Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu
Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu
Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu
Ebook174 pages1 hour

Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Ingawa ni hitajiko la Mungu la kimsingi kwa viongozi, wachache sana wameandika kuhusu suala hili. Katika kitabu hiki, Dag Heward-Mills anaainisha misingi muhimu sana na kusudi la kuongeza uthabiti wa makanisa. Maudhui ya kitabu hiki ni husiani na ya vitendo mno jinsi kwamba yamekuwa zana zisizotupika kwa viongozi wengi wa kanisa.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613953518
Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu

Related ebooks

Reviews for Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Uaminifu na Ukosefu Wa Uaminifu - Dag Heward-Mills

    Kwa nini tunahitaji kufundisha juu ya somo la Utiifu na Uaminifu, na Ukosefu wa Utiifu na Uaminifu? Naamini Bwana ameweka moyoni mwangu somo hili la kivitendo kwa sababu mbalimbali. Kwanza kabisa, nimeona uhusika wa somo hili katika Neno la Mungu. Maandiko yamejaa matukio ya watu watiifu na waaminifu, na wasio watiifu na wasio waaminifu. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwenye matukio haya ndani ya Biblia.

    Pia, miaka yangu michache katika huduma imenifanya niwe macho zaidi na watu watiifu na waaminifu na wale wasio watiifu na wasio waaminifu. Nimetambua athari ya jambo hili kwenye makanisa na katika huduma. Katika kurasa chache zijazo, nitakushirikisha sababu chache za kwa nini somo la utiifu na uaminifu ni muhimu kwa kiwango hicho.

    Sababu Saba Kwa Nini Somo la Utiifu na Uaminifu ni Muhimu

    1.      Utiifu na uaminifu ni sifa kuu kwa kila mtumishi.

    Mtu asiye na uzoefu ni rahisi kufikiria kwamba kwa kadri ulivyojaliwa kipawa zaidi, ndivyo unavyofaa zaidi kwa huduma. Uzoefu wangu mdogo umenionesha kuwa ni watu waaminifu na watii ndani ya kanisa wanaofaa zaidi kuwa viongozi.

    Aliye Rafiki na Aliye na Mvuto!

    Mtu asiye na uzoefu ni rahisi kufikiria kwamba ndugu aliye rafiki [wa watu] anaweza kuwa mchungaji mzuri. Pia anaweza kufikiria kuwa mtu aliye na stadi nzuri za uzungumzaji anaweza kuwa mhubiri bora. Usifanye makosa hayo. Biblia hufundisha kwamba sharti kuu la uongozi ni uaminifu na si kitu kingine chochote.

    …inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.

    1 Wakorintho 4:2

    Nina wachungaji wengi wa ajabu wanaofanya kazi pamoja nami. Wengi wao si watu wenye tabia ya urafiki sana, si wenye mvuto au kipekee si waliojaliwa vipawa vikubwa. Lakini, wakati umethibitisha kuwa wao ni zawadi bora ambazo Mungu amelipa kanisa lake na mimi pia.

    2.      Kupambana kwa kutumia safu ya tano

    Mwanzoni kabisa mwa huduma yangu nilitambua kuwa Ibilisi ni mtaalamu wa kuharibu kanisa kutokea ndani [ya kanisa]. Ikiwa u mtumishi mzuri, uliyeitwa na Mungu na unafanya vitu sahihi, Ibilisi atakuwa na fursa kidogo ya kupambana dhidi yako kwa kutokea nje [ya kanisa]. Kama Yesu alivyosema,

    …kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

    Yohana 14:30

    Utatambua kwamba daima Shetani hana nafasi ya kuanzisha mashambulizi makali dhidi yako kwa kutokea nje. Yesu alikuwa akisema kwamba ingawa adui alikuwa anakuja baada yake, [adui huyo] hana kigezo chochote cha kumharibu yeye. Kuna wahubiri wengi waliopakwa mafuta walio katika kundi hili. Shetani hana kigezo chochote ambacho kwacho atawashinda, hivyo hana budi kumtumia mtu mmojawapo kutokea ndani. Kumhusu Yesu, alikuwa ni msaliti [Yuda] ambaye Shetani alimtumia.

    Nakumbuka nilisoma habari ya jenerari wa jeshi ambaye aliuzunguka mji mkubwa akiwa na lengo la kuuteka. Mji huu ulikuwa umezungushiwa ngome imara ya ukuta iliyosimikwa na ndefu na yenye lango. Jenerali wa jeshi aliuzunguka mji tayari kwa mashambulizi.

    Rafiki mmoja wa jenerali huyu alimsogelea na kumwuliza, Bwana, unafikiria utakwendaje kuushinda ulinzi wa mji huu? Hakuna mtu yeyote katika historia ya hivi karibuni ambaye ameweza kuushinda mji huu mkubwa.

    Jenerali wa jeshi alitabasamu na kusema, Ni safu yangu ya tano. Ninawategemea ili wafanye mbinu.

    Rafiki wa jenerali alivutiwa na kuuliza, Safu ya tano ni ipi? Nilifikiria una safu nne tu.

    Jenerali wa jeshi akajibu, Nina safu tano.

    Ooh, naona. Je, ni kitengo maalumu cha makomando au ni wanajeshi wanaanga wa miavuli? yule mtu aliuliza.

    Nitapambana Kutokea Ndani

    Jenerali alicheka, "Hapana, si hawa. Safu yangu ya tano hujumuisha wapelelezi wangu, mawakala wangu, marafiki zangu na wale wanaonisaidia ambao tayari wako ndani ya mji. Wewe subiri tu. Watafungua malango hayo makubwa kutokea ndani na majeshi yangu yataharakisha kuingia ndani."

    Hii ndio njia pekee ambayo adui anaweza kuharibu huduma yenye mafanikio na yenye nguvu na ambayo inafanya vitu vyote sahihi. Ni lazima jambo hili lifanyike kutokea ndani. Safu ya tano hujumuisha watu wasio watiifu na waaminifu, wenye sura mbili [vinyonga], wenye ndimi mbili [ndumila kuwili] na wasioridhika ndani ya kila huduma. Iwapo watu hawa wataruhusiwa kufanya vurugu, jambo wawezalo kulitimiza vema, wataliharibu kanisa.

    Nilikuwa na Mshirika Asiye Mwaminifu

    Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita pindi nilipoanza huduma, nilipata uzoefu wa athari ya kuwa na msaidizi asiye mtiifu na mwaminifu. Mtu huyu, ingawa rasmi alikuwa akisimama upande wangu wa kuume [yaani mshirika wangu wa karibu kabisa katika huduma], hakuniamini na alikuwa akinung’unika dhidi yangu muda wote.

    Nyumba yake ilikuwa mahali pa kukutania kwa watu wote wasioridhika ndani ya kanisa. Kila wakati walipokusanyika, wangenijadili na kunipinga mimi. Nyakati fulani, wangeongea juu ya ninavyohubiri. Nyakati nyingine, ilikuwa jinsi nilivyokunywa maji katikati ya mahubiri yangu. Bado tena, wengine walihisi sikuwa rafiki kwa kiwango cha kutosha. Lakini Bwana alifunua mambo haya yote kwangu. Nilimwomba Mungu juu ya hilo na kumsihi Bwana nifanye nini.

    Mungu akaniambia, Achana na mtu huyo.

    Nikasema, Bwana, unamaanisha anapaswa kuondoka kanisani?

    Na Bwana akasema, Hicho ndicho nimaanishacho hasa! Mwondoshe ama sivyo hutakuwa na amani na kanisa lako halitakua kamwe.

    Basi, nikaitisha kikao cha viongozi wa kanisa. Wakati wa mkutano nikasema, Natambua kuwa Ndugu X hashirikiani nami. Daima amejaa upinzani uumizao.

    Nikamwambia Ndugu X, Najua kuwa huuamini uongozi wangu tena. Nilikufunza. Nilikukuza. Na leo wewe ni mkubwa mno kubaki chini ya mamlaka yangu.

    Nikauliza, Unafikiria tunapaswa kufanya nini?

    Kisha ndugu huyu akasema, Sote tutafute suluhisho.

    Lakini mandiko ambayo Bwana alinionesha yalikijaza kichwa changu.

    Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; naam, fitina na fedheha zitakoma.

    Mithali 22:10

    Nilizungumza, huku nikimwelekezea kidole msaidizi wangu na kusema, Unajua, kwa namna yoyote nzuri nitakayofanya haitakwenda kusaidia chochote. Huniamini mimi tena.

    Niliendelea, Tangu leo, nimekuvua madaraka ya majukumu yako yote katika kanisa hili.

    Akabwetuka, Nini! Kisha akasema, Nitaendelea kuja kanisani hata kama sitakuwa na wajibu maalumu.

    Ni Lazima Uondoke katika Kanisa Hili Sasa!

    Lakini nilimwambia, Hapana! Lazima uondoke! Wewe si sehemu yetu. Uwepo wako kanisani utakuwa na uharibifu.

    Nakwambia, haikuwa kitu rahisi kumwondosha rafiki na mshirika wa miaka mingi. Lakini ilikuwa ni lazima ifanyike. Biblia hutuambia kwamba wakati Ibrahimu alipokuwa kwenye mgogoro na Lutu alimwelekeza Lutu aende mahali pengine! Ibrahimu alikuwa anasema, Ikiwa tutatengana kutakuwa na amani na kazi ya Mungu itaendelea mbele.

    Mtu asiye mtiifu na mwaminifu huzaa magomvi, chuki na malalamiko. Hisia hizi za ukosefu wa utiifu na uaminifu ni kama moshi ambao huijaza nyumba nzima. Njia pekee ya kuondokana na moshi ni kuondokana na moto.

    Kama tunataka kuwa na kanisa kubwa, tunahitaji kuhudumu katika upendo na umoja. Kama hatuwezi kuwa wamoja, basi tuache kuigiza. Unaona, ninawatia moyo watu waondoke kanisani kwangu ikiwa mioyo yao haiko pamoja nami.

    Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu…

    Mathayo 12:30

    Nitakusihi uondoke, kama nitapaswa kufanya hivyo. Sina mzaha katika hili. Tena naweza hata kukupatia fedha kwa ajili ya usafiri na vitafunwa wakati unapoondoka na kutuacha! Ili kwamba wale miongoni mwetu ambao tunapendana kila mtu na mwenzake na tunaaminiana kila mtu na mwenzake tuweze kukaa pamoja na kuendelea na kazi.

    Ondokana na Waigizaji

    Sijui jinsi ya kujiigiza. Kwa urahisi sijui jinsi ya kufanya hivyo. Lakini kuna waigizaji wengi ndani ya kanisa. Wanaigiza kukupenda na kukusaidia lakini mioyo yao hukudharau.

    3.      Kwa kuwa ni pendo la Mungu kulijaza kanisa

    Huduma inapaswa kufanya kazi kwa nguvu ya upendo, umoja na ushirikiano wa pamoja.

    Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

    Yohana 13:35

    Kuhudumu kama viongozi wenye mafanikio unahitaji kudhihirisha upendo ambao Yesu aliuzungumza. Watu huvutwa na upendo. Pindi wawaonapo viongozi ambao hushirikiana kwa pamoja katika pendo halisi, wanavutwa. Ni lazima usisahau kwamba washirika wa kanisa lako si vipofu. Na tena si viziwi. Wanaweza kuona na kuhisi ukosefu wa umoja na kutopatana wakati unapotokea.

    Kondoo Hunywa katika Maji Matulivu tu

    Jambo moja ambalo kila mchungaji ni lazima alijue kuhusu kondoo ni kwamba, hunywa katika maji matulivu. Ikiwa maji ni meusimeusi na machafu kondoo watayapishilia mbali. Unaona, hawana hakika kama hakuna mamba ndani ya maji!

    …Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

    Zaburi 23:2

    Popote palipo na ulaghai na kutokuaminiana, washirika wa kanisa lako hushituka na kuwa waangalifu na hujiweka pembeni.

    4.      Kuwa na timu kubwa na yenye mafanikio

    Mtu mmoja anaweza kufanya mambo mengi. Mchungaji mmoja anaweza kuwa mahali pamoja kwa wakati mmoja tu. Anaweza kuhudumu mpaka nguvu zake (ambazo zina ukomo) zinakapokwisha.

    Kwa sababu hii, mtu yeyoye anayetaka kupanua huduma yake na kuzaa matunda mengi hana budi kujifunza kufanya kazi na watu wengine wengi. Watu hawa ni timu ambayo ninayoizungumzia. Hata hivyo, ni vema kufanya kazi peke yako kuliko na timu isiyo na utiifu na uaminifu, isiyoridhika, isiyo na umoja na isiyoaminiwa na watu. Ukweli ni kwamba, hakuna uwezekano wa kuwa na timu yenye utendaji mzuri ukiwa na watu wa aina hiyo. Naamini, nimekuwa nikiweza kufanya mambo mengi kama nilivyokwishafanya kwa sababu ya timu ambayo nafanya nayo kazi.

    5.      Kuwa na kanisa kubwa

    Wakati niandikapo, kuna makanisa ya Lighthouse duniani kote – kwa kutaja machache: Ghana, Afrika Kusini, New York na Uswisi. Makanisa haya ni sehemu ya mtandao ulio mwaminifu kwa makao makuu ya kanisa yaliyoko Ghana. Mara nyingi watu huniuliza, Unawezaje kuendesha makanisa katika maeneo haya tofauti? Ni aina gani ya udhibiti ulionao?

    Unaona, sehemu kubwa ya mfumo hutegemea uaminifu. Makanisa huchungwa na watumishi ambao ni watiifu na waaminifu kwa Bwana, kwangu na kwa maono ya Lighthouse.

    Pasipo utiifu na uaminifu, kila mtandao au dhehebu miongoni mwa makanisa daima hukutana na msambaratiko. Mara kwa mara, hujigawa katika vikundi vidogovidogo na vikanisa vidogovidogo.

    Kanisa Lao Lilisambaratika

    Nakumbuka habari ya kanisa moja lililokuwa tawi la dhehebu fulani lililosambaratika kwa sababu ya ukosefu wa umoja. Baadhi ya mbegu za muda mrefu za ukosefu wa utiifu na uaminifu zilijidhihirisha muda mfupi baada ya tukio la harambee ndani ya kanisa. Kama matokeo ya kutokukubaliana huku, mchungaji aliamua kujiuzulu na kuanzisha kanisa lake mwenyewe. Alikasirika sana kiasi kwamba alirudisha fedha zote

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1