Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya
Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya
Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya
Ebook40 pages49 minutes

Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya

Rating: 3 out of 5 stars

3/5

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781641345446
Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya

Related ebooks

Reviews for Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya

Rating: 3 out of 5 stars
3/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Ukweli Muhimu Kwa Ajili Ya Waumini Wapya - Dag Heward-Mills

    SURA YA 1

    Jinsi ya kuwa Mkristo Aliyezaliwa Mara ya Pili

    Ikiwa unataka kuzaliwa mara ya pili, ni lazima ufanye mambo mawili muhimu:

    i. Ni lazima kwanza umwamini Yesu Kristo kama Mwana wa Mungu.

    Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu:…

    1 Yohana 5:1

    ii. Pili, ni lazima umkaribishe moyoni mwako na maishani mwako. Ni lazima uombe ombi kamahili huku ukimaanisha kutoka katika kilindi cha moyo wako:

    Bwana Yesu, naja mbele zako nikiwa mwenye dhambi, aliyepotea na kuhukumiwa kwenda Jehanamu. Ninatubu dhambi zangu naninakuomba unisamehe. Ninaamini kwa moyo wangu wote ya kuwa ulikufa msalabani na ukafufuka tena kwa ajili ya dhambi zangu. Ninakufungulia moyo wangu nakukupokea kama Bwana na mwokozi wangu. Tafadhali ninakuombauyadhibiti maisha yangu na unifanye vile utakavyo niwe. Kuanzia leo, mimi ni wako na wewe ni wangu. Asante Baba kwa karama hii nzuri ya wokovu, Amina.

    Nini Hufanyika Unapozaliwa Mara ya Pili?

    Roho wa Mungu atakushukia, na kuingia moyoni mwako. Kisha sehemu yako ya ndani itazaliwa upya au itazaliwa tena.

    Mungu anakupa moyo na roho mpya kwa pamoja!

    Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.

    Ezekieli 36:26-27

    Ukiwa na roho mpya, unakuwa mtu mpya au kiumbe kipya.Uko tayari kuishi maisha mapya. Maisha haya mapya yanawezekana kwa sababu wewe ni mtu mpya mwenye moyo mpya.

    Kuzaliwa mara ya pili ni rahisi jinsi hiyo. Watu wanataka kufanya mambo magumu. Lakini kuzaliwa mara ya pili ni rahisi sana!

    Je, Mkristo Aliyezaliwa Mara ya Pili ni Nani?

    Mkristo aliyezaliwa mara ya pili ni mtu aliyempokea Yesu Kristo maishani mwake na aliyeamua kuishi maisha yanayodhibitiwa na Neno la Mungu na chini ya mwongozo wa Roho Wa Mungu.

    SURA YA 2

    Ukweli Muhimu

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1