Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Jinsi ya Kutangua Laana
Jinsi ya Kutangua Laana
Jinsi ya Kutangua Laana
Ebook387 pages4 hours

Jinsi ya Kutangua Laana

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345361
Jinsi ya Kutangua Laana
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Jinsi ya Kutangua Laana

Related ebooks

Reviews for Jinsi ya Kutangua Laana

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Jinsi ya Kutangua Laana - Dag Heward-Mills

    SEHEMU YA 1

    UHALISIA WA LAANA

    SURA YA 1

    Kwa Nini Kitabu Hiki Kuhusu Laana?

    Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.

    Isaya 24: 6

    Kutoka kwa maandiko haya ya awali, tambua kwamba laana ndizo zinazoila dunia na wala sio pepo au pepo wachafu.

    1. Wakristo wa Leo ni lazima wawe na Heshima halisi kwa laana.

    Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.

    Zaburi 119: 6

    Wakristo wa Leo wanafahamu zaidi juu ya pepo wachafu na mashetani kuliko laana. Wakristo wa Leo wanaheshimu uhalisia wa majini lakini hawaogopi na kuheshimu uhalisia wa laana.

    Ni ombi langu kwamba, unapokuwa unasoma kitabu hiki, utakuza heshima halisi na yenye afya kwa ajili ya uhalisia wa laana. Ninaamini uhalisia wa pepo, pepo wachafu na mashetani. Ninawafunga kila siku na kuwatoa maishani mwangu. Nimeandika vitabu vingi juu ya pepo. Hata hivyo, pia ninaamini kwamba laana ndiyo sababu halisi iwafanyayo hawa pepo wachafu wapate nafasi ya kufanya kazi na kusababisha kuvunjika moyo, uovu na kifo. Pepo wachafu ndio wanaotekeleza laana! Laana huwapatia pepo wachafu mfumo wa kisheria wa kutekeleza uovu wao. Amini usiamini kuwako kwa laana, laana ni halisi!

    Ni lazima uanze kuujali uwepo wa laana ambazo huamua na kuunda maisha ya mwanadamu kama tunavyojua leo! Mengi ya yale tunayokumbana nayo leo huamuliwa na laana na baraka zilizotamkwa miaka iliyopita. Kwa kweli, moja wapo ya hulka kuu kuhusu mbinguni ni kwamba hakutakuwa na laana tena.

    … lakini hamkumwangalia yeye aliyeyafanya hayo, WALA KUMJALI yeye aliyeyatengeneza zamani.

    Isaya 22: 11

    Ni jukumu la mtumishi wa Mungu kuonyesha laana zinapokuwapo.

    Si makosa mchungaji kugundua uwepo wa laana. Usilipige vita neno la Mungu! Usikatae uwepo wa laana huku neno la Mungu linasema laana ziko. Si makosa mchungaji kusema au kutangaza kwamba mtu au kundi la watu wanateseka chini ya laana! Kwa kweli ni jukumu la mtumishi mzuri wa Mungu kutambua laana wakati Mungu anapomwonyesha, Sikiliza yale nabii Malaki aliyowaambia Waisraeli. Aliwaambia, Ninyi mmelaaniwa kwa laana! Hakufanya makosa kuonyesha hiyo laana. Alikuwa sahihi katika kutambua laana ilikuwa halisi na ilikuwako Laana inaweza kushindwa wakati tu inapotambuliwa. Ukikataa kwamba laana iko, utawezaje kupigana nayo au kuitangua?

    NINYI MMELAANIWA kwa laana: maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

    Malaki 3: 9

    3. Wakati laana inapotambuliwa na kuonyeshwa usiudhike.

    Wakati ule wa Malaki, watu wa Mungu hawakupaswa kuudhika wakati alipowaarifu juu ya kuwako kwa laana. Usiudhike na haya ninayoandika katika kitabu hiki kuhusu laana zinazowaathiri makundi tofauti ya watu. Siandiki mambo haya ili kudhalilisha kundi lolote la watu, bali kutambua laana ili uweze kuitangua. Sehemu kubwa ya kitabu hiki imetolewa kwa ajili ya kutangua na kushinda laana. Usiache nikawa adui yako kwa sababu mimi ninakwambia ukweli ulio katika neno la Mungu juu ya baraka na laana.

    Kama vile nabii Malaki alivyosema ukweli na akawaambia watu kwamba walikuwa wamelaaniwa, mimi pia ninakuambia juu ya kuwako kwa laana.

    Basi mimi nimekuwa adui yako, kwa sababu ninakwambia ukweli?

    Wagalatia 4: 16

    4. Kila laana inaweza kutanguliwa.

    4.Ninaamini kwamba kila laana inaweza kutanguliwa. Ninaandika kitabu hiki ili kila mtu aliye wazi na neno la Mungu aweza kutambua laana na aishinde kupitia kwa hekima ya Mungu. Unawezaje kutangua kitu ukiwa unasema kwamba hakiko? Kukataa kwako kwamba kitu hicho kiko ndio udhaifu wako mkuu zaidi!

    Usitumie mafundisho ya kitabu hiki kudhalilisha, kutukana au kufedhehesha kundi lolote la watu. Hayo ni makosa Tumia mafundisho ya kitabu hiki kuwatoa watu kutoka katika laana zozote zilizotambuliwa.

    Hiki ni kitabu cha tumaini! Ni kitabu cha ushindi! Ni kitabu kinachotangaza ukuu wako juu ya laana kupitia kwa hekima na nguvu za Mungu. Ninaamini kwamba kila kundi la watu ulimwenguni - matajiri, maskini, wanaume, wanawake, Wayahudi, weusi na weupe Mungu anawajali na wana nafasi ya kukwepa na kushinda kila laana inayofinyaza ambayo inafanya kazi maishani mwao. Mungu anakujali na anakutarajia uinuke na uwe mkuu.

    Usitumie kitabu hiki kudanganya, kutumisha au kunyang'anya mtu yeyote. Ukifanya hivyo umelaaniwa! Tafadhali tumia kitabu hiki kushinda, kutangua, kuondoa kabisa na kuzima aina zote za laana ambazo zinawezakuwa zinafanya kazi maishani mwako. Soma andiko lililo hapo chini na utiwe moyo katika mapenzi ya Mungu kwa ajili ya usawa wako na watu wote na ushindi wako juu ya laana zote.

    Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa MUNGU HANA UPENDELEO: BALI KATIKA KILA TAIFA MTU AMCHAYE, NA KUTENDA HAKI, HUKUBALIWA na yeye

    Matendo 10: 34 - 35

    SURA YA 2

    Laana ni Nini?

    Wala HAPATAKUWA NA LAANA YOYOTE TENA: Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia:

    Ufunuo 22:3

    Maisha duniani yamejaa kuvunjwa moyo kusikokoma, huzuni ya kuendelea, majonzi, misiba isiyoelezeka, kifo, utupu, usumbufu wa kila mara, kuchanganyikiwa, kukosa maana, vita, migongano ya kila mara, na umaskini. Maelezo kama hayo yana fasili moja tu basi – laana!

    Watu wengi hata hawafahamu ukweli kwamba kuna laana hapa duniani. Kitabu hiki kimelenga kukusaidia kutambua laana humu duniani na tupate kuzijali kihalisi. Mtu yeyote ambaye hajali laana kihalisi mbeleni maishani anaweza kujuta.

    Moja wapo ya mambo ambayo yameenea sana duniani leo ni ‘laana’ na athari zake za kutisha. Kuna laana nyingi za zamani zinazofanya kazi na pia kuna maelfu ya laana mpya na ambazo ni za kisasa zaidi. Hebu fikiria tu juu ya jinsi maisha yalivyo hapa duniani nawe utakubali mara moja kwamba kuna laana duniani. Si rahisi sana kufasili laana kwa hivyo ni lazima tuangalie Biblia, na tuone laana ni nini hasa. Natutazame fasili kumi za kibiblia za laana.

    Fasili Kumi za Kibiblia za Laana

    1. Laana ni kuomba nguvu isiyokuwa ya kidunia imfanyie mtu mwingine maovu, ambayo yanaweza kusababisha mateso au kumfanya mtu afe. Ombi lilifanywa kwa Balaamu na Balaki mfalme wa Moabu awalaani Waisraeli.

    Ukisema kwamba mtu fulani ana laana, maanake ni kwamba kunaonekana kuna nguvu isiyokuwa ya kidunia inayosababisha mambo yasiyopendeza yafanyike kwao. Unaweza kutaja laana kuwa kitu kinachosababisha matatizo na madhara makubwa sana. Hapa unakombolewa kutoka kwa kila kinachokuletea matatizo na madhara makubwa sana!

    Akatunga mithali yake, akasema,Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli.

    Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye Bwana hakumshutumu?

    Hesabu 23: 7-8

    2. Laana ni tamanio lolote lililotamkwa kwamba uadui fulani au kisirani kimwangukie au kiambatane na mtu fulani. Hasa, 'laana' inaweza kurejelea tamanio linalodhuru au kuumiza linalowekewa mtu mwingine, na nguvu yoyote isiyokuwa na kidunia, kama vile Mungu, kupitia kwa apizo, ombi, uchawi, uganga au pepo. Kubatilisha au kutoa laana kunaitwa kuondoa au kuvunja. Mara nyingi watu huamini kwamba kunataka tambiko au maombi sawa na laana na yafanywe kwa uangalifu.

    Mungu ameweka laana juu ya wote wanaoabudu sanamu. Usiwe na kitu chochote kilicho na uhusiano na ibada ya sanamu nawe utaepuka moja wapo ya laana mbaya zaidi duniani. Usitumikie pesa! Usiabudu pesa! Usifanye jambo lolote kwa sababu ya pesa nawe utakombolewa kutoka kwa laana yenye nguvu.

    Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.

    Kumbukumbu la Torati 27:15

    3. Kulaaniwa ni kuhukumiwa kushushwa na kudhalilishwa. Nyoka alilaaniwa na Mungu na hivyo akahukumiwa kushushwa na kuwekwa katika udhalili. Kwa neema ya Mungu, hutahukumiwa kushushwa na kudhalilishwa kama nyoka alivyofanywa! Nyoka alihukumiwa kuingia katika nafasi ya chini kabisa duniani. Nyoka alihukumiwa kula kutoka mchangani milele. Hiyo ni nafasi ya chini kabisa kiumbe chochote kinaweza kuingia. Unapolaaniwa, huwa unapelekwa katika nafasi ya chini kabisa. Umeandikiwa kudhalilishwa na kudhunishwa kwa kudumu. Wakati huu Mungu anaingia maishani mwako akuinue kwa nguvu zake.

    Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, UMELAANIWA wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; KWA TUMBO LAKO UTAKWENDA, NA MAVUMBI UTAKULA siku zote za maisha yako:

    Mwanzo 3:14

    4. Kulaaniwa ni kuwa na uchungu usiokoma. Uchungu wa kujirudia, usiokoma, wa kila mara, usioacha na wa kuendelea ndio unaofasili jambo kuwa laana. Adamu alihukumiwa kuingia katika huzuni maisha yake yote. Hii ndiyo sababu ya uchungu usiokoma wa mwanadamu. Huzuni isiyoacha, mfadhaiko na giza linaloathiri ulimwengu mzima ni ushahidi wa laana iliyoko. Pokea furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu na uinuliwe juu ya laana hii.

    Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale: ardhi IMELAANIWA kwa ajili yako; KWA UCHUNGU UTAKULA MAZAO SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO;

    Mwanzo 3:17

    5. Kulaaniwa ni kila kitu kuendelea kufanya kazi kinyume chako wakati wote. Kulaaniwa ni kukumbana na uovu, kisirani na kifo wakati unapopaswa kupokea uzuri, bahati nzuri na maisha mazuri.

    MICHONGOMA NA MIIBA ITAKUZALIA; nawe utakula mboga za kondeni;

    Mwanzo 3:18

    6. Kulaaniwa ni kutoa jasho, kung'ang'ana, kufadhaishwa, kuteseka. Mapigano, ming'ang'ano, kutaabika na kazi katika huu ulimwengu wetu ni ushahidi wa laana hiyo. Pokea neema ya kuinuka juu ya ming'ang'ano, kutaabika na kukosa kuwa na faida hapa duniani.

    Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale: ardhi IMELAANIWA kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao siku zote za maisha yako;

    Michongoma na miiba itakuzalia; nawe utakula mboga za kondeni;

    KWA JASHO LA USO WAKO utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi; ambayo katika hiyo ulitwaliwa: kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

    Mwanzo 3:17-19

    7. Kulaaniwa ni kuvunjwa moyo na kukosa furaha kusikokoma na kupokea kinyume cha yale unayopaswa kupokea kutoka kwa jitihada zako zote. Kaini alilaaniwa na hivi ndivyo laana yake ilivyofanya kazi. Utupu, ubatili, kuvunjika moyo, kunyakua na kutamani vitu vizuri ndio ushahidi mkubwa wa maisha ya laana. Hata ingawa amesoma, anafanya kazi kwa taabu; utupu na kukosa faida kumemdhalilisha mwanadamu.

    Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui: Mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

    Basi sasa, UMELAANIWA wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; Utakapoilima ardhi, HAITAKUPA MAZAO YAKE; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

    Mwanzo 4:9-12

    8. Kulaaniwa ni kutokuwa na makao, mtoro, mbio zisizoisha, muombaji siku zote, mzururaji, msikwao na asiyekuwa na maana yoyote. Kuwa msikwao ni kuishi maisha ya laana. Mungu anakutoa kutoka katika kila maisha yanayofanana na msikwao!

    Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui: Mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

    Basi sasa, UMELAANIWA wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; Utakapoilima ardhi, HAITAKUPA MAZAO YAKE; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

    Mwanzo 4:9-12

    Kulaaniwa ni kuwa mtumwa wa watumwa. Mtumwa wa watumwa ana kisirani cha kudumu (amezuiwa kukua na kuendelea), ana kuchanganyikiwa na kutunduwazwa kusikokoma. Kuwa mtumwa wa watumwa ni kuendelea kushindwa kuinuka, ukisumbuliwa na huzuni na majonzi. Umekombolewa kutoka katika kila aina ya utumishi usioepukika.

    Akasema, *NALANIWE Kanaani; Atakuwa MTUMWA KABISA kwa ndugu zake.

    Mwanzo 9:25

    10. Kulaaniwa ni kuzungukwa, kutatizwa, kusumbuliwa kusikokoma, kuteswa kusikokoma, kushindwa kuepuka na kuendelea kufikia hatima ya kuandikiwa taabu na laana. Uwe unaingia au uwe unatoka, unafikia hatima hiyo hiyo na kuchanganyikiwa huko huko. Mungu anakupatia ufunguo wa hekima utakaokukomboa kutoka kwa maadui waliokuzunguka!

    UTALAANIWA uingiapo, UTALAANIWA na utokapo.

    Kumbukumbu la Torati 28:19

    Fasili hizi muhimu za laana zinafunua kwamba mtu aliyelaaniwa kwa kweli amezungukwa. Kulaaniwa ni kuzungukwa. Hakuna kinachafaulu na hakuna kitakachofaulu unapozungukwa. Fasili zote za laana hukulea katika hitimisho. Umezungukwa.

    Walinizunguka kama nyuki...

    Zaburi 118:12

    Natujaribu kuelewa maana ya kuzungukwa ni nini. Unapozungukwa na kifo, utakutana nacho kila upande utakaoenda. Kwa hivyo, ukilaaniwa kufa, upande wowote utakaogeukia bado utakufa tu. Unaweza kufa huku unatengeneza kikombe cha chai. Unaweza kwenda safari ya mbali na bado utakufa tu. Laana haitegemei uwezo wa mtu wa kukwepa. Laana hutimia kwa sababu hakuna namna ya kuikwepa. Wakristo wa Leo ni lazima wawe na Heshima halisi kwa laana.

    Kulaaniwa ni kuzingirwa. Kuzingirwa ni kuzungukwa huku njia zote za kukuletea vitu zikiwa zimezibwa. Utatambua kwamba mambo mengi katika maisha haya hayana maana. Mambo mengi hayana maelezo mazuri kwa nini yako hivyo. Mambo mengi ni kinyume kabisa ya yale utarajiayo.

    Laana huchora picha isiyoelezeka na dhahiri. Picha huleta matokeo ya hadithi ile ile ikisimuliwa juu ya wale walio chini ya laana wakati wowote, kivyovyote, na popote wanapoweza kuwa! Hebu angalia hadithi ya Afrika! Mataifa ya Afrika, yawe yalitawaliwa na wakoloni, au yawe yalipitia ubaguzi wa rangi, au yawe hayakutawaliwa na wakoloni, au yawe yalipitia mageuzi, demokrasia, na uhuru, hayo yote yameibua picha ile ile hapa Afrika.

    Ni maelezo gani yanayoweza kutolewa kwa ajili ya hali ya umaskini ya Afrika? Kila nchi utakayoenda hapa Afrika ni picha moja tu ndiyo inayoonyeshwa. Je, tumezingirwa na kuzungukwa? Huwezi kuiepuka, hata uende wapi au ufanye nini.

    Kwa mfano, kama kuna laana juu ya jamaa mmoja, hakuna msichana hata mmoja atakayeweza kuolewa. Wawe warefu, wafupi, weupe au weusi, wazuri au wenye sura mbaya, matokeo ni yale yale. Hakuna kuolewa!

    Wanadamu wana laana ya kifo kuambaaambaa juu ya vichwa vyao. Uwe tajiri, maskini, maarufu, huna maana, Mzungu, Mmarekani, Mwafrika, mweusi au mweupe, kifo ndicho adui ambaye ni lazima utakutana naye. Hakuna namna ya kumwepuka adui huyu hata uwe nani.

    Ni muhimu kuelewa laana kwa njia hii kama unataka kuishinda. Biblia ndicho kitabu peke yake ambacho kinatwambia jinsi tunavyoweza kutoka wakati tunapozungukwa. Mji mdogo unapozungukwa na mfalme mwenye nguvu na majeshi yake, huonekana kwamba kifo na uharibifu haviwezi kuepukika. Hakuna kukwepa na hakuna njia ya kutoka nje ya huo mji. Chochote utakachofanya matokeo ni yale yale – kifo!

    Je, Umelaaniwa? Je, Umezungungwa?

    Je, una hali yoyote maishani mwako ambayo hukufanya uhisi kwamba umezungukwa na huna njia ya kutokea? Je, kila kitu unachofanya kinaelekea mahali pamoja pa kushindwa kufaulu na kuvunjika moyo? Pengine laana halisi inafanya kazi. Wakristo wengi sana hupoteza wakati mwingi sana kujaribu kujua kama kuna laana kutoka kwa nyanya yao au kwa mababu zao. Hilo sio jambo la lazima. Kwa nini ujisumbue kutaka kujua kama nyanyako, babu yako alileta laana katika jamaa yako? Biblia inatwambia kwamba kuna laana duniani. Kuhusu laana, hiyo ni halisi na iko! Hata uwe na imani kiasi gani, imani yako haiwezi kuwa juu ya yale yaliyoandikwa katika Biblia. Badala ya kupoteza wakati wako kujaribu kujua kama kuna laana katika jamaa yako, ni lazima uchukulie kwamba kuna laana moja. Unalotakiwa kufanya ni jinsi ya kutoka katika hali ambamo umezungukwa. Kama mtu mwingine yeyote duniani, inaelekea sana kwamba umezungukwa. Mara tu unapoelewa maana ya kuzungukwa ni nini, unaweza kutafuta njia ya kutokea.

    Mataifa yote walinizunguka: Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

    Walinizunguka; naam, walinizunguka: Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

    Walinizunguka kama nyuki; Walizimika kama moto wa miibani: Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

    Zaburi 118:10-12

    Ninaweza kukuhakikishia kwamba jamaa yako ni mbovu kama jamaa mwingine yeyote duniani. Nina hakika kwamba jamaa yako ina idadi sawa ya watu wabaya, wenye dhambi, walozi na wachawi kama jamaa mwingine yeyote. Jinsi unavyofikiri kwamba jamaa ya mtu mwingine ina walozi na wachawi, mtu mwingine pia anafikiri kwamba jamaa yako ina walozi na wachawi. Acha kupoteza wakati wako kutafuta chanzo na asili ya laana na uchawi. Sina haja ya kukushauri mimi mwenyewe ili nipate kujua kwamba kuna laana inafanya kazi mahali.

    Biblia imetwambia waziwazi kwamba kuna laana inayofanya kazi hapa chini ya jua. Uwe uko Ghana, Nigeria, Romania, Marekani, Uingereza, Ujerumani, au Malesia, utatoa jasho ndipo ule. Utagundua kwamba kuvunjika moyo kwa sababu ya kifo na kukosa faida viko kila mahali. Moja yapo ya ishara kubwa zaidi kwamba tumetoka katika ulimwengu huu itakuwa kutokuwako kwa laana vyote inavyowakilisha. Kule mbinguni, hili andiko maarufu …WALA HAPATAKUWA NA LAANA YO YOTE TENA… (Ufunuo 22:3) litadhihirika kikamilifu. Unapofikiria juu ya laana usifikiri kupita kiasi. Laana iko kila mahali. Inafanya kazi na kusababisha kuvunjika moyo na utupu mkubwa katika kila kitu tunachofanya duniani. Sulemani mtu aliyekuwa na hekima zaidi ya wote, alijua kwamba kuna laana kubwa inafanya kazi. Kwa kweli, inataka hekima kutambua kwamba laana inafanya kazi mahali.

    Sulemani Alieleza Laana iliyo hapa Duniani

    Unaona Sulemani aliposema, YOTE NI UBATILI alikuwa anamaanisha nini? Kila kitu alichofanya kiliishia njia ile ile: ubatili, kutokuwa na maana, utupu kulaaniwa, kuvunjika moyo, kuchanganyikiwa! Maisha duniani yana laana ya kuvunjika moyo, ubatili, na kukosa faida kwa kung'ang'ania vitu. Adhabu ya Adamu kwa uasi wake kwa kweli imekuwa kali sana Sulemani alijaribu kukwepa laana kwa kufanya mambo mengi tofauti. Haijalishi Sulemani alifanya nini, aliishia mahali pale pale – ubatili! Alijivumbulia kwamba maisha yamejaa ubatili. Natuangalie mambo tofauti tofauti ambayo Sulemani alijaribu.

    Sulemani alisema, Hebu tujaribu raha. Acha tutafute ‘vitu vizuri’ maishani.' Lakini akapata kwamba, hili pia, halina maana. Kwa hivyo akasema, Kicheko ni upumbavu. Kutafuta raha kunatupatia uzuri gani? Baada ya kufikiri sana, akaamua kujichangamsha na divai. Na huku akiwa bado anatafuta hekima, akafumbata upumbavu. Kwa njia hii, akajaribu kupata raha ya pekee ambayo watu wengi huipata katika maisha yao mafupi hapa ulimwenguni.

    Sulemani pia alijaribu kutafuta maana kwa kujijengea majumba makubwa makubwa na kwa kupanda mashamba ya mizabibu. Akatengeneza mashamba na mabustani na kuyajaza na kila aina ya miti ya matunda Alijenga mabirika ya kukusanya maji ya kunyunyizia miti yake iliyonawiri. Alinunua watumwa, wake kwa waume, na wengine walizaliwa nyumbani mwake. Pia alikuwa na makundi na mabadhi makubwa makubwa zaidi ya mfalme yeyote aliyeishi Yerusalemu kabla yeye.

    Sulemani alikusanya idadi kubwa ya fedha na dhahabu, hazina za wafalme wengi na mikoa mingi. Alikodisha waimbaji wazuri sana, wake kwa waume, na akawa na wake na masuria wengi wazuri. Alikuwa na kila kitu anachoweza kutamani mwanamume!

    Kwa hiyo akawa mtu mkuu kuliko wote waliokuwa wameishi Yerusalemu kabla yeye, na hekima yake haikushindwa. Alichukua chochote alichotaka. Hakujinyima raha yoyote!

    Sulemani alipata raha nyingi hata katika kufanya kazi kwa bidii. Lakini alipokuwa akitazama kila kitu alichokuwa amekifanyia kazi kwa bidii kukipata, yote yalikuwa hayana maana – kama kufukuza upepo. Kwa kweli hakukuwa na chochote cha thamani mahali popote. Aliielezea vizuri akasema; vyote ni utupu na ubatili.

    Kwa maana mtu hupata nini kwa kazi yake yote, na kwa juhudi ya moyo wake alivyojitahidi chini ya jua? Kwa kuwa siku zake zote ni masikitiko, na kazi yake ni huzuni; naam, hata usiku moyoni mwake hamna raha. Hayo nayo ni ubatili.

    Mhubiri 2:22-23

    Kwa kweli ni jambo zuri unapogundua kwamba laana inafanya kazi. Hiyo ni nini? Unapojua juu ya laana, unaweza kuombea hekima ya kuiepuka na kuzuia athari zake. Katika kitabu hiki chote, utajifunza juu ya laana nyingi na jinsi zilivyo halisi. Pia utagundua jinsi hekima ya Mungu inavyoweza kukufanya uepuke na kushinda laana katika maisha haya.

    SURA YA 3

    Laana za Ulimwengu Wote

    Wala HAPATAKUWA NA LAANA YOYOTE TENA: Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia:

    Ufunuo 22:3

    Kuna aina tatu za laana ambazo zinapatikana waziwazi katika Maandiko.

    1. Laana za Ulimwengu Wote

    2. Laana za Biblia

    3. Laana za Kutengenezwa na Desturi

    Laana za Ulimwengu Wote ni laana zilizokuja duniani tangu mwanzo na zimeendelea kuathiri ulimwengu wote mpana bila kukoma.

    Laana za Biblia ni mambo ya kawaida ambayo sote tunajua kwamba Biblia imevitaja kama vitu vilivyolaaniwa. Shughuli au kitendo chochote kinachovuka mipaka fulani huleta laana hizi za Biblia. Katika Biblia yote, unapata mifano ya laana hizi za Biblia ikionyeshwa.

    Laana zinazotengenezwa na Desturi, ni laana zinazotamkwa na watu juu ya wengine, kwa sababu ya makosa yaliyofanyiwa huyo mtu. Laana isiyo na sababu haiwezi kuja lakini laana kama hizo huwa na nguvu zinapopata sababu.

    Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake, KADHALIKA LAANA ISIYO NA SABABU HAIMPIGI MTU.

    Mithali 26:2

    Katika sura hii na zile mbili zinazofuata, tutaangalia Laana za Ulimwengu Wote, Laana za Biblia, na Laana chache za kutengenezwa na Desturi.

    Laana za Ulimwengu Wote

    1. Laana juu ya wanaume.

    Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale: ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

    Michongoma na miiba itakuzalia; nawe utakula mboga za kondeni;

    Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi; ambayo katika hiyo ulitwaliwa: kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

    Mwanzo 3:17-19

    2. Laana juu ya wanawake.

    Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.

    Mwanzo 3:16

    3. Laana iliyotolewa na Nuhu.

    Akasema, naalaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

    Mwanzo 9:25

    4. Laana juu ya Israeli.

    Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo; ndipo zitakapokujia laana hizi zote, na kukupata.

    Kumbukumbu la Torati 28:15

    5. Laana juu ya wale waichukiao Israeli.

    Wayahudi ni watu waliobarikiwa. Ni jambo la hatari kuwachukia na kupigana nao. Wakati wa Vita Vikuu vya Pili, Adolf Hitler na timu yake ya wauaji waliua Wayahudi milioni sita, lakini mwisho wake, kama Wajerumani milioni saba na nusu pia waliuawa. Taifa la Ujerumani liliharibiwa mwisho mwaka wa 1945 lakini taifa la Israeli lilizaliwa baada ya 1945. Watu waingiao katika maisha ya kuwachukia Wayahudi wanaingia katika laana moja kwa moja. Huna haja ya kuingia katika laana inayowangojea wote wanaochukia na kuwalaani watu wa Mungu.

    Amua kuwapenda na uingie katika baraka za Mungu. Ni baraka hizi ambazo huduma nyingi hutafuta kuingia kwa kuunga mkono Israeli na kufanya mambo ya kuisaidia Israeli.

    Kanisa la Mungu lazima litambue baraka zilizoko kwa wale wapendao Israeli.

    Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.

    Mwanzo 27:29

    Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

    Mwanzo 12:3

    SURA YA 4

    Laana Kuu Zaidi Katika Biblia

    MUSA AKAWAAGIZA WALE WATU siku iyo hiyo, akasema, HAWA NA WASIMAME JUU YA MLIMA WA GERIZIMU KWA KUWABARIKIA watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini; NA HAWA NA WASIMAME JUU YA MLIMA WA EBALI KWA LAANA; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali.

    Kumbukumbu la Torati 27:11-13

    Musa ndiye aliyeandika baraka na laana nyingi kuu za Biblia. Alitangaza laana hizi kwa watu wa Mungu alipoanzisha Israeli kuwa taifa.

    Laana Kuu Zaidi Katika Biblia zimeorodheshwa kama vitu ambavyo ni lazima ujiepushe navyo. Ni lazima uishi maisha yako kwa njia ambayo utajiepusha kabisa kuingia katika jambo lolote kati ya haya. Kama hutajali kisawasawa laana hizi zilizoandikwa, zitazunguka maisha yako na kuathiri kila jambo utakalofanya. Kutembelea Yad Vashem Memorial kule Israeli kutakusaidia kujali laana hizi zilizotangazwa na Musa kihalisi.

    Bila kujali laana hizi kihalisi, kila mara utafanya mambo yatakayoleta haana hizi maishani mwako. Ninatambua watu wengi ambao hawajali laana za ulimwengu kihalisi. Inavutia kwa sababu ninaamini kwamba maisha kwa kiasi kikubwa huamuliwa na baraka na laana ambazo tayari zimetamkwa hewani.

    1. LAANA JUU YA WAABUDU SANAMU.

    Watu wapendao pesa na kuabudu pesa kama sanamu wamelaaniwa, (hata kama wao ni wachungaji). Hakuna sanamu inayostahili kuabudiwa. Siku zote utapata laana juu ya watu wafuatao pesa na kuzitumikia badala ya kumtumikia Mungu. Wachungaji wanaotumikia pesa badala ya kumtumikia Mungu huleta laana juu yao wenyewe na juu ya huduma zao.

    Watu wanaoacha huduma zao na kutafuta mafanikio peke yake hukaribisha laana ya waabudu sanamu. Huisimamisha katika mahali pa siri mioyoni mwao na kuifuata kisiri badala ya kumfuata Mungu. Hili huleta kuvunjika moyo, utupu, na kisirani. Na hiyo ni laana!

    Katika Biblia yote, hili jambo moja ndilo linaloamsha ghadhabu ya Mungu. Utatambua kwamba Mungu kamwe hakutoa kauli juu ya idadi ya wake aliokuwa nao Ibrahimu, Isaka, Daudi, Yakobo na Sulemani. Lakini aliikasirikia miungu yao. Siku zote Mungu hukasirika unapokuwa mbadala yake. Siku zote Mungu hukasirika kunapokuwa na kitu au mtu mwingine anayeweza kukufanya uende, utoe sadaka na kugeuza maisha yako. Wakati Mungu hawezi kukufanya wewe ukaenda kufanya mambo kwa ajili yake lakini pesa na kazi zinaweza kufanya hivyo, anakasirika kwa sababu anatambua kwamba wewe una mungu mwingine.

    NA ALANIWE MTU AFANYAYE SANAMU ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri...

    Kumbukumbu la Torati 27:15 (SWU)

    Msifanye SANAMU YO YOTE, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

    Mambo ya Walawi 26:1

    USIJIFANYIE SANAMU YA KUCHONGA, wala mfano wa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1