Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Nguvu ya Damu
Nguvu ya Damu
Nguvu ya Damu
Ebook70 pages1 hour

Nguvu ya Damu

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

"Biblia inazungumzia aina nyingi za damu: damu ya mbuzi, damu ya kondoo, damu ya njiwa! Biblia pia inasema wazi wazi kwamba pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi. Je, aina yoyote ya damu miongoni mwa damu hizi inaweza kuondoa dhambi zetu? Jibu ni 'Hasha!" "Sasa nini kinaweza kuosha dhambi zetu?" Hakuna kingine isipokuwa damu ya Yesu! Damu ya Yesu pekee ndiyo yenye nguvu za kuosha dhambi zetu na kuleta wokovu.
Katika kitabu hiki muhimu sana, utagundua ukweli mwingi mtakatifu kuhusu damu ya Yesu Kristo. Utaona jinsi damu ya Yesu inavyotoa uzima na jinsi damu ya Yesu ilivyopata umuhimu wake. Utaelewa kuchangamana kwa Roho Mtakatifu na damu ya Yesu. Kwa kweli, kuna nguvu katika damu ya Yesu."

LanguageKiswahili
Release dateMay 15, 2018
ISBN9781641353700
Nguvu ya Damu
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Nguvu ya Damu

Related ebooks

Reviews for Nguvu ya Damu

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

2 ratings1 review

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

  • Rating: 5 out of 5 stars
    5/5
    In fact for the pages I read it very very good

Book preview

Nguvu ya Damu - Dag Heward-Mills

Sura ya 1

Maneno na Damu ya Yesu Kristo

Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa Yesu Kristo. Kuna mambo mengi tunayoweza kujifunza juu ya Yesu Kristo! Tunaweza kujifunza kuhusu maisha yake, familia yake, mafanikio yake, huduma yake, malengo yake na mtindo wake wa uongozi. Lakini mambo mawili muhimu juu ya Yesu Kristo ni maneno yake na damu yake.

Maneno ya Thamani

Maneno ya Yesu ni muhimu kwa sababu yanatufundisha ukweli na hekima ya Mungu.

Inatosha kuyapa maneno ya Yesu umuhimu mkubwa kuliko maneno yote ya wanadamu. Siku hizi, maneno ya Yesu yametenganishwa na maneno mengine ya maandiko kwa wino mwekundu.

Zamani, maneno ya Kristo yalichanganywa pamoja na yale maandiko mengine. Biblia za kisasa zinayapa heshima ipasayo yale maneno ya Yesu. Katika Biblia zenye maandishi ya wino mwekundu, maneno ya Yesu yamewekwa katika tabaka la kipekee; tabaka lisiloweza kulinganishwa na lingine.

Katika kipindi cha Mageuzi ya kanisa, watu waliangazia sana kazi ya Kristo Kalvari. Kabla wakati huo, utu wa Kristo ndio uliokuwa ukiangaziwa. Katika miaka iliyofuata, habari za kina za Maisha yake ya duniani kuanzia kwenye kihori cha ng'ombe hadi msalabani ndiyo yaliyokuwa yakiangaziwa katika utafiti mkali. Siku hizi, lazima tuangazie zaidi damu ya Yesu Kristo.

Kwa bahati nzuri, thamani ya kipekee ya damu ya Yesu inatambuliwa leo. Damu ya Yesu inapewa hadhi kubwa kama inavyopaswa kupewa.

Damu ya Thamani

Dhambi zetu haziwezi kuoshwa na kuondolewa kwa maneno ya Yesu. Tunahitaji damu ya Yesu kutuosha na kutuondolea uovu wetu na hali yetu ya dhambi ili majina yetu yaandikwe katika Kitabu cha Uzima. Haijalishi Yesu aliongea kwa kiasi gani, alihubiri kwa kiasi gani na alfundisha kwa kiasi gani, bado alihitaji kutunusurisha kwa nguvu za damu yake. Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi! Kulihitajika kumwagika damu ili dhambi zetu ziweze kufunikwa.

Nani Angeweza Kulipia Dhambi Zetu?

Ni kweli kwamba kuhubiri na hekima ya Mungu inapatikana katika mafundisho ya Yesu Kristo. Lakini nani angelipia dhambi zetu? Nani angelipa gharama ya kutuwezesha kuepuka jehanamu? Tumekombolewa (tumerudishwa) kwa damu ya Yesu Krsito. Hatukombolewi kwa maneno ya Yesu lakini tunakombolewa kwa damu yake. Tulikombolewa si kwa damu ya fahali na mbuzi bali kwa damu ya Yesu.

Acha Kuhubiri na Uruhusu Damu Itiririke

Kwa nini Yesu Kristo aliacha kuhubiri wakati alipokuwa na umri wa miaka thelathini na tatu na kwenda msalabani? Kwa nini hakuendelea na kazi yake ya kuhubiri na kufundisha neno la Mungu katika nchi nyingine? Si angekuwa ameenda Syria, Lebanon, Uingereza, Ujerumani, Iraq, Uajemi, India na Afrika? Bila shaka angelienda! Wakati anayatoa maisha yake msalabani, alikuwa na umri wa miaka thelathini na tatu. Kama angeliishi miaka mingine arubaini, hadi pengine kufikia umri wa miaka themanini, angeweza kusafiri ulimwenguni kote.

Nilipozuru Chennai huko India, niliona kanisa moja lililojengwa kwa heshima ya Mtakatifu Tomasi, yule mwanafunzi aliyeona shaka. Tomaso alikuwa mmoja wa wale mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo. Ni dhahiri kuwa mtume Tomaso alienda India na kuhudumu huko. Akiwa huko India, aliuawa kwa sababu ya imani yake na kukajengwa kanisa huko kwa heshima yake. Ikiwa Tomaso aliyeishi na kutembea na Yesu aliweza kwenda India basi Yesu mwenyewe angeweza kwenda vile vile. Yesu Kristo alikuwa na uwezo wa kutembea kila mahali duniani na kuhubiri injili ya ufalme.

Yesu Kristo aliacha kuhubiri kwa ghafla na akaelekea Yerusalemu ambapo alijua angekamatwa, kuteswa na kuuawa. Yesu alisema, 'Hakuna mtu aniondoleaye, Bali mimi nautoa mwenyewe.' Kwa nini Yesu alifanya hivyo? Je, alikuwa anafikiria vizuri?

Kwa nini Msalaba?

Kwa nini Yesu kwa kupenda kwake na ufahamu wake mwenyewe alikwenda mahali pa kusulubiwa ambapo watu waovu wangemuua? Hii ndiyo njia aliyoruhusu damu yake imwagwe kwa ajili ya dhambi za mwanadamu. Kama Yesu asingemwaga damu yake kwa ajili yetu, huduma yake ingedumu hadi wakati ule ambapo ujumbe wake ungefifia. Leo hii, nguvu ya damu ya Yesu iliyomwagwa bado inafanya kazi. Inafika juu ya mlima mrefu zaidi na kwenye bonde la chini zaidi la ulimwengu wetu. Nguvu za Mungu za wokovu zinatolewa hata baada ya miaka elfu mbili tangu kufa kwa Yesu Kristo kwa sababu ya damu ya Yesu. Ndio sababu damu ya Yesu ni

Enjoying the preview?
Page 1 of 1