You are on page 1of 2

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-2012: NAOMBA NAFASI NA WABUNGE 357 TU.

Nisiku chache tu zimepita tangu wizara ya elimu kupitia waziri wa wizara hiyo ndugu Shukuru Kawambwa wa wizara hiyo atangaze matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka-2012. Huku bila aibu akisema yakuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri. Sifuri! Yaani Zero. Toba! Halafu tulivyo watu wakujiridhisha kusiko na maana sasa tunasema tunafanya mpango hawa waliofeli waende vyuo vya ufundi. Hapana tusiwadanganye masikini. Kabla na hata baada ya matokeo hayo kulitokea hali ya sintofahamu kutokana na kucheleweshwa kwa matokeo hayo. Uvumi na uzushi ukaanza kuenea hapa na pale. Waenezaji wa uzushi huo hawakuwa na makosa kwani kutokana na hali ya kawaida matokeo ya kidato cha nne hutangazwa wiki ya kwanza ya mwezi wa pili. Nikiwa mmoja wa waathirika wa kusubiri matokeo hayo, nikalazimika kutembelea makabrasha yangu, nikagundua kuwa mwaka jana matokeo hayo yalitangazwa siku ya jumatano tarehe nane mwezi wa pili. Huku Moses Andrew Swai kutoka Feza boys akitangazwa mwanafunzi bora kitaifa. Nilikuwa mmoja wa watanzania waliosubiri matokeo hayo kwa udi. Ni kwasababu katika elimu, mimi huamini kabisa kuwa maendeleo ya kweli kwa Watanzana na Afrika kwa ujumla ndimo yalimo. Niliyasubiri matoeo hayo kama mtego. Huku kumbukumbu ya mjadala juu ya hoja ya ndugu Mbatia pale Bungeni kuhusu Mitaala ya elimu yetu ikiwa bado kichwani mwangu. Nikiwa mpekuzi wa kurasa za mtandao huu wa ndugu yetu wakaribu kabisa bwana Michuzi punde nikauona ukurasa wa matokeo hayo yametangazwa. Kwa desturi, magazetini ni kesho yake kwani bongo wengi hatuna mazoea yakufanya kazi usiku, au mda wa ziada na hata umeme wetu ni manati na wamashaka. Basi kama ilivyokawaida nikatembelea tena mtandao wa wizara hiyo. Mshtuko wa kwanza ni kuwa sikuona majina ya watahiniwa. Nikashangaa kidogo, sio kawaida. Oh! Pengine ni sababu za kiusalama security yamefichwa. Yamechelewa matokeo pengine mwaka huu yamesahihishwa ki-sayansi zaidi labda ndiyo maana yamechelewa. Nikamkumbuka pengine idadi kubwa iliyoongezeka ya shule za kata zileeee za ndugu Edward Lowasa zimeanza kutema watahiniwa kwa wingi. Lowasa alikuwa waziri, na alizipigia sana chapuo shule hizo. Ni kwa ni njema kabisa. Yaani idadi ya watahiniwa imeongezeka mara dufu zaidi. Ikawawia mzigo wasahihishaji na wapanga matokeo kumaliza kazi kwa wakati tarajiwa. Mwaka huu pia ni waziri mwenyewe kachukua rungu na kutangza matokeo hayo kinyume na mamzoea ya ndugu katibu mkuu wa baraza hilo la mitihani mama Joyce Ndalichako. Nini tena! Ahh! Nikawaida mabadiliko hutegemewa. Kwani ni maendeleo. Mabadiliko nikwania nzuri tu kwani huleta maendelao. Haya sasa pengine ni kwania hiyo hiyo watanzania wanajaribu kumshauri pia waziri huyo huyo kwa nia nzuri tu abadili mawazo nakuachia nafasi hiyo ngumu ya u-waziri wa wizara hiyo ngumu pengine kuliko yoyote hapa Tanzania. Yaani wizara ya Elimu ambayo imeshuhudia Ma-daktari na Ma-Profesa, wasomi wa shahada za Uzamivu wakishindwa kuwasaidia watanzania wenzao waweze pia kufikia ngazi hiyo ya elimu kutokana na yaliyokuwa yanatokea wakati kama huu. Matokeo.

NAFASI/MKUTANO NAWABUNGE BILA MALIPO YA ZIADA. Kutokana na hali hiyo tatanishi kabisa yamatokeo kuwa si mazuri sana. Naomba nafasi na wananchi 357 ambao wanaitwa wabunge. Kati yao nawatambua wale 239 Wamajimbo na wale 102 wakuteuliwa ili tuzungumzie matokeo haya. Kwanza tutajiuliza nini mchango wetu katika matokeo hayo. Je tangu 2010 tumewasaidia masikini wetu hao kupitia elimu kwa kiasi gani. Halafu mada ya pili, tutazungumzia nini tufanye baada ya kugundua ni majimbo gani yametoa shule ambazo hazikufanya vizuri, swala la walimu hatutapenda kuwasingizia hawa kwani ishara zinaonyesha kuwa tulisha wasahau. Hapa simuhitaji waziri ndugu Shukuru Kawambwa, bali namhitaji mbunge aitwae Ndugu Shukuru Kawambwa. Pamoja tuzungumzie pia jimbaoni kwake vipi? Mada ya tatu tutajadili pamoja na kwa nia njema kabisa kwanini karibu kila mwaka shule za mwisho zitokee maeneo yaleyale. Japo kwa sasa siamini sana katika vyama, nitawaomba wabunge twende mbali zaidi tujiulize pia ahadi zetu katika ELIMU inamaanisha nini. Mkutano huu utakuwa na staili ya semina ya siku mbili lakini haitakuwa namalipo ya ziada zaidi ya nauli zakuja na kurudi majimboni. Nitawaomba labda tukubaliane ifanyike mkoani Lindi, Mtwara, Tanga, Unguja, Tabora au Rukwa nk. Nia yetu pia iwe nikuona kiasi gani tunaweza kuchangia walao shilingi elfu mbili ili tuweze kuwalipia watahiniwa 28,582 ambao wizara hiyo ilisema matokeo yao yamezuiwa kwa sababu ya kutolipa ada ya mtihani na wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja. Naomba nafasi hii na wabunge kwa sababu wabunge ndiyo wananchi walichaguliwa kutuwakilisha hivyo ni jamaa zetu wa karibu sana. Nawatambua pia wale wakuteuliwa na ambao wapo karibu kabisa na sisi wananchi wao. Wabunge ni ndugu zetu wakaribu tulikunywa nao na kula nao wakati wa kampeni. Kisha tuliwachagua wao sio kutokana pengine na vyama vyao bali wao binafsi tuliwaamini watatusaidia kwenye hili, ELIMU. Na ndugu yenu wakaribu kabisa Frdrick Meela, kwa mguso na mshtuko mkubwa sana wa matokeo hayo.

You might also like