Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa
Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa
Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa
Ebook421 pages13 hours

Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa

Rating: 4 out of 5 stars

4/5

()

Read preview

About this ebook

Usiku mmoja, wakati akiwa ni mwanafunzi wa utabibu katika mji mmoja huko Ghana, katika hali ya mwujiza Mungu alimpaka mafuta Dag Heward-Mills wakati alipokuwa akimsubiri Bwana. Alipakwa mafuta kwa namna isiyo ya kawaida na kusikia maneno, “Tangu sasa na kuendelea unaweza kufundisha...” Wito huu usio wa kawaida ndio uliomwongoza kwenye huduma iliyosambaa duniani kote.

LanguageKiswahili
Release dateMay 16, 2018
ISBN9781641353786
Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa

Related ebooks

Reviews for Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa

Rating: 3.75 out of 5 stars
4/5

4 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Ndoa ya Mfano Wa Kuigwa - Dag Heward-Mills

    Maandiko Matakatifu:

    The Holy Bible in Kiswahili, Union Version 1994

    © Hakinakili 2014 Dag Heward-Mills

    Jina la Awali : MODEL MARRIAGE

    Mtafsiri: Emmanuel E. Buganga

    Taasisi Tafsiri: Trans-Africa Swahili Christian Ministries,

    S.L.P. 772, Mwanza

    Tanzania

    Barua-pepe: tascmt@yahoo.com

    Toleo Asilia lilichapwa mwaka 1992 na Parchment House

    Toleo la kwanza Kiswahili limechapishwa na

    Parchment House, 2014

    Kwa habari zaidi kuhusu Dag Heward-Mills

    Kampeni ya Yesu Mponyaji

    Andika kwa:  evangelist@daghewardmills.org

    Tovuti:  www.daghewardmills.org

    Facebook: Dag Heward-Mills

    Twitter:  @EvangelistDag

    ISBN: 978-1-64135-378-6

    Haki zote zimehifadhiwa chini ya sheria za kimataifa ya hakinakili. Uchapaji au utoaji wa kitabu hiki au sehemu yake kwa njia yoyote ile hauna budi kupata idhini ya mchapaji, isipokuwa kwa matumizi ya nukuu katika mapitio au makala za kihakiki.

    SHUKRANI

    Kitabu hiki ni zao la utafiti mkubwa, majadiliano na uchambuzi wa kina. Ningependa kushukuru juhudi za watu mbalimbali katika hatua mbalimbali za uandishi wake.

    Kwanza kabisa na zaidi ya wote, ningependa kumshukuru mke wangu Adelaide kwa kunipatia uzoefu wa kivitendo katika ndoa na kwa juhudi zake katika masomo mbalimbali ya ndoa. Anastahili kutajwa kipekee kwa kusaidia kuiweka pamoja sura inayohusu Mji Wakambo na vilevile sehemu kubwa ya taarifa kuhusu Silika.

    Pia namshukuru Mchungaji E. A. T. Sackey na Mchungaji Eddy Addy, watumishi wenzangu wakuu wanaonisaidia, kwa juhudi zao mbalimbali kwa miaka mingi; majadiliano yao, michango na uchambuzi wa masuala mwafaka hususani kutoka katika mtazamo wa ndoa wa kiroho, kibiblia na kimafundisho.

    Ninawiwa na jopo la madaktari wa kitabibu: Dk. Joe Adjei, Dk. Rosemary Ampofo, Dk. Henrietta Orleans-Lindsay, Dk. Mina John, Dk. Louisa Appea-Danquah na Dk. Joyce Wilson kwa uchambuzi wao, majadiliano mbalimbali ya kitabibu, na utafiti wa kitabibu.

    Ningependa kumshukuru Meja na Bi. Lawrence Mefful, kwa jukumu lao katika Idara ya Ushauri wa Ndoa, na pia kwa kusaidia kutoa mengi ya majibu kwenye sura ya Maswali na Majibu.

    Shukrani zangu tena zimwendee mke wangu Adelaide na Amelia Aidoo kwa jitihada zao kwenye sura inayohusu Talaka.

    Shukrani kwa Duke Gyamerah kwa usanifu wa kwanza kabisa na William Aggrey-Mensah kwa kupitia tena usanifu kabla ya uchapaji. Asante, Vida Gyamerah, kwa mchango wako pia.

    Shukrani zangu zamwendea Doris Ademola kwa kazi ya awali ya upangaji wa muundo wa kitabu na kwa kazi ya uhariri na pia Johnny Awanyo kwa msaada wake wa muswada. Wa mwisho lakini si kwa udogo, napenda kulishukuru kanisa la The Lighthouse Chapel International kwa kunipatia orodha ya maswali ambayo walidhani yalikuwa mwafaka kuhusiana na mazingira ya ndoa halisi kwenye sura ya Maswali na Majibu.

    Hatimaye tena nimshukuru Amelia Aidoo, na Juanita C. Sackey, kwa uhariri wao wa mwisho, upangaji wa muundo wa kitabu na kazi za kuhitimisha kwenye toleo letu hili la pili la kitabu-elekezi cha ushauri wa ndoa.

    Kwenu ninyi nyote watu wa ajabu, nataka kusema kuwa mu jopo kubwa!

    Yaliyomo

    SHUKRANI: UTANGULIZI

    UTANGULIZI

    SEHEMU 1: WAPENDANAO

    Sura ya 1: Wapendanao

    Sura ya 2: Utambuzi Rasmi wa Mahusiano kupitia Kanisa

    Sura ya 3: Kuwashauri Wapendanao

    SEHEMU 2: MAMBO YA MSINGI

    Sura ya 4: Fasili ya Ndoa

    Sura ya 5: Sababu za Kibiblia za Ndoa

    SEHEMU 3: MAHUSIANO

    Sura ya 6: Ndoa ya Muundo wa Mungu

    Sura ya 7: Mji wa Kikristo

    Sura ya 8: Upendo katika Ndoa

    Sura ya 9: Mawasiliano katika Ndoa

    Sura ya 10: Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu katika Ndoa

    SEHEMU 4: MAJUKUMU

    Sura ya 11: Majukumu ya Mume

    Sura ya 12: Majukumu ya Mke

    Sura ya 13: Mke Kamili

    Sura ya 14: Utunzaji Mji na Wasaidizi wa Nyumbaji

    SEHEMU 5: SILIKA

    Sura ya 16: Utangulizi Kuhusu Silika

    Sura ya 17: Inamaanisha Nini Kuwa na Mume au Mke Sanguini

    Sura ya 18: Inamaanisha Nini Kuwa na Mume au Mke Mkoleriki

    Sura ya 19: Inamaanisha Nini Kuwa na Mume au Mke Mmelankoli

    Sura ya 20: Inamaanisha Nini kuwa Mke au Mume Mflegmatiki

    SEHEMU 6: MATATIZO NA UFUMBUZI

    Sura ya 21: Ufumbuzi wa Matatizo katika Ndoa

    Sura ya 22: Ndugu wa Mume au Mke

    Sura ya 23: Mji wenye Kuasili [Mji wa Kambo]

    Sura ya 24: Kile Ambacho Kila Mkristo Hupaswa Kujua Kuhusu Talaka

    SEHEMU 7: UFUNGUO MKUU WA KUKUBALI

    Sura ya 25: Ufunguo wa Kukubali

    SEHEMU 8: MWILI WA MWANADAMU

    Sura ya 26: Kuufahamu Mwili wa Mwanadamu kupitia Picha

    Sura ya 27: Njia za Mpango wa Uzazi

    SEHEMU 9: UHUSIANO WA KINGONO

    Sura ya 28: Utangulizi wa Furaha ya Tendo la Ndoa

    Sura ya 29: Usiku wa Harusi

    Sura ya 30: Fungate

    Sura ya 31: Tendo la Ndoa Liburudishalo

    Sura ya 32: Tendo la Ndoa Lenye Wajibu

    Sura ya 33: Tendo la Ndoa Lisisimualo

    Sura ya 34: Kilele

    Sura ya 35: Hofu za Kawaida Kuhusu Tendo la Ndoa

    Sura ya 36: Tendo la Ndoa kwa ajili ya Uzazi

    Sura ya 37: Maeneo Tata Kuhusu Tendo la Ndoa

    SEHEMU 10: KANUNI ZA TENDO LA NDOA

    Sura ya 38: Kanuni Tengefu za Kibiblia 1-12

    Sura ya 39: Kanuni Tengefu za Kibiblia 13-24

    Sura ya 40: Kanuni Tengefu za Kibiblia 25-33

    SEHEMU 11: ZAIDI KUHUSU SILIKA

    Sura ya 41: Silika na Tendo la Ndoa

    Sura ya 42: Kukuza Silika za Kiroho Zilizokomaa

    Sura ya 43: Vidokezo vya Jinsi ya Kuhusianana Silika za Mwenzi Wako

    SEHEMU 12: MAISHA YA KIMAPENZI YALIYOBORESHWA

    Sura ya 44: Jinsi ya Kuboresha Maisha Yako ya Kimapenzi

    Sura ya 45: Tendo la Ndoa Uzeeni

    SEHEMU 13: UJAUZITO, KUJIFUNGUA NA UANGALIZI WA MTOTO

    Sura ya 46: Jinsi ya Kujua U Mjamzito

    Sura ya 47: Kile Kinachotokea Wakati wa Wiki Arobaini za Ujauzito

    Sura ya 48: Matatizo Nane ya Kawaida Wakati wa Ujauzito

    Sura ya 49: Maisha ya Kawaida Wakati wa Ujauzito

    Sura ya 50: Jinsi ya Kujitunza Mwenyewe Wakati wa Ujauzito

    Sura ya 51: Matatizo Manne Madogomadogo Yanayotarajiwa wakati wa Ujauzito

    Sura ya 52: Utungu na Kujifungua

    Sura ya 53: Hatua Tatu za Utungu

    Sura ya 54: Unyonyeshaji

    Sura ya 55: Kipi cha Kutarajia kutoka kwa Mwanao katika Miezi Kumi na Miwili ya Mwanzo

    Sura ya 56: Kumpa Kinga Mtoto Wako

    SEHEMU 14: MALEZI

    Sura ya 57: Malezi na Kile Ambacho Kinajumuishwa Ndani Yake

    SEHEMU 15: VIWANGO VIPYA

    Sura ya 58: Watoto wa Kuasili

    Sura ya 59: Kumpoteza Mwenzi

    SEHEMU 16: MASWALI MAHUSUSI YA WENZI WALIOOANA NA MAJIBU YAKE

    Sura ya 60: Maswali Mahususi ya Wenzi Waliooana na Majibu Yake

    UTANGULIZI

    Ninayo furaha kutambulisha toleo la pili na lililoongezwa la kitabu-elekezi cha ushauri wa ndoa ambapo hapo awali kiliitwa Kitabu-Elekezi cha Ushauri wa Ndoa. Kitabu hiki Elekezi, kilichochapwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1922, na kilicho toleo la kale zaidi katika huduma hii, kimepata kuwepo kutokana na miaka mingi ya kujifunza Neno la Mungu na kujipatia uzoefu wa kivitendo katika ndoa. 

    Kutokana na uzoefu wangu wa kichungaji, natambua kuwa ndoa na changamoto zake tata vyaweza kuwaathiri vibaya Wakristo wengi na kuwazuia watu walioitwa kwenye huduma.

    Ninayo furaha kukiandika na kukiweka pamoja kitabu hiki kwa kupitia hatua mbalimbali za maisha yangu kwa sababu nimejifunza kutokana na uzoefu wangu kwamba tunasisitiza mambo tofauti katika hatua tofauti za maisha na huduma. Kwa mfano, nimegundua kuwa silika ya mtu katika uhusiano wa ndoa, kimsingi, huamua tabia ya mtu katika mazingira ya ndoa. Pamoja na ushauri mwingi, mafundisho na maombi, watu wengi huishi tu kwa kulingana na maumbile ya silika zao. Kweli hizi hazikuwa dhahiri kwangu miaka kumi iliyopita kama zilivyo leo. Pia, miundo ya tabia ya mwanamume na mwanamke ni rahisi sana kutabirika, kwa kuwa haibadiliki sana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

    Kwa hiyo, kwangu mimi, ingawa kimsingi unafanana, ushauri wa ndoa ni lazima ufanywe ukiwa na utambuzi wa kweli hizi, yaani, miundo ya tabia ya silika na jinsia. Iwapo wachungaji watazielewa kikamilifu kweli hizi muhimu, hawatachanganyikiwa wakati washauriwa wao hawabadiliki sana. Pia ninaamini kuwa tutakuwa kwenye hatari ndogo ya talaka wakati tuelewapo maumbile yetu ya silika, uanaume wetu na uanamke wetu hutuathiri kwa kiwango gani.

    Pia nimechunguza mazingira tata ambayo husababisha talaka; jambo lililoonekana kuwa lisilowezekana kabisa mwanzoni mwa huduma yangu ya Kikristo. Nimefikia hatua ya kuukubali mchango wa magonjwa ya kisaikolojia na kiakili yasiyo rahisi kuchunguzwa katika tabia ya wenzi, hususani wanawake. Pengine, katika matoleo yajayo ya kitabu hiki, kutakuwa na marejeo zaidi kuhusu masuala hayo.

    Kwa kutambua kuwa uzoefu wa ndoa yangu pekee una mipaka, katika kitabu hiki daima nimejaribu kuchota kutoka kwenye fahamu za wanaume na wanawake kuhusu masuala mbalimbali. Katika kufanya hivyo, nimekusanya mielekeo na mitazamo tofauti kutoka pande zote ikijumuisha wanaume na wanawake, wasomi na wasiosoma; matabibu na wasio matabibu.

    Utafiti huu pia umewezeshwa na baadhi ya tafiti ambazo zilifanywa kwenye makundi na watu tofautitofauti.

    Yote katika yote, imekuwa ni safari endelevu ya kujifunza ambayo haitakwisha. Naomba kwamba Mungu atakupatia hekima kwa ajili ya ndoa yako na vilevile hekima ya kuwasaidia wengine. 

    Naomba kwamba kila wenzi wafaidikao na kitabu hiki watakuwa na ndoa imara na yenye furaha.

    SEHEMU 1

    WAPENDANAO

    Sura ya 1

    Wapendanao

    Mpendwa ni Nani?

    Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake...

    Wimbo Ulio Bora 2:16

    Mpendwa ni mtu ambaye una uhusiano naye, ambao unakusudiwa kuishia katika ndoa. Kwa maneno mengine, yeye ni mwanamume au mwanamke ambaye mmekubaliana rasmi kuoana. Wengine hutumia neno mchumba, rafiki wa kiume, au rafiki wa kike kuuelezea uhusiano huu, lakini katika kitabu hiki tunachukua na kutumia neno mpendwa.

    Hatuwashauri vijana wa kiume na wa kike kuwa na uhusiano wa karibu na mtu mwenye jinsi tofauti, ambao haukusudiwi kwa ajili ya ndoa, kama ambavyo hawa marafiki wa kiume na marafiki wa kike kwa kawaida hujihusisha wenyewe na tabia zisizofaa kama vile uasherati. Hivyo, tunawaangaliza kuwa mahusiano hayo hayana budi kuingiwa hasahasa kwa kusudi la ndoa, na kwamba kipindi cha kukuza uhusiano kabla ya ndoa (kimapokeo hujulikana kama urafiki) hakipaswi kuwa kirefu sana.

    Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

    1 Wakorintho 7:2

    Je, Una Hakika ya Kutaka Kumwoa Mtu Huyu?

    …jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema…

    1 Wathesalonike 5:21

    Wakamwita Rebeka wakamwuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema, Nitakwenda.

    Mwanzo 24:58

    Mambo Nane ya Kujali Wakati Uchaguapo Mpendwa

    1. Ukweli kuwa wazazi ni watu wazuri haimaanishi kuwa mtoto naye atakuwa mwenzi mwema. Je, amejitoa kabisa kwa Mungu?¹

    2. Usioe kwa sababu wazazi wako wanasema hivyo. Mshirika wako aliyekusudiwa ni rafiki yako?²

    3. Iwapo unaoa mapema sana utakosa baadhi ya mambo fulani maishani (mfano, ujana wako, muda wako wa kuwa mseja na huru).

    4. Zingatia ukweli kuwa kiuhalisia watu hawabadiliki na hivyo chochote usichokipenda kuhusu mpendwa wako na kwa maana hiyo mwenzi, pia kina uwezekano wa kutobadilika. 

    5. Je, utakuwa katika hali ya kujimudu kifedha?

    6. Je, utakuwa na mahali pa kukaa wakati uoapo?

    7. Tofauti za kikabila zinaenda kuathiri ndoa yenu.

    8. Tofauti kubwa ya kiwango cha elimu pia itaathiri ndoa yenu.³

    Tanbihi

    1. Theda Hlavka, Saying I Do Was the Easy Part (Nashville, Tennessee: Broadman & Holman Publishers, 2001), 83 - 88.

    2. William L. Coleman, Engaged: When Love Takes Off (Wheaton, Illinois: Tyndale House Publishers, 1980), 18 - 19.

    3. David H. Olson and John Defrain, Marriage and the Family (Mountain View, California: Mayfield Publishing Company, 2000), 276 and Evans A. Laryea, Joining of Lives (Accra, Ghana: PAL International, 2002),10 - 11, 166 - 205.

    Sura ya 2

    Utambuzi Rasmi wa Mahusiano kupitia Kanisa

    Sababu Tatu kwa Nini Mahusiano ni Lazima Yasajiliwe

    Kila kanisa linapaswa kuwa na daftari la usajiri ambalo hutunza taarifa zifaazo za washirika wake ambao wanakusudia kuoa au kuolewa. Daftari hili hutumika kama utambulisho rasmi wa uhusiano na kanisa, na linapaswa kufanywa angalau miezi sita kabla ya ndoa iliyokusudiwa. Kwa nini kusajili?

    I. Kubaini kama baadhi ya watu wameshaoa au kuolewa tayari

    Baadhi ya wenzi tayari wanaweza kuwa na watoto kutokana na uhusiano wa sasa au wa zamani. Katika baadhi ya tamaduni, ni desturi kuwa na kile kinachoitwa utaratibu wa kidini wa ndoa ya kienyeji. Ni muhimu kujua iwapo wenzi walifanya sherehe hiyo au la. Aina yoyote ya sherehe, mila au utaratibu wa ndoa ya kidini ni lazima viletwe nuruni. Kushindwa kuweka wazi taarifa hizo kunaweza kusababisha uhusiano kufika mwisho.

    II. Kuhakikisha kuwa mahusiano hayo yote hayafichwi

    Ni agizo kuwa mahusiano yote yawe wazi mbele za Mungu, mchungaji na washirika wa kanisa. Kuendesha uhusiano kwa uwazi pia husaidia kuchochea afya na uzima wa uhusiano.

    III. Kupata kuwajua vema wenzi

    Kwa kuwasajili wenzi, utajifunza zaidi kuwahusu wao kwa namna binafsi zaidi:

    1. Majina kamili ya wenzi (kwa kukamilisha matakwa ya daftari la usajili).

    2. Unaweza kupima vizuri kujitoa kwao Kikristo.

    3. Jua kanisa la mpendwa wa mshiriki wako, kama si wa kanisa lako.

    4. Chunguza kiwango chao cha shughuli za kikanisa.

    5. Pata hakika ya uhusiano wowote ule wa zamani.

    6. Tafuta kwa hakika, kama lipo, tukio au matukio ya uasherati kwa wakati uliopita na wa sasa. Pia itakusaidia kujua kama ni mabikira.

    7. Pata hakika kama uhusiano wa sasa ni mzuri au umejaa matatizo.

    8. Fahamu ni kwa haraka kiasi gani wanakusudia kuoana. Uhusiano usio na hakika wa kipindi kirefu haupendekezwi.

    Mambo Kumi ya Kubaini Kupitia Utambulisho Rasmi wa Mahusiano

    1. Jina na umri wa wote wawili mwanamume na mwanamke.

    2. Tarehe [au muda] uhusiano ulipoanza.

    3. Kwa muda gani wamefahamiana kila mmoja na mwenzake.

    4. Hali yao kuhusu seli mundu [siko seli] kwa wote wawili mwanamume na mwanamke.¹

    5. Hali yao kuhusu VVU kwa wote wawili, mwanamume na mwanamke.²

    6. Hali zao nyingine za kiafya mfano, kifafa, shinikizo la damu, homa kali, n.k.

    7. Historia yao ya kielimu kwa wote wawili, mwanamume na mwanamke.

    8. Uzoefu wao wa kazi kwa kwa wote wawili, mwanamume na mwanamke.

    9. Maarifa kuhusu malezi na makubaliano

    10. Tarehe tarajiwa ya harusi.

    Vipimo vya Seli Mundu [Siko seli] na VVU [Virusi vya UKIMWI]

    Umuhimu wa somo hili ni kuliomba kanisa kuweka masuala ya kipimo cha seli mundu na kipimo cha VVU katika mtazamo sahihi.

    Kipimo cha Seli Mundu

    Kama wenzi wana matokeo ya AA (yaani, ukosefu wa umundu) na AS hakuna tatizo lolote. Iwapo wote wawili wana S (yaani, uwepo wa umundu), mshauri hana budi kuwashauri wavunje uhusiano kwa sababu zifuatazo:

    Kuna uwezekano wa asilimia 25 kuwa na mtoto mwenye SS, jambo linalomaanisha kuwa yeyote kati ya watoto wao anaweza kuwa SS. Pia inaweza kumaanisha kuwa hakuna awezaye kuwa na SS.

    Hali hii pia inaweza kulinganishwa na kupata mvulana au msichana. Kuna uwezekano wa asilimia 50 wa kuwa na mtoto wa kiume au wa kike. Hii humaanisha kuwa mtu anaweza kuwa na watoto wa kiume au wa kike.

    mm1

    Picha Na. 1: Matokeo Yenye Uwezekano wa Kutokea Wakati wa Kipimo cha Seli Mundu

    Kitabibu, mtoto mwenye SS anaweza kuwa na matatizo kama vile:

    1. Kulazwa mara nyingi hospitalini.

    2. Gharama mbalimbali zinazohusiana na matibabu.

    3. Muda mwingi kutumiwa hospitalini.

    4. Uwezekano wa kifo cha ghafla cha mtoto.

    5. Vinginevyo muda wa kutumiwa nyumbani utatumiwa hospitalini.

    6. Hii itakuwa ni mbinyo wa ziada kwa mke (mama) ikiongezewa kwenye majukumu yake yote.

    7. Hili litasababisha magomvi nyumbani na uwezekano wa uhaba wa fedha.

    8. Kuna uwezekano wa hofu ya kifo na ugonjwa wakati wa ujauzito, ambayo pia yaweza kuathiri maisha ya tendo la ndoa kwa wenzi.

    9. Mtoto mwenyewe atakuwa si mwenye furaha kabisa.

    Mshauri anaweza kuwaomba wapendanao kukumbuka kama walishakutana na mgonjwa yeyote wa seli mundu. Hali inayokubalika ni kuwa, wote wawili wanaweza kuwa hasi hawana umundu, au katika hali isiyofaa kabisa, mmoja hasi na mwingine chanya. Kama wote ni chanya basi hali inaweza kuwa ya hatari. Ushauri wa kitabibu uko kinyume dhidi ya ndoa hiyo na ndivyo ilivyo kwa kanisa pia, hata hivyo, uamuzi ni wao.

    Iwapo wapendwa wanaamua kuendelea mbele tofauti na ushauri wote wa kitabibu na kikanisa, bado ndoa yao itabarikiwa. Watasaidiwa kupitia maombi ili kwa neema ya Mungu, wasiwe na watoto wenye uwezekano wa ugonjwa huo.

    Kipimo cha VVU

    Iwapo kila mmoja ni chanya, wanapaswa kushauriwa kwa nguvu kuvunja uhusiano na kusahau mpango wa ndoa kwa sababu zilizo wazi.

    Tanbihi

    1. Geoffrey Chamberlain, ed., Turnbull’s Obstetrics. 2nd ed.(Edinburgh, Scotland: Churchill Livingstone, 1995), 262; Robert Shaw, Patrick Soutter and Stuart Stanton, ed. Gynaecology, 2nd ed. (New York: Churchill Livingstone, 1997), 107; Margaret F. Myles, Textbook for Midwives (Edinburgh: Churchill Livingstone, 1986), 215; E. A. Badoe and S.K. Owusu, ed., Health and Disease: A Layman’s Guide to Good Health (Accra, Ghana: University of Ghana Medical School, 2004), 66 - 69.

    2. Geoffrey Chamberlain, ed., Turnbull’s Obstetrics, 2nd ed. (Edinburgh, Scotland: Churchill Livingstone, 1995), 485; William F. Ganong, Review of Medical Physiology (New York: McGraw-Hill, 2003), 533; E. A. Badoe and S. K. Owusu ed., Health and Disease: A Layman’s Guide to Good Health (Accra, Ghana: University of Ghana Medical School, 2004), 101 -7.

    Sura ya 3

    Kuwashauri Wapendanao

    Baada ya kupokea majibu ya vipimo vya kitabibu vilivyoombwa, jadiliana na wenzi masuala yaliyoibuka kutokana na majibu hayo. Thibitisha uendeleaji wa jumla wa uchumba wao na mjue tarehe inayotarajiwa ya harusi.

    Wakati wa kipindi cha uhusiano wenzi wanatarajiwa wawe watakatifu. Ni muhimu kuwasihi wawe imara kujiepusha na uashearti. Mshauri asiwe ni mtu mwenye kuhukumu. Wenzi hawana budi kutiwa moyo ili wawe hai katika shughuli za kanisa, na kubaki salama katika njia ya utakatifu.¹

    Mambo Yanayokatazwa katika Mahusiano baina ya Wapendanao

    1. Epuka kukumbatiana, kushikana na kubusiana.²

    2. Usikae juu ya mapaja yake.

    3. Usikae chumbani pekee yako na mpendwa wako kwa muda mrefu.

    4. Msikae peke yenu katika sehemu zilizojitenga katika saa zisizotarajiwa.

    5. Usiweke mikono yako ndani ya sketi au kuutembezatembeza.

    6. Usilale kwenye kitanda kimoja na mpendwa wako.

    7. Usivue nguo mbele ya mpendwa wako.

    8. Usishikeshike maziwa, uke na uume.

    9. Usifanye tendo la ndoa na mpendwa wako (huo ni uashearati)!³

    Muhimu: Ushauri-awali kabla ya ndoa huchukua kipindi cha miezi sita. Wapendanao ni lazima wataarifiwe kuanza ushauri wao mapema kadri inavyowezekana ili kukidhi maeneo yote ya ushauri kabla ya harusi.

    Washauri hawapaswi kuukubali mbinyo wa kufanya harusi ndani ya muda mfupi. Jambo hili laweza kuwa na udanganyifu.

    Kwa Mwanamke

    Huchukuliwa kuwa ni kosa la binti [mwanamke] iwapo dhambi yoyote ya uasherati itatokea. Hii ni kwa sababu hata ingawa wanaume kwa kawaida huwa wako kwenye msukumo wa kimapenzi katika mahusiano, mwanamke hapaswi kukubaliana na msukumo huo.

    (a) Binti hana budi kutiwa moyo kuwa mdhibiti wa uhusiano.

    (b) Binti hana budi kutiwa moyo kujidhibiti katika mahusiano. Ni lazima ajiheshimu sana na asimruhusu yeyote kumchafua.

    (c) Ni lazima ashauriwe kutunza ubikra wake barabara ili itakapotokea akishauri hapo siku zijazo, awe na uwezo wa kusema kwa ujasiri kile ambacho hakufanya wakati wa urafiki.

    Kutayarisha Harusi (Orodha-elekezi)

    Jadiliana maandalizi ya harusi na wapendanao na toa ushauri kadri uwezavyo. Gusia yafuatayo:

    (a) Uchaguzi wa ukumbi.

    (b) Vazi la Bibi Harusi – uwezekano wa kuazima ni lazima utajwe.

    (c) Suti (bwana harusi na mshenga wake).

    (d) Gari au magari yatakayotumika.

    (e) Muda ufaao kwa harusi.

    (f) Muda wa kufika kwa bibi harusi – waoneshe mambo ambayo huwafanya bibi harusi wachelewe.

    (g) Usomaji wa Maandiko – uchaguzi wa wapendanao.

    (h) Mwenyekiti (wanaweza kumchagua)

    (i) Mpango wa ukaaji katika meza kuu – ukijumuisha wazazi, mwenyekiti, n.k. (kwa kawaida isiwe na wachungaji).

    (j) Kileo harusini (uwe ukifahamu kuwa baadhi ya wapendanao wanaweza wasiwe na udhibiti juu ya suala hili).

    (k) Pendekezo la ugongeshaji glasi na mwitikio. Shauri kuwa hili lifanywe kwa muda mfupi kadri iwezekanavyo likiwa na maana ya kumshukuru Mungu, wazazi, wachungaji na watu wengine muhimu.

    (l) Vibali muhimu (Halmashauri, Baraza la Mtaa linalohusika na ndoa katika eneo au nchi yako).

    (m) Uchukuaji picha. Kuwa macho na wapiga picha wenye tamaa ambao hawajaalikwa lakini baadaye huja na picha zao walizochukua na kudai fedha.

    (n) Uchukuaji video

    (o) Mapambo

    (p) Mipangilio ya fungate.

    (q) Watahadharishe kutotumia fedha zao zote kwa ajili ya harusi.

    Tanbihi

    1. Dexter Yager and Ron Ball, Dynamic People Skills (U.S.A: InterNET Services Corporation, 1997), 144-145, 153.

    2. Joshua Adjabeng, Before You Marry ( Accra, Ghana: Olive Publications, 1999), 26-27.

    3. Eddie L. Long, I Don’t Want Delilah, I Need You (Tulsa, Oklahoma: Albury, 1998), 192.

    4. Dwight Hervey Small, Design for Christian Marriage (Old Tappan, New Jersey: Fleming H. Revell Company, 1974), 177-201 and Gini Andrews, Your Half of the Apple. God and the Single Girl (Grand Rapids, Michigan: Zondervan Publishing House, 1974), 69-79.

    SEHEMU 2

    MAMBO YA MSINGI

    Sura ya 4

    Fasili ya Ndoa

    Utangulizi

    Ndoa ni taasisi iliyowekwa wakfu na kuamriwa na Mungu.¹ Ni taasisi pekee iliyowekwa kabla dhambi haijaingia duniani.

    Njia Tatu za Kuweza Kuoa au Kuolewa

    1. Ndoa za Kiserikali

    (Hii ni kwa mujibu wa sheria za kijamii za nchi.)

    (a) Katika nchi nyingi, Sheria ya Ndoa huamuru kuwa cheti ni lazima kipatikane kutoka kwa mamlaka ya mtaa au halmashauri, ikitoa kipindi cha miezi mitatu ambacho wenzi ni lazima waoane baada ya majina yao kuwa yamekwishatangazwa kwenye Manispaa/Halmashauri au kanisani kwa wiki tatu. Ikiwa hakuna mtu yeyote apingaye ndoa hiyo ndani ya wiki hizi tatu, ndoa itafungwa.

    (b) Usajili wa kisheria ni lazima usainiwe walau na mashahidi wawili.

    (c) Ridhaa ya wazazi hufaa, inatiliwa mkazo na haina budi kutafutwa sana, lakini si muhimu kwa 100% iwapo wenzi wanazidi umri wa miaka 18.

    (d) Ndoa huvunjika tu kwa njia ya talaka ya kisheria.

    (e) Ni kosa la jinai kuoa tena wakati bado ukiwa chini ya Sheria ya Ndoa.

    2. Ndoa za Kitamaduni/Kimila

    (Hii inahusu uhusikaji wa familia.)

    (a) Familia hukutana pamoja na kwa mujibu wa utamaduni humtoa binti yao baada ya sherehe za kimila kufanywa.

    (b) Sherehe za kimila hutegemea familia na kabila.

    (c) Baadhi ya familia huchukulia jambo hili kuwa ndoa kamili na sahihi kabisa na hutarajia wenzi kuishi pamoja sikuzote.

    (d) Baadhi ya familia huchukulia hili kama uchumba tu, yaani makubaliano ya kuoana.

    (e) Kanisa hili halitambui ndoa za kimila kama ndoa isipokuwa mpaka ibarikiwe na wachungaji. Ndoa ya kimila ni mpango wa kuoa wake wengi. (Hii humaanisha mwanamume anaweza kuoa wanawake wengi kadri atakavyo). Kanisa huamini kuwa ni muhimu kwa washirika wake kuoa chini ya Sheria ya Ndoa kwa sababu ndoa ya kisheria chini ya Sheria hairuhusu uoaji wake wengi.

    3. Ndoa za Kiroho

    (Hili liko hivi wapendanao hula kiapo cha kutii sheria ya Mungu ya ndoa na pia kuwa na ndoa iliyotiwa muhuri na Mungu.)

    (a) Kanisa huendesha viapo na kuwabariki wapendanao.²

    (b) Kwa kadri kanisa linavyohusika, utakuwa hujaolewa isipokuwa mpaka hili lifanyike.

    (c) Kanisa pia huchapa majina ya wapendanao wote wanaotaka kuoana katika ubao wake wa matangazo walau kwa wiki tatu, ili kama kuna kipingamizi chochote cha ndoa, sauti ipazwe. Tunawaka wapendanao wote wawili kujaza fomu zote tatu za ndoa ili kuepuka mkanganyiko na mabishano hapo baadaye.³

    Tanbihi

    1. Al Janssen, The Marriage Masterpiece (Wheaton, Illinois: Tyndale, 2001),3 - 4; Evans A. Laryea, Joining of Lives (Accra, Ghana: PAL International, 2002), 33 - 38; Derek and Ruth Prince, God Is a Matchmaker (Grand Rapids, Michigan: Chosen Books, 2003), 51-52.; Christopher Ash, Marriage Sex in the Service of God (Leicester, England: InterVarsity Press, 2003), 66 - 69.

    2. Marva J. Dawn, Sexual Character: Beyond Technique to Intimacy (Grand Rapids, Michigan: William B. Eerdman Publishing, 2001), 207.

    3. Christopher Clulow, ed., Women, Men and Marriage (London: Sheldon Press, 1995), 40 - 43; Joshua Adjabeng, Before You Marry (Accra, Ghana: Olive Publications, 1999),63 - 67.

    Sura ya 5

    Sababu za Kibiblia za Ndoa

    Utangulizi

    Ndoa si mawazo ya mwanadamu, wala hayakuanzishwa na yeye. Alikuwa ni Mungu mwenyewe aliyebaini hitaji la mwanadamu la kuwa na msaidizi na alilishughulikia hilo. Ili kujua kwa nini Mungu aliasisi ndoa, twahitaji kwenda kwenye Biblia kwa ajili ya kupata majibu.

    Sababu za Kibiblia za Ndoa

    1. Kutatua tatizo la upweke

    Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

    Mwanzo 2:18

    2. Kuwa msaidizi

    Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1