You are on page 1of 4

1

. ZINAZOWAKABILI SAFARI YA UKAWA KUELEKEA IKULU:NGUVU YAO NA CHANGAMOTO


Tarehe 28 mwezi wa Aprili,2014 nikiwa napitia taarifa mbalimbali za kisiasa nilikutana na kichwa cha
habari kilichokuwa kinasema "UKAWA kusimamisha mgombea mmoja wa Uraisi".Kwangu mimi
haikuwa taarifa ya kushtua sana bali ilinifanya nitafakari kuhusiana na uhalisia wa tamko hili
walilolifanya.Swala lililonitafakarisha zaidi halikuwa tu hoja yenyewe iliyotolewa bali pia
majira(season) ambapo taarifa hii imetolewa.Wanasaikolojia husema-"Usitoe ahadi nzito aidha
wakati umefurahi sana au umekasirishwa sana".Sababu ya msingi ni kuwa mara nyingi katika
mazingira hayo utatoa ahadi bila kuwa na muda mzuri wa kufanya uchambuzi wa ndani wa ahadi
unayoitaka.Na nikajiuliza,wametoa ahadi hii baada ya kutafakari sana au ni kuwa wamekasirishwa
sana au kufurahi sana?
Lakini hadi hatua hii unaweza ukawa unajiuliza swali,kwa nini kichwa changu cha makala yangu
kinaeleza hatima ya UKAWA na kuelekea IKULU na sio kuelekea KATIBA MPYA?.Ni muhimu kulieleza
hili kwa sababu ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa umoja huu wa katiba ya wananchi unaofupishwa kwa
jina la UKAWA umeendelea kuonyesha ajenda zaidi ya Katiba katika muelekeo wake.Kama ambavyo
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mheshimiwa Freeman Mbowe alivyoeleza katika mkutano huo na
hapa nina nukuu-"Hivi sasa kwa swala la sisi kuungana kwa maana ya kuwa na nguvu ya pamoja
halikwepeki.Siasa ni dynamics(zinabadilika).Fikra za jana ni tofauti na fikra a leo,kwa hiyo ni ukweli
usiopingika kwamba tunahitajiana kwa manufaa ya watu wetu na nchi yetu" Tamko rasmi la UKAWA
kuelezea lengo lao la kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi mkuu nafasi ya urais na pia
kuwa na mgombea mmoja katika nafsi za ubunge,ni ishara wazi kuwa lengo lao la kupata katiba
linaweza kufunikwa na lengo la kushinda uchaguzi.Na hili si jambo la kushangaza hata kidogo kwani
lengo la kwanza la chama chochote cha siasa ni kuchukua dola.Kama wakifanikiwa kuunganisha
nguvu yao,bila shaka uhaguzi ujao utakuwa na ushindani mkubwa ambao haujawahi kutokea.
Wapo wanaowakosoa UKAWA na kusema kuwa maazimio kama haya yalishawahi kusemwa huko
nyuma lakini hayakufanikiwa.Na wengine wanasema ni urafiki wa kinafiki hasa kati ya CUF na
CHADEMA ambao walionekana kuwa maadui wa waziwazi ilipofika wakati CHADEMA walipoamua
kutowahusisha CUF katika kambi yao rasmi ya upinzani bungeni.Wapo wanaosema pia kuwa UKAWA
haina usajili kama chama cha siasa au kama wanataka kuwa na coalition(muungano) katiba yetu
hairuhusu kufanya hivyo.Hizi ni changamoto za kweli lakini ni nyepesi sana kuzikabili na kuzitatua
kwa watu weye malengo thabiti kisiasa.Katika changamoto ninazoziona mbele yao hizi si changamoto
za muhimu kabisa.
Nikianza na hoja ya wale waanaosema kwamba walishawahi kufanya maazimio kama haya na uadui
wa CUF na CHADEMA.Kwenye siasa husemwa hakuna adui wala rafiki wa kudumu ila kuna malengo
ya kudumu.Ni kawaida sana maadui wa kisiasa wa jana ukawakuta ni marafiki wa kudumu sana wa
leo.Nani alijua kama Steven Masato Wasira aliyegombea kwa chama cha upinzani na kumshinda
waziri mkuu mstaafu Jaji warioba hata baada ya kufunguliwa kesi,leo hii yuko ikulu katika sehemu
nyeti ya nchi;hiyo ndiyo siasa.Nchi jirani ya Kenya imethibitisha hilo baada ya mahasimu wakubwa wa
siasa Rais Uhuru Kenyata na Makamu Wake William Ruto kuuunganisha nguvu kwa swala la
kuchukua nchi.Huu unaweza usiwe mfano madhubuti(perfect example) hasa kwa kuzingatia Uhuru
na Ruto walitumia nguvu ya makabila yao lakini kwa mafunzo ya jumla ni mfano muhimu wa kisiasa
wa jinsi maadui wa jana wanavyweza kugeuka kuwa marafiki wa karibu wa kesho. Kwa ufupi ni
2

kwamba kwenye siasa tofauti za jana zinaweza zisiwe na nguvu sana katika maamuzi ya leo ya
wanasiasa na hii ndio maana CHADEMA wametangaza kuwajumlisha CUF na NCCR katika kambi ya
upinzani katika majira haya ya kujijenga kisiasa.
Swala la kuwa UKAWA haina usajili wa kudumu nayo ni hoja isiyoweza kuwa kizuizi cha kudumu kama
kweli wana dhamira ya dhati.Inawezekana sheria isiweze kuruhusu kwa sasa vyama hivi kuwa na
muungano(coalition) lakini sidhani kama ni jambo lisilowezekana hasa kwa kuzingatia kuwa tuko
katika wakati strategic wa wao kuweza kulifanikisha hilo wakati joto la mabadiliko ya katiba
liaendelea.
Kuna mambo mawili ambayo UKAWA wameamua kuyafanyia timing ya kisiasa.Moja ni Fursa ya
kisiasa-wameamua kutumia mjadala wa katiba kujiimarisha kisiasa kwa kutafuta hoja wanayoamini
itakubaliwa zaidi na wananchi na itakuwa chanzo cha wao kuungwa mkono katika harakati za
uchaguzi mkuu ujao.Mjadala huu unawapa uhalali wa kufanya mikutano na kuelezea malengo na
sera yao kwa wananchi,kwa maneno mengine wanapata nafasi ya kueleza ilani zao ingawa bado si
rasmi.Ingawa bado wanakabiliwa na changamoto katika hoja yao ya katiba hasa katika mfumo wa
serikali kama nitakavyoeleza hapo chini,bado kisiasa ni wakati muafaka kwao kutumia vuguvugu hili
wakati wananchi wanatamani sana kusikia kinachoendelea.Pili wameamua kuwaonyesha wananchi
kuwa lengo lao kuu ni kuitakiwa mema nchi bila kujali tofauti zao,hii ndio maana wameamua
kuungana pamoja.Hatua hizi zote zinalenga kuongeza imani yao kwa wananchi kuelekea uchaguzi
mkuu.Na ni ukweli usiopingika kuwa lipo kundi kubwa la wananchi watakaokaa upande wao kwa
kujiuliza-kama wameamua kuweka tofauti zao zote hizi kisiasa lazima watakuwa na nia njema na
nchi yetu.Au haiwezekani vyama vyote hivi viwe na lengo baya lazima CCM ndiyo itakuwa ina nia
mbaya katika hili.Haya ni mawazo yenye maana sana katika hatima ya chama au wanasiasa wowote
wale katika kuelekea kushinda uchaguzi.
Pamoja na fursa za UKAWA bado naziona changamoto nyingi ambazo si rahisi sana(sijasema
haiwezekani) kuzishinda kwa muda mfupi hasa kwa kuzingatia malengo yao ya kushinda uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015.
Changamoto ya kwanza ni nani atasimama kama mgombea Urais kati yao?Hili si gumu sana kwa
baadhi ya vyama lakini ni swala la muhimu kati ya CHADEMA na CUF.Kwa NCCR-Mageuzi wanaweza
wakawa tayari kukubali mgombea mmoja kirahisi hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba katika chaguzi
zilizopita ukiacha ule wa mwaka 1995,nguvu ya NCCR imeendelea kupungua kitaifa na hata katika
ubunge wakibakiza nguvu yao Kigoma tu na hasa inayotokana na umahiri wa wagombea na sio
uthabiti wa chama chenyewe.Pengine wangesimamisha mgombea aliyesimama katika chaguzi
uliopita Mh.Hashimu Rungwe,lakini kura alizopata wakati ule zilikuwa ni 26,388 sawa na asilimia 0.31
,hii ni idadi ndogo sana kuonyesha ushawishi wake.Hata hivyo Hashimu Rungwe akiwa na Hassan
Mmbwana aliyekuwa Kamishina wa NCCR Mageuzi wa Mkoa wa Tanga walitangaza kuhamia Chama
cha Ukombozi wa Umma(CHAUMA) wakitupia lawama ya kukosekana kwa demokrasiaa ndani ya
NCCR-Mageuzi.Pengine aliyebakia angekuwa ni Mwenyekiti wa chama Taifa,James Mbatia,lakini
swali kubwa linabaki kama alishindwa kupata ushindi katika uchaguzi wa ubunge jimbo la KAWE ,je
ataweza kuleta ushawishi ngazi ya taifa?hesabu za kisiasa zinakataa.Hizi ni sababu tosha kwa NCCR
kuwa tayari kutosimamisha mgombea katika uchaguzi mjao katika umoja wao na badala yake
3

kuwaachia CHADEMA na CUF waamue hili.Lakini kwa kufanya hivyo ni ukweli usiopingika kuwa NCCR
watabaki kuwa ni wadau wasio na nguvu katika umoja huu.
Kwa aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa alipata 2,271,941 ambazo ni sawa na
silimia 26.34 huu kwakwe ni mtaji mkubwa hasa ukizingatia mambo mawili.Kwanza tofauti yake na
mshindi wa kwanza Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827(61.7%) ikiwa ni tofauti ya kura
3,004,886.Nadhani mkakati wa chadema ulikuwa ni kuongeza idadi ya kura ili kushinda uchaguzi ujao
au kuendelea kujijengea nguvu yao ya kisiasa,na hii ndio sababu inayoifanya chadema kushiriki kila
uchaguzi hata ule ambao kwa uwazi inaonekana hawatashinda,nia wakati mwingine si ushindi bali ni
kujitambulisha zaidi na kuvutia wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi ujao.Kwa upande mwingine tofauti
yake na aliyekuwa mshindi wa tatu Prof:Ibrahim Lipumba aliyepata kura 695,667 sawa na asilimia
8.06 ni kubwa sana(significant),tofauti ya kura 1,576,274 hivyo kwa mahesabu inaonekana itakuwa ni
vyema kwa Dr.Slaa kusimama kama mgombea wa umoja huo.Lakini je,urahisi wa namba hizi ndio
utakuwa urahisi kwa Prof:Lipumba kukubali kutogombea?
Naamini haitakuwa rahisi kwa CUF kukubali kumwachia Dr.Slaa kuwa mgombea hata pamoja na
ushawishi wa takwimu hizo.Ukweli ni kuwa CUF kwa bara wana nguvu katika maeneo ya pwani zaidi
na maeneo machache yasiyo ya pwani.Lakini kwa sasa CUF ni sehemu ya serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar,hii ni kusema wako kwenye nafasi nzuri kuendeleza nguvu yao katika visiwa hivyo na hata
kuwa na matumaini kuchukua nafasi ya Urais katika siku zijazo.Mkutano wa UKAWA uliofanyika hivi
majuzi Zanzibar,ni wazi kuwa ulikuwa ni kwa manufaa ya CUF kwa kuzingatia wafuasi finyu wa vyama
vingine katika UKAWA.Hata kama tumaini la kushinda uchaguzi wa urasi wa muungano si kubwa sana
kwao,bali ili kuendelea kubaki kuwa chama cha nchi nzima na kushikilia ngome zao bado kuna
umuhimu mkubwa wa CUF kuendelea kupata kura kwa kumtumia Prof;Lipumba katika kugombea
nafasi ya Urais.Tofauti ya CUF ni kuwa ingawa wananguvu kubwa Zanzibar kuliko bara lakini wana viti
vya UBUNGE pande zote mbili na Prof:Lipumba huwa anapata kura kutoka pande zote mbili.Lakini
kwa CHADEMA ni tofauti hawana hata mbunge mmoja upande wa Zanzibar.Kwa mantiki nyingine
katika nafasi ya Urais wa muungano,CUF inaonekana ni chama cha jumla zaidi kuliko wenzao wa
CHADEMA.
Katika mchakato huu wa katiba mpya,maslahi yanayofanana(common interest) kwa vyama hivi ni
kushika dola,lakini maeneo yanayolengwa ni tofauti.Kwa CHADEMA Tanzania bara ni muhimu sana
kwa hatima yao ya kisiasa kwani kwa upande wa Zanzibar ni kama imeshindikana kujipenyeza
kabisa.Kwa CUF upande wa Zanzibar ni muhimu zaidi kuliko upande wa Tanzania Bara kwani nguvu
yao ni dhahiri na imethibibitishwa na ushiriki wao katika serikali ya umoja wa kitaifa(SUK).Kwa
mantiki nyingine pamoja na kutaka kuunga mkono matakwa ya wananchi lakini kwa jicho la kisiasa ni
kusema kuwa kama serikali ya Tanganyika itapatikana itakuwa ni muhimu kwa ushindi wa CHADEMA
kwani kura wanazopata wagombea wa Urais wa CCM zinazopigwa na wazanzibari ni kikwazo sana
kwao na kwa upande wa CUF Zanzibar ni muhimu sana kwao kwani bila nguvu ya CCM ya bara
Zanzibar ni ngome ya asili ya CUF.Kwa maneno mengine uimara na uhai wa CCM Zanzibar
unategemea sana msaada wa karibu kutoka Bara.
Katika kutimiza haja yao ya kuunga mkono rasimu hasa umuhimu wa serikali mbili,UKAWA hawana
budi kujikita katika kuulewesha umma hasa kujibu hoja ngumu kwa upande wao ni namna gani
gharama za uendeshaji hazitaongezeka kwa kuwa na serikali tatu.Hoja ya gharama ndio hasa
4

ambayo haijaeleweka kwa wananchi,wakifanikiwa kuieleza hii na ikakubaliwa kuungwa mkono katika
hoja ya serikali tatu itakuwa ni rahisi sana.Ndani ya vyama vya upinzani nimewahi kusikia maoni
yanayotofautiana pia;kuna wale wanaoamini katika marais watatu na kuna wale wanaosema tuwe na
rais mmoja ila mawaziri wakuu 2 kila upande wa muungano,hili nalo lazima wakubaliane katika
kufanikisha kuungwa mkono na jamii.Nimesikia wakisema kuwa hakuna utafiti wa kisayansi
uliofanywa ili kuthibitisha gharama itaongezeka.Lakini ukweli ni kuwa hakuna utafiti uliofanywa wa
kuonyesha gharama itapungua ndani ya serikali tatu,kwa nini hawataki wananchi waamini kuongeza
idadi ya serikali ni kuongeza gharama?Ili kujenga ushawishi wao katika hili,watafute kampuni
inayoaminika ifanye utafiti wa kitaalamu ili watumie taarifa hiyo kuwa kama authority yao katika
kuthibitisha kuwa gharama hazitaongezeka.
Kwa upande wa chama tawala naona kuna makosa makubwa yanayofanyika katika kutetea hoja
yao.Nguvu kubwa imewekwa katika kushambulia wapinzani na kueleza ubaya wa serikali
tatu,ikiwemo mbinu ya kuwawekea hofu wananchi wa vita na kuvunjika kwa muungano.Hoja hizi
hazitaleta matunda wanayoyataka,kwa historia zilitumika pia katika kupinga mfumo wa vyama vingi
lakini umaarufu wa Mrema ulithibitisha kuwa hoja za kutia hofu haziwezi kushawishi watu wakuunge
mkono badala yake watataka kujua zaidi kuhusu unayetaka wamuogope na matokeo yake wanaenda
kuwa wafuasi wake.Badala yake,CCM inatakiwa ijikite katika kueleza umuhimu wa serikali mbili na
kujibu kwa ufasaha swali gumu kwa upande wao-kama kero zimeshindwa kuisha kwa miaka yote ya
muungano itawezekanaje kuaminini mfumo huu?Pia maoni ya rasimu ni maoni ya wananchi kwa
nini wao wanayapinga?Kundi la wanaotaka serikali 2 hizi ndizo hoja za msingi za kujibu na kushawishi
umma.
Katika uchaguzi mkuu uliopita idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 20,137,303, waliopiga kura ni
8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha,hii ni changamoto inayoikabili
UKAWA kuwabadilisha WASHABIKI kuwa WAPIGAKURA.Wanaweza wakazunguka nchi nzima lakini
kama idadi kubwa ya wafuasi wao si wapiga kura waaminifu hasa maeneo ya mijini,matokeo
yatawashangaza itakapofika wakati wa kupigia kura rasimu ya katiba.
Katika kukuza demokrasia haya ni mambo yanayoweza kutarajiwa kila wakati,ila si rahisi kama
inavyoweza kuonekana kwa nje.Ni kweli UKAWA wanataka kuingia IKULU,ni muhimu wakazizingatia
changamoto hizi zinazowakabili.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Joel Arthur Nanauka
jnanauka@gmail.com
0688-67 79 68

You might also like