You are on page 1of 1

UTUMISHI WA UMMA NI NINI?

Kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Utumishi wa Umma ya mwaka 1999 (toleo la Pili la mwaka 2008), utumishi wa umma ni mfumo wa kiutawala na kimenejimenti uliyokabidhiwa jukumu la kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma inayokusudiwa kutoka kwa serikali yao au taasisi yoyote kwa niaba ya serikali kwa kuzingatia sera, sharia, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali. NI MAKUNDI GANI YA WATUMISHI YANAYOUNDA SEKTA YA UTUMISHI WA UMMA? Kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Utumishi wa Umma ya mwaka 1999 (toleo la Pili la mwaka 2008), makundi yanayounda sekta ya utumishi wa umma ni, (a) utumishi wa serikali kuu, (b) utumishi wa serikali za mitaa, (c) utumishi wa sharia na mahakama, (d) utumishi wa afya, (e) utumishi wa waalimu, (f) utumishi wa kisiasa, (g) utumishi wa huduma za kawaida (operational service), (h) utumishi wa taasisi na wakala za serikali zinazojitegemea na vyombo vingine vya umma, (i) utumishi wa jieshi la wananchi Tanzania, (j) utumishi wa bunge, (k) ututmishi wa jeshi la polisi, (l) utumishi wa jeshi la magereza, (m) utumishi wa uhamiaji, na (n) utumishi wa zimamoto na uokoaji.

You might also like