You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTOAJI LESENI ZA BIASHARA CHINI YA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA. 25 YA 1972 KWA MFUMO WA KUHUISHA NA KULIPIA ADA 1. UTANGULIZI Serikali ilirudisha rasmi utozaji wa ada za Leseni za biashara kupitia Sheria ya Fedha Na.5 ya mwaka 2011. Maandalizi yamekuwa yakifanyika kutoka wakati huo na ada zimeanza kutozwa rasmi 01/07/2013 kwa mfumo wa kuhuishwa (Renewal). Kutokana na marekebisho hayo, utaratibu wa kutoa Leseni za Biashara BILA MALIPO uliondolewa na kusitishwa na Serikali tarehe 30 Juni, 2013. Leseni za Biashara zilizotolewa kuanzia tarehe 1 Julai, 2004 hadi 30 Juni, 2013 ambazo hazikuwa na UKOMO zinatakiwa kupelekwa kwenye Mamlaka zilizotoa Leseni hizo, ili zihuishwe na kulipiwa ada kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa Serikali. Kila mfanyabishara mwenye Leseni ya Biashara anapaswa kujaza Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara na kuambatisha Leseni ya Biashara aliyonayo na kuiwasilisha katika Mamlaka husika, kwa ajili ya kuhuisha na kulipia ada. Maombi yapelekwe katika Mamlaka iliyotoa Leseni husika. Kwa Leseni za Biashara za kundi A kama ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara. Maombi hayo yawasilishwe katika Ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara zilizopo Barabara ya Sokoine Jengo la NSSF-Water front, Ghorofa ya Nne chumba Na. 416. Kwa wale Wafanyabiashara wa Kundi B kama ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 wafike Ofisi za Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya zilizo katika maeneo yao, watapata huduma kutoka kwa Maafisa Biashara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa. 2. UTARATIBU WA KUFUATA ILI KUFANIKISHA ZOEZI NA KUPATA HUDUMA KWA HARAKA 1. Kwa wafanyabiashara wa Kundi A wajaze Fomu ya Maombi ya Leseni za Biashara (fomu inapatikana katika tovuti ya Wizara sehemu ya Marketing Sector (www.mit.go.tz) au fika Wizarani NSSF-Waterfront ghorofa ya 4 chumba Na. 416, Kwa Wafanyabiashara wa Kundi B wawasilishe maombi Ofisi za Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya zilizo katika maeneo yao; 1

2. Waambatishe Leseni za Biashara za kudumu walizonazo na kuwasilisha kwenye Mamlaka husika kama ilivyoainishwa hapo juu; 3. Kwa wafanyabiashara wa Kundi A wafanye malipo kupitia Benki ya CRDB mahali popote kwa kutumia Account Number 0150413356300; jina Revenue Collection Trading License-MIT. Wafanyabiashara wa Kundi B wataelekezwa Benki ya kulipia na Halmashauri zao; 4. Kwa wafanyabiashara wa Kundi A wawasilishe pay slip ya Benki ghorofa ya Mezanine (NSSF-WaterFront) kwaajili ya risiti ya Serikali, Wafanyabiashara wa Kundi B wataelekezwa Ofisi ya kuwasilisha ili wapewe reisiti ya SerikaliMweka Hazina wa Halmashauri; 5. Kwa wafanyabiashara wa Kundi A wawasilishe Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara, Leseni ya Biashara na risiti ya malipo ghorofa ya 4 kwa ajili ya kuandikiwa Leseni ya Biashara, Wafanyabiashara wa Kundi B wataelekezwa ofisi ya kupeleka na kuandikiwa Leseni ya Biashara ofisi za Biashara za Halmashauri. Waombaji wapya wa Leseni za Biashara mnapaswa kujaza fomu ya maombi ya Leseni za Biashara na kuambatisha nyaraka kama inavyojieleza katika fomu ya maombi na kufuata hatua ya 1 hadi 5 kama ilivyoelezwa hapo juu. Mnashauriwa kuhuisha na kulipia ada Leseni za Biashara mapema kabla ya tarehe 31 Desemba, 2013 ambapo adhabu na faini kwa wafanyabiashra watakaochelewa kuhuisha (Renew) itaanza kutolewa tarehe 1 Januari, 2014. 3. TAHADHARI Wafanyabiashara mnatadharishwa kuwa hapa mjini kuna mawakala wasio waaminifu maarufu kwa jina la VISHOKA. Mnashauriwa kuwaepuka na muweke utaratibu wa kufuatilia Leseni za Biashara zenu wenyewe. Kwa wale ambao, wameshaletewa Leseni za Biashara na mawakala waliowatuma mnashauriwa kwenda kwenye Mamlaka iliyotoa Leseni husika kwa ajili ya kufanya uhakiki kwa kuwa imebainika kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya biashara kwa kutumia Leseni batili (Feki) TAFADHALI FIKA NA KUFANYA UHAKIKI KWA FAIDA YA BIASHARA YAKO. MAELEZO ZAIDI YANAWEZA KUPATIKANA PIA KWA KUTUMIA ANUANI IFUATAYO: Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, S. L. P. 9503, Simu Na-+255-22-2127897/8, Fax: +255-22-2125832 Website www.psmit.go.tz DAR ES SALAAM. 2

WIZARA YAVIWANDA NA BIASHARA

You might also like