Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa
Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa
Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa
Ebook211 pages2 hours

Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa

Rating: 1 out of 5 stars

1/5

()

Read preview

About this ebook

Wachungaji wanashinikizwa kuwafurahisha na kuwapendeza washirika wao kwa habari njema. Shinikizo hii ya watu imesababisha kubadilisha kwa maneno ya Kristo mpaka imekuwa vigumu kutambua ujumbe wa msalaba. Leo, tunarudi kwa ukweli wa msingi wa Ukristo kwamba tunapaswa "kupoteza" ili "kumpata" Kristo. Nguvu itarudi katika kanisa kadiri tunavyohubiri kwamba tunapaswa kujitoa dhabihu, kuteseka na kufa kwa ajili ya Kristo. Nguvu ya maneno ya Kristo haiwezi kuondolewa na mtu yeyote hata kama amefanikiwa au ni mtu wa nguvu namna gani.

LanguageKiswahili
Release dateJul 26, 2016
ISBN9781613954232
Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa

Related ebooks

Reviews for Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa

Rating: 1 out of 5 stars
1/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kupoteza, Kuteseka, Kujitoa Dhabihu Na Kufa - Dag Heward-Mills

    Kama Mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

    Luka 14:26

    Kumfuata Yesu siyo jambo rahisi. Kuishi kwa ajili ya Kristo siyo rahisi. Usimwamini mtu yeyote anayeleta tafsiri ya uongo ya Ukristo kwako. Ukristo ni kumfuata Yesu Kristo katika mambo yote na kufanana naye!

    Mambo yote Yesu aliyoyasema kuhusu kuwa mwanafunzi wake, kwa ujumla yanaonekana kama vile hakutaka mtu yeyote amfuate. Aliwaonya watu mbalimbali waliojaribu kumfuata juu ya hatari nyingi zitakazowakabili katika kumfuata Yeye.

    Yesu Anatuonya

    Alisema, Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu (Luka 14:26).

    Alimwambia mtu tajiri aliyetaka kumfuata: Kama unataka kunifuata ni lazima uuze vyote ulivyo navyo (Mathayo 19:21).

    Pia alisema, Kama ukinifuata hutakuwa na mahali pa kuishi kwa sababu sina hata nyumba ambazo mbweha na ndege wanazo (Luka 9:58).

    Alisema, Kama kweli unataka kunifuata ujue kuwa hutaweza kuwaaga watu wa familia yako (Luka 9:61).

    Alimwambia mtu mmoja ambaye wazazi wake walikuwa wamekufa, Kama kweli unataka kunifuata, hutahusika katika kumzika baba yako (Luka 9:59)

    Yesu Hashushi Viwango vya Mtu Yeyote

    Ni dhahiri kabisa, Yesu hakukusudia kufanya mambo yawe rahisi kwa mtu yeyote. Wala hakushusha mnara wa mtu yeyote. Hakumtendea mtu yeyote kwa upendeleo maalumu. Alijua alikuwa anatualika kwenye upendeleo mkuu ambao haujatolewa kwa mwanadamu yeyote. Upendeleo huo ni wa kuokolewa kwa damu ya Yesu, kumjua Mungu, kwenda mbinguni!

    Maonyo haya ya Yesu Kristo hayavunji moyo mamilioni ya watu ambao wanaitikia kwa haraka pendo lake lenye kicho. Watu mailioni wanampenda Yesu Kristo bila kujali hali ngumu alizoziweka kwa ajili ya kumfuata.

    Hata hivyo, kumjua Mungu aliye hai na Mwana wake Yesu Kristo ni zaidi kuliko fidia inayotosha kufidia kwa ajili ya mambo magumu tunayopitia.

    Usimsikilize mtu yeyote anayedai kwamba kumfuata Yesu ni kubarikiwa katika mambo yote, au kuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio. Kamwe huo siyo Ukristo. Ukristo unahusu kupoteza, kujitoa mhanga, kuteseka na kufa.

    Dhiki na magumu yanayowakabili Wakristo wote yanaweza kupangwa katika makundi makuu manne: kupoteza, kujitoa mhanga, kuteseka na kufa.

    Mambo haya ni ahadi nne za kiroho ambazo Wakristo wote lazima watazamie kwa sura moja au nyingine. Hakuna hata mmoja anayemfuata Yesu kweli atakayeepuka ahadi hizi nne.

    Usichukue taarifa ya mtu yeyote anayekuambia vinginevyo! Huyo anakuna tu masikio yako yanayowasha. Katika umbo moja, sura moja au nyingine, labda kwa jina tofauti, ni lazima utapitia msalaba wa Yesu Kristo kama kweli wewe ni mwanafunzi wake.

    Ahadi zetu nne ni kupoteza, kujitoa mhanga, kuteseka na kufa. Je, ahadi hizi ni za kiroho? Ndiyo, Maandiko hapo chini yanatuonesha jinsi tunavyokusudia kupoteza, kuteseka, kujitoa mhanga na kufa kwa sababu ya imani yetu, wito wetu na makusudi ya kiroho.

    Kitabu hiki kimekusudia kuonesha jinsi ahadi hizi za kweli zilivyo. Si vibaya kama unavyoweza kuwaza lakini mwishoni itageuka kuwa baraka. Tilia maanani jinsi Maandiko hayo hapo chini yanavyoorodhesha wazi ahadi hizi kwetu sote.

    1. Umeahidiwa kukutana na hasara na kupoteza

    Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atalkayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

    Mathayo 16:25

    Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwaajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo.

    Wafilipi 3:7-8

    Kwa ajili ya Kristo utapitia ahadi kwa hasara na kupoteza. Hii ina maana zaidi kwa mtu yeyote anayejali na kutafakarikuhusu jambo hili.

    a.       Hasara maana yake kwa hakika utakuwa huna kitu. Inawezekana vikawepo vitu vichache au hakuna matazamio ya kurejesha vitu utakavyopoteza.

    b.      Hasara maana yake utateseka kwa kunyang’anywa kila kitu.

    c.       Hasara maana yake hutaweza kutunza au kuendeleza kitu chochote katika maisha yako.

    d.      Hasara maana utaacha na kunyang’anywa kila kitu unachokimiliki.

    2. Umeahidiwa Kukutana na Mateso

    Kwa sababu ya Kristo utapitia ahadi kwa kuteseka. Hii ina maana zaidi kwa mtu yeyote ambaye anajali kutafuta nini hasa maana ya kuteseka. Usichukue taarifa za watu ambao hawaingizi wazo la kuteseka katika kutembea kwao kwa imani. Watu wote wakuu wa imani waliteseka kwa sababu walimwamini Mungu.

           a. Kuteseka maana yake utapatwa na maumivu mara kwa mara, dhiki, hasara,

                 kuumizwa na mambo yasiyopendeza.

           b. Kuteseka maana yake utapitia shida, misuguano, ugumu wa mambo na umaskini

               katika maisha yako.

           c. Kuteseka maana yake utatembea kwa kupitia misiba, kutofarijiwa na matatizo.

           d. Kuteseka maana yake utaumizwa vibaya, utachoshwa na kukutana na shida.

    Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na KUTESWA kwa ajili yake; mkiwa na mashindano yale yale mliyoyao na kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.

    Wafilipi 1:29-30

    Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu, mtu asifadhaishwe na dhiki hizi, maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa TUMEWEKEWA HIZO.

    Kwa maana tulipokuwapo kwenu TULITANGULIA KUWAAMBIA KWAMBA TUTAPATA DHIKI; kama ilivyotukia, nanyi mwajua.

    Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili nijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida. 

    1 Wathesalonike 3:2-5

    Wakifanya imara roho zawanafunzi na kuwaonya wakae katika ile imani, nay a kwamba imetupasa KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU KWA DHIKI NYINGI.

    Matendo ya Mitume 14:22

    3. Umeahidiwa kukutana na kujitoa mhanga

    Kwa ajili ya Kristo utapitia ahadi kwa kujitoa mhanga. Hii ina maana zaidi kwa yule anayejali kutafuta ili kujua kujitoa hasa maana yake nini. Tafadhali usiwasikilize Wakristo wasiohubiri kuhusu kujitoa kunakotakiwa kufanywa nasi kama Wakristo. Kujitoa mhanga ni sehemu ya dini tuliyo nayo.

    a.       Kujitoa mhanga maana yake ni kutoa kwa Mungu zana unazomiliki kwa ajili ya kuabudu.

    b.      Kujitoa mhanga ni kuachilia kitu chenye thamani au kinachohitajika kwa ajili ya kitu kingine chenye thamani ya juu zaidi.

    c.       Kujitoa mhanga ni kuruhusu kuumizwa au kupata hasara kwa ajili ya kitu kingine.

    d.      Kujitoa mhanga ni kutoa mali zako bila kujali ukweli kwamba hupati faida yoyote.

    Basi, ndugu zangu nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu,ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenmye maana.

    Warumi 12:1

    Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani tundala midomo iliungamayo jina lake.

    Waebrania 13:15

    4. Umeahidiwa kukutana na kifo

    Kwa ajili ya Kristo utapitia ahadi ya kufa. Kule kusema kwamba tutakufa ina maana nyingi. Hii ndiyo sababu Yesu alituambia kubeba misalaba yetu na kumfuata.

    a.       Kufa maana yake ni kukoma kuonekana na kutofanya kitu chochote.

    b.      Kufa maana yake ni kupoteza nguvu na uwezo.

    c.       Kufa maana yake ni kupita polepole au kupotea kabisa  kidogo kidogo.

    d.      Kufa maana yake ni kusimamishwa moja kwa moja.

    Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike, MSALABA wake kila siku anifuate.

    Luka 9:23

    NIMESULIBIWA PAMOJA NA KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu;na uhainilio nao sasa katika mwili, ninao katika imanai ya Mwana wa Mungu ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

    Wagalatia 2:20

    Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, NINAKUFA KILA SIKU.

    1 Wakorintho 15:31

    Sehemu ya 1

    KUPOTEZA

    Sura ya 2

    Jinsi ya Kutekeseka kwa Hasara kwa Ajili ya Kristo

    Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepta hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo.

    Wafilipi 3:8

    Lazima ukubali kupoteza kila kitu kwa ajili ya Yesu Kristo kama vile Paulo alivyofanya. Paulo aliteseka kwa kupoteza vitu vingi. Ikiwa hutapoteza ujue hutaweza kupata. Wanafunzi kumi na mbili wa Yesu walipoteza kila kitu kwa sababu walimfuata Yesu. Waliacha vyote! Walipoteza weledi wao, familia zao na marafiki zao kwa kumfuata Yesu. Jambo hili kwao lilikuwa ni hasara kubwa kwa mtu binafsi. Huwezi kumfuata Yesu mpaka umekuwa tayari kupoteza kitu chochote.

    Petro akaanza kumwambia, TAZAMA, SISI TUMEACHA VYOTE, tukakufuata wewe.

    Marko 10:28

    Huduma yako ina mipaka kwa sababu ya mambo unayoyatunza. Kama unabeba vitu fulani unapokimbia, hutakimbia kwa haraka inavyotakiwa. Mungu anatutazamia kuwa tutaacha mambo yote na kumfuata Yeye. Katika kumfuata Yesu tunatakiwa tuache usingizi wetu, marafiki zetu, luninga zetu, amali zetu, na kazi zetu.

    Lazima Upoteze Fedha Zako

    Kuingia katika huduma inahusisha kupoteza fedha. Unapoingia katika huduma utapoteza mambo ya kifedha. Pia Wachungaji wengi hawatambui kwamba watatoa fedha zao kwenye huduma. Kila mtumishi lazima awekeze binafsi kwenye huduma. Kwa hakika, huwezi kufanya hivyo ikiwa fedha yako  haikutenganishwa na fedha ya kanisa.

    Ni jambo la maana kwamba mali unazomiliki mwenyewe zitenganishwe na mali za kanisa. Ikiwa kutenganishwa huku hakuko wazi, unapoteza baraka za utopaji. Utakuwa huna cha kutoa kwa sababu mali zote ulizo nazo ni za kanisa. Na ni jinsi gani unaweza kutoa kwa kanisa vitu ambavyo ni vyake.

    Lazima Upoteze Faraja Zako na Hali yako Njema

    Usipojitolea muda wako wa mapumziko ili kuwa na Bwana, hakutakuwa na matunda halisi. Watumishi wengi wana muda kwa kila jambo lakini si kwa Bwana. Kuna wakati wa luninga, kurafikiana kusiko na maana, kompyuta, biashara na michezo lakini hakuna muda wa ushirika binafsi na Bwana. Huduma yako ni kitu kinachoakisi muda wako mwenyewe na Bwana.

    Kuna mambo mengi katika huduma, ambayo yanaweza kuondoa faraja zako. Kama hukujiandaa kutoa mambo madogo madogo ya maisha, hutaweza kamwe kutoa zaidi katika huduma.

    Kusisitiza juu ya faraja Fulani katika ulimwengu huu inaweza kuwa sababu ya kutokusonga mbele katika huduma. Unatakiwa uweke upendo juu ya mambo yaliyo juu, si katika mambo ya duniani (Wakolosai 3:2). Moyo wako unapouweka katika mambo yaliyo juu, hutahangaika kuhusu mambo ya dunia hii.

    Usiku mmoja, nilikuwa nimesimama karibu na Bahari ya Pasifiki katika nchi ya kigeni. Mbele yangu kulikuwa na boti kubwa kadhaa zenye gharama zilizomilikiwana watu milionea. Nikawageukiwa Wakristo waliokuwa wanatembea pamoja nami na kusema, Ninataka kuwa na boti yangu mbinguni.  Mmojawao akanicheka na kusema, Oh hapana, ninataka niwe na boti ya kwangu hapa hapa.Mazungumzo haya mafupi yaliakisi mawazo mawili ya kujifunza leo. Wakristo wengi wanataka wawe na faraja zao hapa, wakati wachche wao wanazitaka faraja hizo watakapofika mbinguni.

    Sikuendesha gari ambalo hasa nilitaka kuliendesha. Kwa kweli, sikuwahi kuendesha kamwe gari ambalo hasa nilipenda kuliendesha. Ninafahamu ni aina gani ya gari ambayo ni nzuri na bora lakini ninaafanya yale ninayoyafanya kwa ajili yahuduma.

    Lakini mimi sikutumia mambo hayo hata moja. Wala siyaandiki hayo ili iwe hivyo kwangu mimi; maana ni heri nife kuliko mtu awaye yote abatilishe huku kujisifu kwangu.

    1 Wakorintho 9:15

    Siishi katika nyumba bora au katika

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1