You are on page 1of 3

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Cables: "MUHIMBILI" Telephones: +255-22-2151367-9 65000 FAX: +255-22-2150534 Web: www.mnh.or.tz Postal Address: P.O. Box DAR ES SALAAM Tanzania

TAARIFA KWA WANANCHI KUHUSU UBORESHAJI WA HUDUMA MAGONJWA YA MOYO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMILI SEPTEMBA 9, 2013 Awali ya yote nashukuru kupata fursa hii ya kukutana na vyombo vya habari ili kuzungumizia baadhi tu ya mafanikio ambayo Hospitali ya Taifa Muhimbili imeyapata kupitia Kituo cha Upasuaji Moyo na Mafunzo (Cardiac Surgery Treatment and Training Centre. Huduma za Upasuaji Moyo: Kama mnakumbuka tarehe 21 Mei 2008 upasuaji wa moyo ulianza rasmi hapa Muhimbili, ukifanywa na madaktari wetu baada ya kupata mafunzo nchini India na Israel. Wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji katika kipindi cha mwaka mmoja na hadi kufikia leo tayari wagonjwa 453 wameshafanyiwa upasuaji. Upasuaji wa moyo unaofanyika ni sawa na upasuaji katika vituo vikubwa vya upasuaji wa moyo duniani kote. Wataalam wetu wamekuwa wakifanya upasuaji wa kuziba matundu kwenye moyo na kubadilisha valvu ambazo zimebana na kushindwa kuruhusu damu kupita kwenye moyo au kulegea na kufanya damu kuvuja kwenda kwenye sehemu isiyohusika katika moyo na kurudisha moyo katika hali yake ya kawaida ya afya ya mgonjwa. Pamoja na kufanya upasuaji huduma nyingine ambazo zimefanyika na zinaendelea kufanyika ni pamoja na kliniki mbalimbali kama vile za magonjwa ya valve, moyo kupanuka, mishipa ya moyo kuziba, mapigo ya moyo kushuka, magonjwa ya moyo ya kuzaliwa ya watoto na upasuaji wa moyo na mishipa ya damu. Ufungaji wa Vifaa Tiba: Kituo hiki kina vifaa vya kisasa na vya hali ya juu na mahsusi kwa ajili ya kumudu matibabu ya magonjwa makubwa ya moyo. Hospitali inaendelea kutafuta taasisi zenye uzoefu mkubwa wa matibabu ya moyo ili kuanzisha ushirikiano utakaowezesha kupata wataalamu wao kuja kushirikiana na wataalamu wetu kutibu magonjwa makubwa ya moyo hapa hapa nchini kama njia ya kuongeza uwezo kitaaluma. Tunafurahi kuwaambia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa fedha kwa ajili ya kununua mtambo mkubwa wa kuchunguza mishipa na shinikizo ndani ya moyo na maradhi makubwa ya moyo ya kuzaliwa (Catheterization Laboratory). Huu ndiyo mtambo amboa kwa kipindi kirefu umekuwa ukipelekea Serikali yetu kupeleka wagonjwa wengi wa moyo kufanyiwa
1

matibabu nchini India. Mtambo huu umefungwa siku za hivi karibuni, tutaujaribu (testing) mapema mwezi Oktoba mwaka huu. Mtambo huu umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 3.6 Jinsi mtambo wa (Catheterization Laboratory) unavyofanya kazi: Mtamo huu wa Cath Lab ndio unaotusaidia kuangalia mishipa ya damu inayoenda kwenye moyo, kuangalia moyo jinsi unavyofanya kazi na pia kama mtu anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo mashine au mtambo huu unatusaidia kuangalia vitu mbalimbali kwenye moyo wa mgonjwa husika ili kujiridhisha kuona kama kuna jinsi yoyote mgonjwa huyu atanufaika na upasuaji huu. Cath Lab inasaidia pia kuweka kifaa saidizi katika moyo wa mtu (pacemaker) ambacho ni kama betri kinachosaidia kuufanya moyo ufanye vizuri siku zote. Wafanyakazi wa Kituo hiki: Kituo hiki kinahitaji wafanyakazi wa kada mbalimbali wapatao 365 lakini kwa sasa kina watalaam 121. Lakini nafurahi kuwambia kuwa katika mwaka uliopita wa fedha tulipata kibali kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100 ili kukidhi mahitaji halisi ya kituo hiki katika kutoa huduma. Pamoja na hayo tuna changamoto ya kupata watalaam waliobobea katika magonjwa ya moyo ambao hawapatikani kwa urahisi katika soko la ajira. Lakini tunajithaidi kuajiri watalaam ambao tutawapeleka kubobea hususani katika ubingwa wa nusu kaputi, upasuaji na mishipa ya damu, upasuaji wa moyo kwa watoto n.k Gharama za Matibabu: Kama mnavyojua, huduma za maradhi ya moyo zina gharama kubwa na zinahitaji wataalamu wa hali ya juu. Ili huduma hii iwe endelevu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapitia upya utaratibu wa kulipia matibabu ikiwa ni na kuzishauri kampuni zote za Bima ya Afya kulipia wateja wao wanaohitaji huduma mbalimbali za moyo. Kwa kufanya hivyo Kituo kitaweza kujiingizia kipato kitakachotumika kuboresha huduma pamoja na kuweka motisha kwa wafanyakazi. Kituo hiki kitakuwa faraja kubwa kwa nchi yetu na kitaipunguzia Serikali mzigo ikizingatiwa kwamba asilimia 70 kati ya wagonjwa wote wanaopata rufaa ya Serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi ni wagonjwa wa moyo. Mathalan serikali kwa makisio inatumia kama dola za kimerakani 10,000 kulipia gharama za matibabu ya mgojwa mmoja nje ya nchi ukilinganisha na dola za marekani 6,000 mgonjwa akitibiwa katika kituo chetu cha Moyo Kwa hiyo, kuanzishwa kwa kituo hiki kutapunguza matumizi ya Serikali kwa kiwango kikubwa sana. Hata hivyo Serikali inapitia mchakato wa uboreshaji wa utoaji wa huduma pamoja na upatikanaji wa fedha ili kila Mtanzania aweze kupata huduma bora hapa kwetu. Uwekezaji Uliofanywa hadi sasa Ujenzi wa Kituo hiki umejengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Ujenzi pamoja ufungaji wa vifaa hadi hivi sasa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 32 ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechangia kiais cha shilingi bilioni 16,411,741,367 ambapo Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imechangia shilingi bilioni 15,630,769,600. Uwekezaji huu ni wa dhati na tuna kila sababu ya kuipoingeza Serikali zote mbili kwa kazi kubwa iliyofanyika hapa.

Mchanganuo wa uwekezaji umebainishwa katika jedwali lifuatalo;


Na 1 2 3 Maelezo Msaada wa Ujenzi na kufunga baadhi ya vifaa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ujenzi Bajeti ya Maendeleo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kununua vifaa tiba, mitambo na ufungaji katika kipindi cha 2010 2013 Gharama za Uendeshaji kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka mwaka 2008 2012 Jumla Kuu Bei kwa Tshs 15,630,769,600.00 1,900,000,000.00 11,974,000,000.00

3,400,723,973.00 32,905,493,573.00

Utaratibu wa Kutibiwa katika Kituo hiki: Kituo hiki cha Mafunzo na Upasuaji wa Moyo kitapokea wagonjwa kupitia mfumo wa rufaa kwa Hospitali zote zilizothibitishwa kuleta wagonjwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kundi la kwanza ni Hospitali zilizoko katika Jiji la Dar es Salaam ambazo ni CCBRT, Lugalo, Amana, Temeke, Mwananyamala, Hospitali binafsi kama Agha Khan, Hindu Mandal, Kairuki n.k. aidha tutapokea wagonjwa kutoka Hospitali za Rufaa ngazi ya Kanda kama KCMC, Bugando, Mbeya na Hospitali zote za Mikoa, Wilaya na Hospitali Teule. Tumeweka wagonjwa katika makundi matatu yafuatayo; Wagonjwa wa Msamaha Kutokana na Sera ya Msamaha wagonjwa kwa njia hii watachujwa ili kuhakikisha hakuna matumizi mabaya ya sera hii. Aidha tunaweka utaraitibu mzuri wa kuiomba Serikali kulipa fedha zote kwa Hospitali kwa wagonjwa wote watakaopewa huduma kwa njia ya msamaha. Uchangiaji wa gharama za matibabu Hapa ndugu na wanafamilia wa mgonjwa kama ilivyokawaida watatakiwa kuchangia gharama za matibabu ambapo kiasi kingine kitalipwa na Serikali kuu au Serikali za Mitaa kulingana na mgonjwa alikotoka. Wagonjwa wa Kulipia (Private) Kundi hili ni kwa wateja ambao wana uwezo wa kulipia fedha taslimu au kupitia bima za afya mbalimbali ambazo zipo kwa sasa. Baada ya kusema hayo nawashukuruni sana kwa kunisikiliza. Asanteni Dkt. Marina Njelekela, MKURUGENZI MTENDAJI, SEPTEMBA 9, 2013.

You might also like