Kiswahili bila kulazimika daima kukopa maneno au semi kutoka kwa lugha ya Kiingereza. Kwa ajili ya lengo hilo, kurasa za mwisho za kitabu hiki kinacho msamiati mahasusi unaosheheni tafsiri za maneno mengi ya Kiingereza katika Kiswahili sanifu.

LanguageKiswahili
Release dateApr 4, 2015
ISBN9781310475436
Nyayo Za Obama
Author

Safari E. Ohumay

Safari E. Ohumay is a US citizen who was born in a rural village of Tanzania. He first came to the US as a graduate student in Development Management and returned home after graduating in 1976. Earlier on he studied Math and Economics and graduated with a BS degree from the university of DaresSalaam in early 1972. After a two year stint in senior management in two Tanzanian industrial processing firms he received a job offer from the World Bank Group in Washington DC through its Young Professionals Program.For the next 18 years he travelled extensively from Washington to many parts of Asia and Africa as the World Bank’s Program manager focusing in Infrastructure and Urban development under the theme of poverty alleviation. He spent most of his career in the World Bank working with countries such as Bangladesh, Burma, Indonesia, Pakistan and Srilanka in Asia, and Kenya, Malawi, Swaziland and Tanzania in Africa. Recently he joined the US Agency for International Development team in Afghanistan for one year as a Field Program officer at the height of the US campaign against Al-Kaida. Safari E. Ohumay lives in the Washington suburbs of Maryland and works as a freelance consultant.

Related to Nyayo Za Obama

Related ebooks

Reviews for Nyayo Za Obama

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Nyayo Za Obama - Safari E. Ohumay

    Nyayo za Obama ni fasihi ya lugha ya Kiswahili iliyosanifiwa katika sura ya kitabu. Maudhui na mandhari ya fasihi hii siyo mageni kwa wengi kwani hadithi juu ya Barack Obama na nchi anayoiongoza, Marekani zinapatikana kote katika ulimwengu wa utandawazi, wavuti na tovuti, na barua pepe nakadhalika. Madhumuni hasa ya kitabu hiki ni kutumia hiyo hadithi ya Barack Obama na nchi anayoiongoza na kuiweka katika herufi na fasili ya lugha ya Kiswahili.  Kwa mtazamo huo Nyayo za Obama ni fasili za maisha yake na taifa lililomwezesha kufika hapo aliko kwenye kilele cha siasa- rais wa 44 wa Marekani tangu George Washington.

    Kwa kuziandika fasili hizo katika lugha ya Kiswahili tunatanabahi kwamba chombo muhimu kuliko vyote katika uwasilishaji wa hadithi, hotuba, mahubiri au maelezo ya aina fulani kimo ndani ya fasihi ya lugha ambayo wasomaji au wasikilizaji walengwa wanaielewa. Kwa sisi wa Afrika ya Mashariki na wapenzi wa utamaduni wa Kiswahili, wahenga wetu walituachia urithi wa lugha ya Kiswahili katika fasihi za maandishi ya vitabu, mashairi, riwaya na mengineyo. Fasihi hapa inamaanisha vitu vyote vilivyoko katika maandishi, yawe kwenye karatasi, au kwa elektroni; na lugha iliyotumika kusanifu hayo maandishi huchukua fasihi hiyo. Kwa mantiki hiyo Nyayo za Obama ni kitabu ambacho kinachangia katika kukuza na kuboresha lugha ya Kiswahili kwa kuandika  fasili zake juu ya mada mbalimbali za ulimwengu  wa karne ya ishirini na moja..

    Fasihi za lugha ni muhimu sana siyo tu katika watu waliyojijumuisha kama taifa moja, bali ni mojawapo ya njia tegemevu ya kuleta maelewano bora baina ya mataifa na hivyo kushamirisha amani na neema duniani.  Kila taifa likiwakilishwa na viongozi wake kawaida hufanya maazimio yanayoiainisha hiyo nchi kama taifa moja wakati wa kilele cha uhuru wake. Viongozi waanzilishi wa Marekani katika kilele cha uhuru wao kutoka kwa Wakoloni wa Uingereza walikuwa na haya kati ya mengine katika ilani zao za uhuru:

    Tafsiri: Wanadamu wote wameumbwa  sawa na kuna haki fulani zisizohamishika ambazo serikali kamwe zisikiuke.  Haki hizi ni pamoja  na haki ya kuishi,  huria, na kufukuzia starehe.  Endapo serikali itashindwa kulinda haki hizo, siyo tu ni haki, bali pia ni wajibu wa watu kupindua serikali hiyo. Badala yake watu hawana budi kuunda serikali ambayo imeazimiwa kulinda haki hizo. Serikali hupinduliwa kwa nadra, na haipaswi kupinduliwa kwa sababu uchwara. Katika hali hii, historia ndefu ya maonevu  imewaongoza watawaliwa kuipindua serikali ya udhalimu.

    Katika kipindi kile kwenye karne ya 18 watu wa Marekani ile ya majimbo 13 ya mwanzo walikuwa na utamaduni wa lugha ya Kiingereza na hivyo wengi wao, hata kama siyo wote waliweza kusikia au kusoma maazimio hayo yaliyoandaliwa na viongozi  wa wakati ule, na  hivyo walielewa vizuri  matarajio ya azimio la viongozi wao.

    Katika karne hii ya 21 lugha rasmi ya taifa la Marekani bado ni Kiingereza ijapokuwa wananchi wake leo wamekuwa anuwai sana.   Jambo ambalo lingalifikiriwa la mwujiza kutokea katika  miongo miwili iliyopita lilijitokeza kwa kishindo hivi karibuni hapa nchini Marekani. Jambo hilo ni kwa watu wa Marekani, nchi ambayo uchumi wake ulikuwa ukishamiri juu ya migongo ya watumwa wa asili ya Afrika karne mbili tu zilizopita, leo hii wako na rais wao mwenye asili ya Kiafrika.  Barack Obama aliposhinda kinyang’anyiro cha uteuzi wa chama chake  cha Demokrasia na halafu akaenda kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2008, na akawa rais wa Marekani wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika, taifa lilijiduwaza na yeye alikuwa na haya ya kusema kwa taifa lililomchagua:

    Tafsiri: Endapo kuna mtu huko ambaye bado anayo tashwishi kuwa Marekani ni mahali ambako vitu vyote vinawezekana; ambaye bado anaajabia iwapo ndoto ya waanzilishi wetu ni hai katika enzi yetu; ambaye bado anashukia nguvu ya demokrasia yetu, leo jibu lako limewadia.

    Hilo ni jibu ambalo liliashiriwa na misururu ya watu iliyonyooka na kuzungukia mashuleni, makanisani kwa halaiki ambayo nchi kamwe hakuwahi kuiona; na watu ambao walisubiri kwa saa tatu, na  saa nne, wengi wao ikiwa mara ya kwanza katika uhai wao, kwa maana waliamini kwamba safari hii ni tofauti; kwamba sauti yao (kura) ndiyo tofauti hiyo.

    Hilo ni jibu ambalo lilisemwa na vijana na wazee, tajiri na maskini, Mwanademokrasia na Mwanarepablika, mweusi, weupe, walatino, Waasia, Wamarekani wazawa, mashoga, wandoa, wenye vilema na wasiyo navyo- Wamarekani waliotoa ilani kwa dunia kwamba kamwe hatukuwahi kuwa halaiki ya Majimbo Mekundu na Majimbo Buluu: sisi ni, na daima tutakuwa Marekani.

    Hilo ni jibu ambalo liliwaongoza wale walioambiwa daima  na wengi mno kwamba wadharau, wawe na woga na wahaka wa kile tunachoweza kufanikisha, kwa kuweka mikono yao kwenye tao la historia na kulipinda mara ingine tena kulielekeza kwenye rajua ya siku bora.

    Imechukua muda mrefu kuja, lakini usiku huu, kutokana na tulichokifanya leo, katika uchaguzi huu, katika pindi isiyo na kifani, mageuzi yamewajihi Marekani.

    Hivi punde nilipokea simu ya hisani kutoka kwa Seneta McCain.  Alipambana kwa dhati, na hata amepambana zaidi kwa ajili ya nchi anayoipenda. Amevumilia kujitolea kwake mhanga, kitu ambacho wengi wetu tunashindwa  kuanza kukiwaza, na tuko na hali bora kwa ajili ya huduma  alizotoa huyu  kiongozi mjasiri na wa moyo msafi. Natoa pongezi kwake na kwa Gavana Palin kwa yote waliyoweza kufanikisha, na natumaini kushirikiana nao katika kufufua ahadi ya nchi hii katika miezi ya usoni.

    Nataka kumshukuru mbia wangu katika msafara huu, mtu aliyefanya kampeni kutoka kwenye moyo wake, na aliyezungumza kwa niaba ya wanaume  aliokua nao katika mitaa ya Scranton na akasafiri nao kwa treni kwenda nyumbani Delaware, Makamu wa rais Mteule wa Marekani, Joe Biden.

    "Nisingekuwa nasimama  hapa usiku huu pasipo na msaada tegemevu wa mwendani wangu kwa miaka kumi na sita iliyopita, jabali la familia  na kipenzi cha maisha yangu, Bi. Michelle Obama mke wa rais mpya.  Sasha na Malia, nanyi nawapenda sana, na mmestahili kupata mtoto mpya wa mbwa ambaye atakuwa nasi kule Ikulu. Na ilihali hayuko nasi tena najua bibi yangu anatutazama, pamoja na familia ambayo imenilea na kunifikisha hapo nilipo sasa.  Ninabakia na shauku ya kuwa nao leo, nikifahamu kwamba deni wanaloniwia  halina kiwango…………………………

    Hata hivyo, juu ya hayo yote,  nisingesahau kutaja wale ambao walistahiki ushindi huu- ushindi huu niwenu".

    Sikuwahi kuwa mgombea aliyetarajiwa zaidi kuliko wote kwa ofisi hii.  Hatukuanza na pesa nyingi, au marafiki wengi wa kutuunga mkono.  Kampeni yetu haikutotolewa katika shoroba za Washington- ilianza katika vichochoro vya Des Moines na sebule za Concord na roshani za Charleston.

    Hotuba hiyo ilisifiwa sana  na watu wengi, na inasemekana kwamba ilisikilizwa na Wamarekani karibu wote, na watu wa nchi geni wengi sana vilevile. Kama kulikuwa na watu ambao hawakusikiliza moja kwa moja waliweza baadaye kuisoma kwenye fasihi mbalimbali za Kiingereza na kwa lugha zingine, tafsiri zake.  Hapa sasa tunayo tafsiri yake  ya lugha ya Kiswahili kama fasili ya kitabu hiki.

    Siyo kila mada ilipata kutajwa katika zile dakika kumi na sita za hotuba. Wakosoaji walionelea kuwa ombwe la kumtaja Mungu lilikuwa kitendo cha kutafakari, hususan likilinganishwa na  hotuba  kama hiyo ya  ushindi wa George W Bush wa mwaka 2000.  Mbali na msemo wa kawaida Mungu awabariki  na Mungu ibariki Marekani, Obama hakuwarejesha watu kwenye mahitaji yao ya sala au ya Mungu. Ilihali, Bush alitoa mwito wa kusali na alisisitiza imani yake kwa Mungu aliposema, Ninayo imani kwamba, pamoja na baraka za  Mungu, sisi kama taifa tutasonga mbele, na akasimulia zaidi imani yake kwa kusema, ninaamini kila kitu hutokea  kwa ajili ya sababu.  Pamoja na hayo, watu wengi waliamini nchi ilikuwa mbioni kwenye mageuzi yaliyotarajiwa kuletwa na hotuba za Obama.

    Hiyo ilikuwa hotuba ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa Novemba 2008, na hivyo Obama alikuwa na kipindi cha kujitayarisha kabla ya kuchukua kiapo cha  ofisi ya rais, ambacho hufanywa daima tarehe 20 Januari ya mwaka uliyofuatia uchaguzi mkuu.

    Kwa mara ya kwanza, Obama na familia yake walianza kujitayarisha kuhamia Washington kwenye anwani ya 1600 Pennsylvania, Avenue, ambayo ndiyo Ikulu ya nchi.  Wakati alipochaguliwa kuwa seneta wa Marekani mnamo mwaka 2004, Obama na familia yake hawakuhamia, bali yeye peke yake alipanga  fleti ndogo karibu na Kilima cha Bunge ambayo alitumia kama maskani kwa siku 3 kwa wiki kwani kila mwisho wa wiki alirudi kwa familia yake kule Chikago.  Safari hii hakuwa na budi; iliwabidi wahamie. Katika hotuba yake ya kiapo cha ofisi ya rais, tarehe 20, Januari  2009, alikuwa na haya ya kusema:

    Raia wenzangu,  nasimama hapa leo nikiwa mnyenyekevu kwa jukumu lililoko mbele yetu, mwenye shukrani kwa imani mliyoniwekea,nikikumbuka wazi wahenga wetu walivyojitolea……….Wamarekani 44 hadi leo wamechukua kiapo cha rais….Swali tunalouliza leo siyo  kama serikali yetu ni  ndogo mno au kubwa mno, bali kama inafanya kazi yake-kama inapatia familia ajira zenye kulipa ujira unaokidhi maisha, huduma za afya wanazomudu, na akiba  stahiki ya kustaafu. Kama jibu ni ndiyo, tunakusudia kusonga mbele. Endapo jibu ni hapana, programu zitakomeshwa. Na wale miongoni mwetu wanaosimamia pesa za wananchi watawajibishwa kuzitumia kwa iktisadi, kubadilisha tabia mbaya, na kufanya shughuli zetu katika mwanga wa siku……….Akigusia sera na siasa ya mambo  ya nje alikuwa  na onyo:   Kwa wale ambao wanabakia kwenye mamlaka kwa ajili ya ufisadi na udanganyifu, na unyamazishaji wa upinzani, mfahamu kwamba mko kwenye upande mbaya wa historia, lakini kwamba, tutakunyoshea mkono iwapo mko tayari kufungua ngumi zenu…………

    Hotuba hiyo kwa nchi  na dunia nzima ilihudhuriwa na watu waliokadiriwa kufikia milioni mbili jijini Washington.  Lakini  pia wengine wote waliobakia makwao waliitazama kwa hamu kwenye runinga, wakaisikiliza kwa lugha ya Kiingereza ambayo asilimia 99 wanaielewa.

     Lakini  kwa sababu kadhaa  wananchi wengi wa nchi nyingi hasa wale wa nchi za bara la Afrika Kusini mwa Sahara, hawapati fursa ya kuwasikiliza viongozi wao kwa lugha wanayoelewa.

    Mnamo mwaka 1960, katika bara la Afrika nchi kubwa ya Kongo iliyokuwa chini ya ukoloni mkatili, kwanza wa mfalme Leopold, uliofuatwa na ukoloni wa serikali ya unyonyaji ya Ubelgiji, ilijinyakulia uhuru wake.  Na baada ya maafikiano kati ya viongozi wenyeji wa wakati ule, Patrice Lumumba alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa nchi huru ya Kongo.  Katika hotuba yake ya kutangaza uhuru kwa watu wake Patrice Lumumba alizungumza kwa lugha ya Kiswahili, na alikuwa na haya ya kusema:

      Mnajua wazi kama kwa siku ya leo, ninyi  nyote kwa kusikia sauti yangu, kwa redio nashanal mtakuwa na furaha tele, sauti ya mtu mwenyeji… Niliapa ya kama mimi nitatumikia ninyi kazi na roho moja pasipo kuogopa……… Leo  imepita miaka mingi, tunaona tabu usiku na jua kwa sababu ya kufukuza maadui yetu na kondosha kati ya nchi yetu Kongo mambo ya kuonelea, mambo ya kuiba vitu vyetu,…. Mambo ya kufunga watu bure pasipo na sababu.. . ..hao tuliamua kufukuza kabisa milele…

    Hotuba hiyo ya lugha ya Kiswahili ilitangazwa kwenye redio nchini kote.  Lakini kwa vile takriban asilimia 45%  tu ya Wakongo  walielewa lugha ya Kiswahili, idadi ya Wakongo walioweza kuelewa maudhui ya hotuba japo muhimu sana haitajulikana kamwe.  Kitu kibaya zaidi ni kwamba hata leo hii nchi hiyo ya Kongo ( na zinginezo barani) bado haina lugha moja  ambayo zaidi ya robo tatu ya watu wake wanaweza kuitumia katika maisha yao ya kila siku.

     Kutumia Kifaransa au Kiingereza, iliyokuwa lugha ya utamaduni wa mkoloni inayozungumzwa na wale wananchi wachache waliopata elimu ya juu, kunafanya idadi kubwa ya wananchi kutoelewa mambo mengi ya taifa lao ikiwa ni pamoja na sera, katiba, sheria na uchumi, nyaraka ambazo zinapatikana  nchini zaidi katika fasihi ya lugha geni badala ya lugha ya taifa anayoelewa kila raia; lakini mbaya zaidi vilevile kwa taifa isiyo na lugha ya utamaduni wake ni uwepo wa yamkini ya wananchi wake kuelewa vibaya au kupotoshwa juu ya sera, hotuba za viongozi, na sheria zinazowahusu  kwa ajili ya ukosefu wa lugha na fasihi inayoeleweka vizuri kwa walio wengi bila kuhitaji tafsiri.

    Mnamo mwaka 1963, nchi ingine ya Afrika,  Kenya iliyokuwa koloni la Uingereza ilijitangazia uhuru wake  baada ya kuupigania na kumwaga damu, na kiongozi wake Jomo Kenyatta alilihutubia taifa lake jipya  kama Waziri Mkuu kwa kutaja maneno ya mhemko kama  haya kitambo tu baada kuanza hotuba yake iliyokuwa katika lugha ya Kiingereza:   Ndugu, nadhani nimezungumza ya kutosha kwa lugha ya kigeni, na kwa maana hiyo lugha ya kikoloni( Brothers, I think I have spoken enough in foreign, and for that matter, a coloni..colonialist language).  Tunataka kutawala nchi yetu!  (We want to rule our country!), aliwekea mkazo.  Mwaka uliofuata wa 1964 Kenya ilichukua uhuru wake  kwenye ngazi ya juu zaidi na kuwa Jamhuri yenye rais kama kiongozi wake.  Mzee Jomo Kenyatta  alichukua wadhifa huo akiwa rais wa kwanza wa jamhuri hiyo mpya. Mzee Kenyatta hakupendezewa hata kidogo na utumiaji wa lugha isiyo ya kienyeji kwa watu wake kwani walioelewa lugha ya Kiingereza walikuwa wachache sana. Wala hakujaribu kusukumiza lugha ya kabila moja kama ndiyo lugha ya taifa kwa raia zake. Hata hivyo alijaribu sana kutumia lugha ya Kiswahili kila alipohutubia wananchi hasa akianzia na salamu yake maarufu ya Harambee!.  Na katika enzi ya utawala wake lugha ya Kiswahili ilishamiri ikichukuliwa kama ndiyo lugha ya taifa, na taifa la Kenya likaanza kuimarika dhidi ya ukabila uliotumiwa na wakoloni kuwatenganisha.  Lakini zimwi la ukabaila lilianza kilinyemelea taifa la Kenya  baada ya Mzee Jomo Kenyatta kuhitimisha maisha yake na kuwaachia viongozi wengine hatamu ya uongozi.

    Kenya na Tanzania, na pengine  maeneo mengine hasa ya mijini ya Uganda, Rwanda, jamhuri ya Kongo, na Burundi zimeneemeka kwa kuwa na lugha moja ya wengi- Kiswahili ambacho karibu kila mwananchi anaielewa kwa kiasi fulani.  Vile vile nchi za jirani kusini na kusini magharibi ya Tanzania wameneemeka kwa watu wao kuwa na welevu fulani wa Kiswahili.  Nchi za Kusini mwa bara hadi Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Namibia, Angola na Msumbiji ambazo viongozi wao walitumia Tanzania kama makimbilio ya na kitovu cha vita vyao dhidi ya ukoloni vimepata athari nzuri fulani za lugha ya Kiswahili.

     Lakini nchi nyingine za Afrika hasa Afrika ya Magharibi, hazikubahatika na lugha moja ya kimataifa ambayo inafahamika kwa watu wengi mithili ya Kiswahili.  Kwa nchi kama hizo, ile lugha aliyoiita  Mzee Jomo Kenyatta, lugha ya kikoloni ndiyo imekuwa lugha rasmi ya taifa kwa mataifa mengi ya Afrika hasa Afrika ya Magharibi.  Kutokana na hali hii ya fasihi za lugha ambazo  ni sehemu muhimu ya utamaduni wa watu kuishi nje ya utamaduni wa taifa, nchi zinazotumia lugha za nje kama lugha rasmi daima zitakuwa na changamoto za kuelewana wenyewe kwa wenyewe katika mambo yanayohusu  ubia  wao kama taifa moja.

    Kwa namna  wakoloni  Waingereza walivyotumia ukabila kwa minajili ya kuwatenganisha Waafrika wakati wa ukoloni, ilikuwa vigumu kwa nchi nyingi za Afrika chini ya Uingereza kuchukua lugha ya kabila moja na kuifanya iwe lugha rasmi ya taifa.  Hivyo wakati wa ujio wa uhuru na kuibuka kwa taifa jipya, ilikuwa rahisi kuchukua lugha ya Kiingereza kuwa ndiyo lugha rasmi mintarafu ya lugha ya taifa jipya ili kuepukana na mstakabali wa kabila moja kuchukua kipaumbele ya aina yoyote juu ya wenzake.

      Lakini kwa bahati mbaya maamuzi hayo  yaliambatana na dosari moja kamambe: kwamba wakati huo wa uhuru  wananchi nusura wote, isipokuwa wachache waliopata fursa ya elimu wakati huo, hawakuelewa vizuri lugha hiyo ya kigeni.  Kwa hivyo siyo jambo la kushangaza kumaizi kuwa wananchi hawakuelewa  mengi yaliyokuwemo kwenye fasihi za lugha ya Kiingereza, yawe maandishi au maongezi ya hotuba ambayo yanahusu maamuzi juu ya maisha yao. Katika fasihi muhimu zilizoko kwenye lugha ya kigeni ni pamoja na katiba, ya nchi, azimio la uhuru, sheria  za kila aina na hata amri mbalimbali za serikali.

    Huko Afrika ya Magharibi nchi nyingi zaidi zilikuwa chini ya himaya ya Ufaransa ambayo ilikuwa na mtindo wake maalumu wa kuwatawala wazawa wa hapo.  Ufaransa iliweka  lugha ya Kifaransa kama ruwaza ya kuigwa na wenyeji, endapo wangetamani kulingana na Wafaransa. Na walimaanisha hiyo ari yao ya kuwastaarabisha Waafrika, kwani wengi walitopea kwenye lugha hiyo walitambuliwa hata kule Ufaransa kwa umahiri wao. Hivyo Kifaransa kilizingatiwa sana kupitia nyanda za elimu na utawala, na matokeo yake sasa yanatishia kumeza tamaduni mbalimbali za hapo hususan katika fasihi za lugha. Kwa Mwafrika aliyesoma na aliye na ufasaha wa lugha ya Kifaransa kishawishi cha kuandika waraka au makala, au hata kitabu kwa minajili ya kuchapishwa, katika lugha ya Kifaransa ni kikubwa mno  kukiepa japo wasomaji wazawa wa fasihi hizo watakuwa wachache sana ikilinganishwa na idadi ya watu katika jamii ya kawaida ya Kiafrika. Mtanziko huo unaimarika hasa wakati hakuna lugha ya wenyeji inayoweza kueleweka kwa upana na kina  kushabihia Kifaransa.

    Hali hiyo ya nguvu ya lugha ya Kifaransa kwa waliokuwa watawaliwa wake imejisambaza  hata huku Marekani Waafrika walikofikia kama wahamiaji.  Hadithi ya watalii Wafaransa wawili ( Wazungu) waliotembelea jiji la Washington na vitongoji vyake vya majimbo ya Maryland na Virginia hivi karibuni inatuwekea bayana ishara za nguvu ya lugha ya Kifaransa kwa Waafrika wa Magharibi ya bara.

     Mathalan, katika ibada za makanisa ya hapa Marekani kuna ibada za lugha mbalimbali hasa kwenye parokia za Kanisa Katoliki. Lugha zinazotumika zaidi, kama tunavyojua bila shaka ni Kiingereza, ambayo ndiyo lugha rasmi ya Marekani na yenye fasihi nyingi kote duniani kuliko zote; kuna lugha  ya Kihispania ambayo ni utamaduni wa watu wa Amerika ya Kusini walio na historia ndefu na watu wa nchi ya Hispania ya Ulaya ya kale; na kuna lugha ya Kifaransa, na zinginezo.  Wafaransa hao wawili,  tuwaite Claude na Marie, ni  Wakristo wa dini Katoliki;  kabla ya kuondoka kwao Paris, waliambiwa kwamba makanisa ya Marekani yanayo ratiba za ibada zao katika lugha mbalimbali ikiwemo ibada ya Kifaransa. 

    Hivyo Claude na Marie alipofika Marekani, walipata kabrasha la ratiba ya kanisa moja  upande  wa Maryland na haikuwa masafa marefu kutoka kwenye hoteli yao. Walikuwa wakitarajia kwamba watu wa ubalozi wao pengine na watalii kama wao kutoka Ufaransa wangekuwepo pamoja na Wamarekani wa asili ya Kifaransa.  Walikuwa wamechelewa kidogo na hivyo walipofika karibu waumini wote walikuwa wameshaingia ndani na ibada ilikuwa imeanza pindi fupi. Walisali wote pamoja, wakaimba wote pamoja, na hata wakasalimiana na kutakiana baraka na waumini wengine kwa lugha yao ya Kifaransa.  Lakini hawakuwahi kuona katika maisha yao, shamla kama hiyo ya waumini waliogeuza kanisa kuwa penye shangwe ya kumburudisha mfalme.

    Baadaye walipokuwa wakisimulia hiyo safari yao ya kanisani, kitu cha ajabu walichotaja haikuwa kwamba walienda kwenye kanisa la madhehebu mengine. La ; bali waumini waliowakuta  nusura wote walikuwa  weusi wa asili ya Afrika ya Magharibi na ya Kati- maeneo ambayo yalitawaliwa na Ufaransa. Ibada ilikuwa nzuri na iliongozwa na kasisi naye alikuwa wa asili ya Afrika.  Japo fasihi zilizotumika zilikuwa za Kifaransa, pamoja na injili na sehemu zingine za bibilia, vitabu vya nyimbo, na hata mahubiri  yalikuwa katika lugha ya Kifaransa. Claude na Marie walihitimisha kuwa lazima hawa waumini wote wamesoma sana  kwa ustadi wao wa kuelewa Kifaransa kiasi hicho.  Pamoja na hayo, ndani yake kulikuwa na utamaduni fulani wa Kiafrika, hasa katika nyimbo za kwaya.

    Baada ya kusema hayo yote juu ya umuhimu wa lugha na fasihi zake, naweza kurejea kwenye madhumuni ya Nyayo Obama katika kitabu hiki.  Kama nilivyosema hapo nyuma, maudhui na mazingira  ya kitabu siyo mageni hasa katika fasihi za lugha maarufu kama Kiingereza, Kifaransa, na pengine Kijerumani. Bali yameandikwa katika lugha ya Kiswahili,  ambayo ni lugha rasmi  na  inayozungumzwa kote nchini Tanzania; kuanzia visiwani hadi mwambao wa ziwa Tanganyika, masafa ya maili elfu na zaidi, kando kando ya ziwa Victoria, kuzungukia mlima Kilimanjaro, hadi mto Ruvuma kule kusini Tunduma kwenye mpaka na nchi ya Msumbiji, na kwenye mipaka na nchi za Zambia, Malawi na jamhuri ya Kongo.  Kote huko Kiswahili ndiyo lugha ya wengi, pengine pamoja na lugha za makabila ambazo zimeanza kudorora katika kila kizazi kipya.  Kwa hivyo kinadharia yaliyomo kwenye kitabu hiki, juu ya rais Barack Obama na nchi ya Marekani anayoitawala yanaweza kusomwa na karibu kila Mtanzania anayeweza kusoma a, e, I, o, u.

    Mlimbuko huo wa lugha ya Kiswahili wa Tanzania haukutokea kwa ajali, kwani wakati wa uhuru wake Tanzania ilikuwa  na watu waliojumuika katika matapo ya makabila zaidi ya 200, kila moja ikiwa na lugha yake pekee. Kiongozi mpya wa taifa jipya, Julius Nyerere wala hakutoka kwenye kabila kubwa au mashuhuri zaidi wakati huo.  Julius Nyerere kwa kila aina ya tathmini alikuwa kiongozi wa hekima kubwa na aliyekuwa na dira ya bara lote la Afrika na alitambua mara moja umuhimu wa lugha kama sehemu muhimu ya kujenga, kwanza taifa lake changa na utamaduni wake, na halafu kutumia utamaduni huo wa kuongozwa na lugha kwenye kufikia mstakabali wa mwungano wa nchi zote huru za Afrika.  Dira hiyo japo halikuhitimisha mlimbuko wake, hata hivyo ilipata msingi ndani ya lugha ya Kiswahili kwa kuitawaza kama lugha ya taifa na kutekeleza uamuzi huo kwa dhati.

    Nchi zingine ambazo ziko katika utamaduni wa fasihi ya lugha ya Kiswahili kwa viwango tofauti ni Kenya, hasa wenyeji wa mwambao wa bahari ya Hindi, wanaoishi mijini,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1