Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri
Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri
Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri
Ebook208 pages2 hours

Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Watu wengi wanahangaika na dhana ya utoaji zaka ingawa zoezi hili la zamani limepelekea utajiri unaofahamika wa Wayahudi. Katika kitabu hiki, Askofu Dag Heward-Mills anafundisha namna utoaji zaka unavyowakilisha kanuni za utengenezaji utajiri na muujiza wa mafanikio. Furahia moja ya juzuu ya kiwango cha juu ya Dag Heward-Mills.

LanguageKiswahili
Release dateJul 26, 2016
ISBN9781613954249
Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri

Related ebooks

Reviews for Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kwa Nini Wakristo Wasiotoa Zaka Huwa Maskini ... Na Jinsi Wanatoa Zaka Wanavyoweza Kuwa Matajiri - Dag Heward-Mills

    Sura ya Kwanza

    Sababu Sita Zinazowapelekea (Zinazowafanya) Wasiotoa Fungu la Kumi (Zaka) Kuwa Maskini

    1.    Wasiotoa fungu la kumi huwa maskini kwa sababu hawana cha kuvuma.

    KWA MAANA WAO HUPANDA UPEPO, NAO WATAVUNA TUFANI; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.

    Hosea 8:7

    Mafanikio katika uhalisia wake hutokana na mtu kupanda mbegu na hatimaye kuvuna mavuno. Kwa hiyo, kutokutoa fungu la kumi (Zaka) kunakutenganisha na kanuni hii ya msingi kabisa ya kupanda na kuvuna. Ikiwa hutoi mafungu yako ya kumi/Zaka zako unaathiri fedha zako kwa sababu unaondoa/unaweka pembeni misingi mikuu ya mafanikio.

    2. Wasiolipa fungu la kumi (Zaka) huwa maskini kwa sababu hawavuti baraka kwenye maisha yao.

    LETENI ZAKA KAMILI ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na KUWAMWAGIENI BARAKA, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

    Malaki 3:10

    Kutoa fungu la kumi (Zaka) kunavuta aina mbalimbali za baraka kwa sababu Neno la Mungu ndivyo linavyosema. Mtu aliyebarikiwa hupata kibali na kusaidiwa. Maisha yetu hapa duniani ni magumu sana. Farao alipomwuliza Yakobo habari za maisha yake alisema Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi? Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; SIKU ZA MIAKA YA MAISHA YANGU ZIMEKUWA CHACHE, TENA ZA TAABU, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao. (Mwanzo 47:9).

    Ayubu pia alisema kwamba siku za mwanadamu ni chache, nazo zimejaa tabu. Hata pasipo laana fulani katika maisha yako, bado utakumbana na matatizo mengi na tabu nyingi. Kama hutoi fungu la kumi (Zaka) hutakuwa na baraka za kupambana na matatizo yaliyopo ya maisha haya. Unawezaje kuendelea vizuri katika maisha kama hakuna Neno la baraka lililotamkwa juu ya maisha yako ya tabu? Usishangae kuona umaskini unaongezeka katika maisha yako kama hutoi fungu la kumi (Zaka). Baraka zinazotajirisha ambazo hazichanganywi na huzuni huja kwa wingi juu ya maisha ya mtu anayetoa fungu la kumi (Zaka).

    3. Wasiotoa fungu la kumi huwa maskini kwa sababu wamelaaniwa.

    Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. NINYI MMELAANIWA KWA LAANA; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

    Malaki 3:8-9

    Kuna laana maalumu kwa ajili ya watu wasiotoa fungu la kumi (Zaka). Ni moja kati ya laana ishirini na tano hapa duniani. Laana hii inayowapata wasiotoa fungu la kumi huja kuongezea aina nyingine nyingi za laana tulizorithishwa kuanzia kwa Adamu, Nuhu pamoja na vizazi vingine. Laana ya watu wasiotoa fungu la hutenda kazi kipekee kwa kujumulishwa pamoja na laana ambazo wazazi wako na mababu zako wamejinunulia kwa ajili yao wenyewe na vizazi vyao vinavyofuata. Karibu sisi sote ni wafuasi wa watu ambao walilaaniwa kwa sababu moja au nyingine kupitia mambo waliyoyafanya.

    Siku moja, nilipatwa na hofu kubwa pale nilipogundua kwamba kuna uwezekano mkubwa kabisa mababu zangu walikuwa wafanya biashara ya utumwa. Niligundua kuwa kulikuwa na ngome ya kale iliyokuwa imejengwa katika mji aliozaliwa baba yangu mzazi ambayo bila shaka ilikuwa ikitumiwa wakati wa biashara ya utumwa kwa hakika. Mimi nilitokana na uzao wa mtu ambaye hakuwa ameuzwa utumwani. Kwa hiyo basi mimi inawezekana kabisa nilitokana na uzao wa mtu aliyemwuza baba yake, kumwuza baba yako lazima kutailetea laana familia yako. Umeshawahi kujiuliza maeneo ambayo watu waliwatoa ndugu zako kwa kubadilishana vito vya thamani (madini) na vioo vya kujitazamia hivi sasa ndiyo maeneo yaliyokumbwa na umaskini mkubwa kuliko maeneo mengine yote duniani?

    Kutokulipa fungu la kumi kunakuletea laana ya ziada iliyo hatari zaidi juu ya maisha yako. Usije ukasahau kwamba tayari una taabika chini ya laana ya Adamu. Pia, bado unapambana na laana ya Hamu, kama wewe ni wa uzao wa Hamu.

    RAFIKI YANGU MPENDWA, NI JAMBO GANI LA ZAIDI UNALOWEZA KUFANYA? JE! HUU SI WAKATI ULIOAMRIWA KUFANYA KILE AMBACHO KITAKULETEA BARAKA? Unahitaji baraka ya mtoa Zaka ili kuzuia laana hizi zote zilizo hatari! Je, si jambo la kushangaza unapoona ya kwamba unazidi kuwa maskini kadri unavyokataa kulipa fungu la kumi?

    4. Watu wasiolipa fungu la kumi huwa maskini kwa sababu waharabu hula mali zao wakati wote.

    NAMI KWA AJILI YENU NITAMKEMEA YEYE ALAYE, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

    Malaki 3:11

    Baraka iliyo kubwa zaidi kwa wewe unayetoa fungu la kumi ni kwamba Mungu humkemea yeye alaye (mharabu) kwa ajili yako. Ukiwasikiliza viongozi wa serikali kutoka katika nchi maskini, unapata picha kwamba kama wangepata fedha kidogo tu ya ziada matatizo yao yangeisha. Kwa bahati mbaya sana, hali halisi haiko hivyo. Ukweli ni kwamba yale maeneo ambayo yanapata misaada mingi ya kifedha ndiyo yanayobakia kwenye umaskini. Hali hii ya utata inakuwepo kwa sababu ya wale wanaopokea misaada kukosa uwezo wa kutunza fedha wanayopokea.

    fikiri ungehitaji kitu gani kujaza ndoo iliyo na mashimo mengi? Kama utajiri ungekuwa una maana ya ndoo iliyojazwa maji, kwa vyovyote ungehitaji maji mengi zaidi kuijaza ndoo hiyo. Lakini kama yale mashimo yangezibwa basi ungehitaji kiasi kidogo tu cha maji kuijaza ndoo hiyo.

    Hii ndiyo baraka ya ajabu itokanayo na mharabu kukemewa. Baada ya mharabu kukemewa, utahitaji kiasi kidogo tu kukufanya wewe kuwa mtu tajiri. Kama huna baraka ya aina hii, basi utatafuta kazi nzuri na kupata fedha nyingi lakini wakati wote utashindwa kuwa tajiri. Lakini pale ambapo mharabu amekemewa, inawezekana kabisa usipate fedha nyingi, lakini ndoo yako wakati wote itajaa kwa haraka na mara itaanza kujaa na kufurika.

    Rafiki mpendwa, hili ndilo Mungu anaahidi kukufanyia endapo utakuwa unatoa fungu la kumi.  Ondoka kwenye umaskini  leo nawe utapokea baraka ya yeye ambaye mharabu wake amekemewa. Umeshawahi kujiuliza kwanini watu wanakuwa wanene wanapofikia katika umri wa utu uzima? Mara nyingi huwa hawali sana. Ukweli ni kwamba watu katika umri wa utu uzima hujinyima chakula ili wapungue uzito lakini bado utakuta wanazidi kuwa wanene. Je, sababu za kuongezeka uzito ni nini? Kadri watu wanavyozidi kuongezeka umri mfumo mchakato wa kikemikali unaobadilisha chakula ili kitumike kwa ajili ya kukuza kiumbe (Metabolism) hupungua kasi yake ya utendaji kazi. Kwa maneno mengine, ule moto unaochoma mafuta hupungua kasi yake. Kama ule moto unaochoma mafuta mwilini (Metabolic fire) uliokuwa na uwezo wa kuunguza  uniti kumi za mafuta kila siku, inaweza kupungua hadi kufikia uniti tano.

    Ghafla, unaanza kuwa na ongezeko la ziada ya mafuta uniti tano kila siku. Bila jitihada zozote unajikuta umeongezeka uzito na kuwa mpana na mwili kuongezeka. Ndiyo maana ni rahisi kuujua umri wa mtu kutokana na ukubwa wa umbo lake. Kadiri unavyozidi kuongezeka umri, moto unaochoma mafuta hupungua kasi yake (mharabu anakemewa) na ndipo kuongezeka uzito (Mafanikio) hutokea.

    Kwa hakika, wasiotoa fungu la kumi wanazidi kuwa maskini kwa sababu ya kuwepo kwa waharabu ambao hawajashughulikiwa katika maisha yao.

    5. Wasiotoa fungu la kumi huwa maskini kwa sababu matunda ya mashamba yao huharibiwa wakati wote.

    Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, WALA HATAHARIBU mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

    Malaki 3:11

    Hasara isiyo na maana ya yale uliyoyapata kwa kutapanya, usimamizi mbovu, upuuziaji/kutojali, moto, ajali, vurugu, wizi na hata vita inaumiza lakini ukweli ni kwamba yote hayo ni kazi ya mharabu.

    Moja kati ya baraka zilizo kuu ni ile ya kukemewa kwa alaye. Yeye alaye ni ndugu wa mharabu. Tofauti iliyopo kati ya yeye alaye na mharabu ni kwamba mharabu  huchukua utajiri wako kwa namna ambayo ni ya maumivu makali na bila huruma. Inaumiza zaidi kuona mharabu akiwa kazini kwa sababu huoni maana katika hasara unayoipata. Anza kutoa mafungu yako ya kumi na Mungu ameahidi kumkemea yeye alaye.

    6. Wasiotoa fungu la kumi huwa maskini kwasababu hupoteza matunda yao kabla hawajapata nafasi ya kuvuna.

    Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu HAUTAPUKUTISHA MATUNDA YAKE KABLA YA WAKATI wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

    Malaki 3:11

    Sababu nyingine inayowafanya wasiotoa fungu la kumi kuwa maskini ni kwamba matunda ya mavuno hupotea kabla hawajapata nafasi ya kuyavuna. Wasiotoa fungu la kumi wamelaaniwa kwa laana ya mavuno yaliyoshindikana. Mavuno yaliyoshindikana maana yake ni kushindwa kuvuna mavuno yenye uwiano na kile ulichowekeza.

    Mtu moja aliwahi kufundisha kwa ujasiri kabisa kwamba kama ungefanya kazi kwa bidii ungelikuwa tajiri. Akaendelea kusema, "Watu ambao si matajiri hawafanyi kazi kwa bidii. Watu waliopo katika nchi zinazoendelea wanapaswa tu kukunja mashati yao ya mikono mirefu na kufanya kazi na utajiri utakuwa ndio fungu lao.

    Lakini ukiangalia huku na kule, utagundua kwamba watu wengi wanafanya kazi kwa bidii sana lakini si matajiri! Utaona watu ambao wanafanya kazi kwa masaa kumi na mbili bila kupumzika lakini wanaambulia kipato kidogo sana- karibu sawa na hakuna. Wakati ambapo maili chache kutoka hapo walipo, utakuta watu ambao hufanya kazi kwa saa moja tu kwa siku lakini wanapokea mamilioni.

    Ni kweli kwamba, kufanya kazi kwa bidii kunapawa kutupelekea kupata mafanikio lakini mara nyingi haiwi hivyo. Dereva wa basi kule Sweden anapata kipato kikubwa cha  mara kumi na tisa zaidi ukilinganisha na dereva mzuri wa basi katika nchi ya Ghana (mwenye sifa zinazolingana na yule wa Sweden)

    Kwanini hali iwe hivi? Kwa nini wasivune kiasi kinacholingana kwa masaa hayohayo ya kazi na kazi hiyo hiyo? Kwanini mtu mmoja apande mbegu mia moja na avune mavuno mia na mtu mwingine apande mbegu mia moja hiyo hiyo lakini avune mavuno ishirini na tatu?

    Hapa ndipo tunapoona wazi jinsi mavuno yaliyoshindwa yalivyo katika uhalisia wake. Mavuno yaliyoshindwa ni pale mtu anaposhindwa kuvuna mavuno yenye uwiano na kuwa na ulinganifu na kile alichowekeza (mbegu aliyopanda) Watu wanakabiliana na hali hii ya mavuno yaliyoshindwa.

    Mara nyingi chanzo cha mavuno yaliyoshindwa huwa nje ya uwezo wa mtu huyo anayekabiliana na mavuno yaliyoshindwa. Kwanini Mmexico anapata kipato kidogo sana pamoja na bidii yote ukilinganisha na mwanadamu kama yeye aliyeko maili tano tu kuvuka mpaka kuingia Marekani? Kwanini mtu mwingine aliyeko katika ardhi ya Marekani anawekeza kiasi kile kile cha muda na jitihada kama alivyo Mmexico lakini anapata mara kumi na tisa zaidi yake? Vyanzo pamoja na majibu ya utata huu yako nje ya mwanadamu kuyatatua. Lakini Mungu mwenye enzi yote anamuahidi mtoa fungu la kumi kwamba atazuia mavuno yasiangukie kwenye udongo kwa namna isivyostahili. Hataruhusu mavuno yako yadondoke kabla ya wakati wa mavuno.

    Je, ni jambo la ajabu kwamba utoaji wa fungu la kumi ndio ufunguo mkubwa wa mafanikio halisi? Je, unashangaa kuona kwamba wasiotoa fungu la kumi wanaweza kuwa maskini kwa kuweka asilimia kumi ya mapato yao mbali na Mungu?

    Je, Unaweza kufanya nini bila msaada wa Mungu? Je, unaweza kwenda mbali kiasi gani bila msaada wa Mungu? Wakati sasa umefika wa kuanza kutoa fungu la kumi ili kwamba mavuno yako yasiweze kutupwa kwenye udongo kabla hujayafurahia.

    Sura ya Pili

    Laana Zinazowafuatilia Wasiotoa Fungu la Kumi

    Kutokulipa fungu la kumi kunachochea laana nyingine mbalimbali. Watu hufikiri kwamba kutokulipa fungu la kumi kunampelekea tu mtu kupata Laana iliyotamkwa na Nabii Malaki. lakini ukweli ni kwamba, kutokutoa fungu la kumi kunasababisha laana nyingi zaidi ya zile zilizotamkwa na Nabii Malaki. Kutokulipa fungu la kumi kunavuta laana nyingine kadha wa kadha ambazo zinamadhara mabaya na hilo hasa ndilo sura hii unalenga kuzungumzia.

    Je, laana ina maana gani hasa? Kuna namna nyingi ya kuelezea maana ya laana. Maana hizi kumi na mbili za laana zitakusaidia kuelewa maana ya kuwa chini ya laana. Siwezi kuthubutu kuwaza juu ya maana ya mtu chini ya laana nyingi.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1