Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari
Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari
Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari
Ebook112 pages3 hours

Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari

Rating: 3 out of 5 stars

3/5

()

Read preview

About this ebook

Usiku mmoja, wakati akiwa ni mwanafunzi wa utabibu katika mji mmoja huko Ghana, katika hali ya mwujiza Mungu alimpaka mafuta Dag Heward-Mills wakati alipokuwa akimsubiri Bwana. Alipakwa mafuta kwa namna isiyo ya kawaida na kusikia maneno, “Tangu sasa na kuendelea unaweza kufundisha...” Wito huu usio wa kawaida ndio uliomwongoza kwenye huduma iliyosambaa duniani kote.

LanguageKiswahili
Release dateMay 16, 2018
ISBN9781641353779
Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari

Related ebooks

Reviews for Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari

Rating: 3 out of 5 stars
3/5

2 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kitabu Cha Mistari Ya Bibilia Ya Kukari - Dag Heward-Mills

    The Holy Bible in Kiswahili, Union Version 1994

    © Hakinakili 2017 Dag Heward-Mills

    Jina la Awali : Bible Memorisation Handbook

    Kwa habari zaidi kuhusu Dag Heward-Mills

    Kampeni ya Yesu Mponyaji

    Andika kwa: evangelist@daghewardmills.org

    Tovuti: www.daghewardmills.org

    Facebook: Dag Heward-Mills

    Twitter: @EvangelistDag

    ISBN : 978-1-64135-377-9

    Haki zote zimehifadhiwa na sheria ya kimataifa ya hakinakili. Idhini ya maandishi lazima itolewe na mchapaji ili kutumia au kuzalisha sehemu yoyote ya kitabu hiki.

    Yaliyomo

    Sura ya 1: Kukariri Bibilia ni Nini?

    Sura 2: Umuhimu wa Kukariri Biblia

    Mwanza

    Kutoka

    Mambo ya Walawi

    Hesabu

    Kumbukumbu la Torati

    Yoshua

    Ruthu

    1 Samweli

    2 Samweli

    1 Wafalme

    2 Wafalme

    1 Mambo ya Nyakati

    2 Mambo ya Nyakati

    Ezra

    Nehemia

    Esta

    Ayubu

    Zaburi

    Mithali

    Mhubiri

    Wimbo Ulio Bora

    Isaya

    Yeremia

    Maombolezo

    Ezekieli

    Danieli

    Hosea

    Yoeli

    Amosi

    Yona

    Mika

    Habakuki

    Sefanai

    Hagai

    Zekaria

    Malaki

    Matayo

    Marko

    Luka

    Yohanna

    Matendo Ya Mitume

    Warumi

    1 Wakorintho

    2 Wakorintho

    Wagalatia

    Waefeso

    Wafilipi

    Wakolosai

    1 Wathesalonike

    2 Wathesalonike

    1 Timotheo

    2 Timotheo

    Tito

    Filemoni

    Waebrania

    Yokobo

    1 Petro

    2 Petro

    1 Yohanna

    2 Yohanna

    3 Yohanna

    Yuda

    Ufunua wa Yohanna

    Sura ya 1

    Kukariri Bibilia ni Nini?

    Kukariri Bibilia ni msingi mkuu wa huduma kubwa. Leo, watu wengi hawasimamii msingi imara na hivyo basi hawawezi kuzalisha kazi kubwa kwa Mungu hapa duniani.

    Kwa kazi ngumu na mtazamo wenye bidii na tabia ya kiunyenyekevu, utaijenga tabia muhimu inayoweza kubeba karama kuu za Mungu. Kupitia kukariri Biblia huduma yako itaenda kwa viwango vya juu viwezekanavyo.

    Kukariri Bibilia ni kuikita akilini mistari ya msingi ili uweze kuinukuu pale inapohitajika.

    Kuwa Mfuasi wa Kristo

    Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.

    Mathayo 4:19

    Lazima uelewe kwamba lengo ni kukufanya kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu kristo aliyekariri maandiko.

    Kila siku maishani ni siku ya kukariri andiko kwenye Biblia.

    Kila siku maishani ni fursa kubwa ya kujenga tabia nzuri na iliyoboreshwa.

    Kila mazungumzo na mtu mwingine ni fursa ya kukariri andiko.

    Kila mazugumzo na mwamini mwenzako ni fursa ya kujaribiwa kwenye ujuzi wako wa kukariri.

    Katika kurasa zifuatazo, utapata fungu la maandiko ambalo kila Mkristo anategemewa kukariri. Mimi binafsi nimechagua kila mojawapo ya maandiko haya. Maandiko hayajadhamiriwa kwako kwa kurejea tu. Ni kwa ajili ya kukariri! Kuna maandiko mengi utayajua lakini kuna baadhi ya maandiko ambayo unapaswa kuwa tayari kunukuu!

    Beba kitabu hiki wakati wote. Uwe tayari kunukuu andiko lolote wakati wowote ule unapoulizwa. Unapokuwa Mkristo kwa miezi kadhaa, lazima uwe tayari kunukuu mojawapo ya maandiko haya. Hakika lazima uwe mtu wa Mungu wa kunukuu Biblia.

    Nakutangazia kuwa mfuasi wa Yesu Kristo na mfano mzuri wa huduma kupitia kitabu hiki cha kipekee cha kukariri Biblia!

    Sura 2

    Umuhimu wa Kukariri Biblia

    Mtumishi lazima awe mbeba Neno la Mungu. Lazima awe mtu aliyevikwa kabisa kwa neno la Mungu na utukufu wake. Ndio maana kukariri Biblia ni muhimu kwa kuendeleza huduma.

    Hapo mwanzo kulikuwa na Neno. Hii ina maana kwamba neno la Mungu daima litakuwa kwenye msingi wa kila kitu anachokifanya Mungu.

    Leo, kuweka akilini maandiko kunapata umuhimu tena kwa sababu Mungu anajenga kanisa lenye utukufu zaidi. Utukufu wa kanisa hili la mwisho litakuwa bora zaidi kuliko utukufu wa kanisa lilioanza kutangaza habari njema za Yesu Kristo. Hii pia inamaanisha kwamba watumishi watakaoinuka, katika siku za mwisho watakuwa wamepakwa mafuta zaidi na wenye utukufu kuliko kabla. Watalijua Neno la Mungu na kulinukuu kwa wepesi!

    Je huduma hizi zenye utukufu na makanisa haya yenye utukufu yatazaliwaje na kuumbwa? Biblia iko wazi kwenye hilo. Kupitia Neno la Mungu mtumishi hujengwa na kutayarishwa kwa ajili ya kazi kubwa katika huduma ya Yesu. Yote haya yanahusu maarifa yetu ya maandiko!

    Katika 2 Timoteo 3:16-17, tunaona maono yenye nguvu na muhimu ya jinsi ya kuwa mtumishi bora aliyetayari kwa kazi zote nzuri: andiko!

    Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

    Kitabu hiki cha Kukariri kinakupa baadi ya maandiko muhimu ambayo unapaswa kuyajua. Ni mkusanyiko wa thamani wa maandiko yote unayopaswa kuyajua. Chukua maandiko yaliyopo kwenye kitabu hiki moyoni mwako kupitia stadi ya kukariri. Kadiri unavyokariri utakuwa umejipa mwenyewe msingi imara kwa ajili ya huduma.

    Kuwa kama Yesu Mkombozi wetu! Yesu Kristo alijawa maandiko aliyokariri.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1