Professional Documents
Culture Documents
(2012/13 FY) na hivi sasa dola za kimarekani milioni 307,675,487/- tayari zimeshatolewa na kutumika. Ripoti hiyo ya Global Fund-Tanzania (2013), pia inaonesha kwamba takriban dola za Marekani milioni 60,657,059/- ziliidhinishwa kununua Dawa Mseto aina ya ACTs na dola za Marekani milioni 44,869,885/- sawa na asilimia 74 tayari zilishatolewa. Licha ya fedha hizi kutolewa, uhaba wa dawa ya Alu bado unaendelea. Ni matarajio yetu kwamba Wizara itaelekeza zaidi juhudi zake kwenye kusambaza dawa ili kuhakikisha uhaba huo unapungua au kuisha hadi kufikia asilimia sifuri. Kwa sasa, bado uhaba wa ALu upo, hususani katika mikoa ileile ambayo awali iliripotiwa na Sikika kuwa na ukosefu mkubwa wa dawa hizo. Si lengo letu kuendeleza malumbano na Wizara ya Afya lakini tunaishauri kwa mara nyingine tena iwajibike zaidi kwa watanzania kwa kununua na kusambaza dawa hizi kwa wakati ili kupunguza vifo vitokanavyo na Malaria kwa watanzania wasio na hatia.
Mr. Irenei Kiria Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, S.L.P. 12183, Dar es Salaam, Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Barua pepe: info@sikika.or.tz, Tovuti: www.sikika.or.tz