You are on page 1of 7

AMA KWELI UKIWA MUONGO IPO SIKU UTAUMBUKA. TENA KWA MH. MBUNGE KAMA HUYU Mh.

HALIMA MDEE KIOO CHA JAMII AMBAE AMECHUKUA DHAMANA YA WANANCHI ANAWAWEKA
REHANI WANANCHI KWA KUKUBALI KUNUNULIWA ETI ILI TU KUMCHAFUA Mh. WAZIRI TENA Profesa
ALIEPEWA DHAMANA NA UMOJA WA MATAIFA KUWA KIONGOZI NA KUFANYA MAKUBWA DUNIANI
ILIMLADI TU KUMPAKA MATOPE HAIWEZEKANI KAMWE. SASA Mh. MDEE JIBU TUHUMA HIZI
IWEZEKANAVYO. UONGO WAKO HAUNA NAFASI KWA WATANZANIA KWANI NI WATU MAKINI
WAELEWA NA WACHAMBUZI.
Mheshimiwa spika
Kuna mambo kadhaa ambayo ninasyaleta kwako kimaandishi kwa hatua stahiki chini ya sheria za bunge
,kama sehemu ya majibu yangu.
A. Kwanza ni tabia ya mhe Halima mdee waziri kivuli wa ardhi,nyumba na maendeleo ya
makazi,kuwa anaiba nyaraka za wizara na kazi zake na kuzichapisha,tena neon kwa neon kama
kazi yake,na kwa upotoshaji mkubwa.ni fundi wa cut and paste na mara nyingi aya zake
haziendani zinajikanganya .nimechoka na tabia hii na nimevumilia vya kutosha.katika hotuba
yake ya mwaka jana aliiba nyaraka za wizara za rasimu ya andiko la utafiti wa mashamba
.nikavumilia .sasa ameiba nyaraka ya siri niliyokuwa ninamwandikia mhe waziri mkuu
nikimtaarifu hatua niliyofikia na kuomba maelekezo kuhusu mchakato wa kuhamisha wananchi
wa chasimba huko bunju dare s salaam .
Mheshimiwa spika ,nielewavyo mimi mhe mdee ametenda kosa la kujipatia barua iliyokuwa
imeelekezwa kwa mhe waziri mkuu bila kunakiriwakwake jambo ambaloni kosa chini ya sheria
ya usalama wa taifa ,sura ya 47,toleo la 2002(classified information).ninaelekeza suala hii kwako
mhe spika ili uwasiliane na mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu hatua stahiki kwa wizi
huu.ninikabidhi pia nakala ya barua hiyo aliyoiba na utaona kwamba ameinakili verbatim na
ndiyo chanzo cha kupoyosha na kunishambulia na kubeza juhudu ninazofanya kwa kukamilisha
kazi niliyoagizwa na waziri mkuu(kiambatanisho).
B. Mheshimiwa spika ,jambo la pili ni uongo uliosheheni katika hotuba ya msemaji mkuu wa kambi
rasmi ya upinzani bungeni .halima james mdee kuhusu mapitioya utekelezaji wa bajeti ya
2013/2014 na makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya
makazi kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Ninawasilisha lalamiko hili kwako chini ya kanuni za bunge (toleo la aprili 2013),kanuni ya 64
(1)amayo inasema
Bila kuathiri masharti ya ibara ya 100 ya katiba inayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na
majadiliano katika bunge ,mbunge(i)hatatoa ndani ya bunge taarifa ambazo hazina ukeli.
Kama ninavyoonesha hapa chini mhe mdee amesema uongo na upotoshaji mwingi dhidi yangu
kama ifuatavyo:

MGOGORO WA ARDHI BAINA YA WANANCHI WA CHASIMBA BUNJU DAR ES SALAAM
KIWANDA CHA SARUJI NA HARUFU YA WIZI NA UFISADI.
1. Anadai kwamba waziri ameomba shs 15,000 kwa sq.m lakini anawali[pa wananchi shs
5,000 kwa sq.m kwa hiyo amejipatia kiudanganyifu shs 10,000/sq.m.kwa kuwa mhe
mdee tayari alishaiba barua na nyaraka husika zilizoelekezwa kwa waziri mkuu ,alijua
kwamba fidia ilioombwa ni shs 5,000 kwa sababu wa ufinyu wa bajeti .anabuni na
kuuliza uongo huu kwa makusudi ya kunichafua.alete ushahidi wa madai yake.kama
asingelikuwa na hila angeuliza nieleze fidia ilikuwa kiasi gani kwa nini ilipungua ,siyo
kusema shs 10,000 imekwenda wapi? Athibitishe kwanza ilitolewa lini ili na mimi
niweze kumjibu ilikokwenda?.
2. Wananchi wanaohama ni 4096.viwanja vinavyoombwa ni 4,500.viwanja vilivyosalia ni
404 ni vya nini?mhe mde anauliza swali hili kwa hila kama uongo kwa sababu
anatambua kwamba katika zoezi la chasimba kaya hazijulikani kikamilifu na zimekuwa
zikiongezeka kadri wananchi wanavyojitokeza.kwanza kulikuwa na kaya 902
zilizokwenda mahakamani ,zikaongezeka hadi kaya 3,336 nilipofanya mkutano na
wananchi desemba 2012, zikaongezeka hadi kaya3,990 wakati wizara ilipokamilisha
zoezi mara ya kwanza na kuongezeka kwa kaya nyingine 106 zilizojitokezakuomba
zifanyiwe tathmini nje ya muda.jumla ikawa 4,096 nilipoandika kwa waziri mkuu.kwa
mtu anayejua shughuli ya mipango miji zoezi sharti liwe na viwanja vya ziada.na kama
wananchi wa chasimba zaidi hawatajitokez,ni dhahiri viwanja vitagawiwa kwa watumiaji
wengine.suala lak ni uongo na upotoshaji waziri anaonekane ameiba viwanja adhibitishe
wizi huo.
3. Anadai kwamba waziri,mthamini mkuu na mkurugenzi wa upimaji wa ramani wamejilipa
mamilioni ya posho katika zoezi .alete ushahidi wa mamilioni ya posho yaliyolipwa kwa
waziri,mthamini mkuu na naibu katibu mkuu ambaye alikuwa mkurugenzi wa
upimaji(dr.sellasie mayunga).
4. Anadai selikari imejigeuza dalali kutekeleza maagizo ya mahakama ambayo hukumu
imejaa utata mkubwa.alete uthibitisho wa utata huo katika hukumu ya mahakama ya
rufaa,ambayo anataka serikaliisitekeleze!je anahamasisha wananchi kuasi amri ya
mahakama?
5. Alete uthibitisho jinsi gani serikali ikikopa na kulipa kwa tax credit payment sytem
iliyopendekezwa, viwango vya kodi vitaathirika kivipi kwa sababu kila mwaka kuna
muswada wa fedha?.aoneshe kwanini hazungumzii jambo hili kiupotashaji kwa sababu
anajua fika kwamba kulipa deni kwa kupunguza kodei ya kila mwaka hakuizuii serikari
kuongeza viwango vya kodi mwaka hadi mwaka, kadri itakavyohitajika na kuamuliwa na
bunge inapopitisha bajeti.
6. Alete ushahidi kwamba shirika la TAWILAT halikutoa huduma ya elimu na mengineyo
kama ilivyotakiwa katika mchakato wa kutatua mgogoro.je yeye kazi iliyotakiwa
kufanywa na TAWILAT anayodai haikufanywa anaifahamu ?kwa kuwa kazi zilizofanywa
na TAWILAT zilianishwa kinaga ubaga katika barua ya waziri mkuu ambayotayari mhe
mdee alishajipatia isivyo halali,aoneshe kwa nini madai yake siyo hila kunichafua mimi
wazi wazi kuwa nmemdanganya waziri mkuu.
7. Alete sheria inayonizuia mimikama waziri wa ardhi,tena niliyekuwa mkurugenzi
mtendaji wa UNHABITAT iliyoanzisha na inafadhili shirika la TAWLAT kulitumia kufanya
kazi hizo nchini kwangu Tanzania.kwa juhudi zngu nikiwa umoja wa mataifa,taasisi hizi
zilianzishwa katika nchi za afrika kama kiunganishi cha wananchi maskini hasa
wanawake na vyombo vya fedha katika kuboresha nyumba na maisha yao
mijini,ikiwemo Tanzania (TAWLAT), Kenya (KEWLAT),Uganda (UGWLAT),Ghana
(GAWAT),na Mozambique (MOZAWLAT).waziri wa ardhi mstaafu mhe john chiligati
(mb.)alishilikiana na TAWLAT na kufanya kazi nao kabla mimi sijarejea nyumbani.kwa
hiyo TAWLAT ni mojawapo ya mashirika wadau w wizara ya ardhi na nyumba.ni dhahiri
kwamba tangu nirejee nimekuwa nikiisaidia taasisi hii katika shughuri zake kadhaa .ni
wajibu wangu!mhe mdee alete mgongano wa wa masilahi kama si hila na fitna
kuchafua.aidha alete ushahidi unaonizuia mimi kuwasiliana na kiwanda na kukishauri
kuwezesha taasisi kama TAWLAT kuisaidia serikali katika kutekeleza zoezi hili nyeti
baada ya kujua UNHABITAT imepatia ujuzi?. Jeanajua tofauti ya kushauri na
kulazimisha? Anajua kuwezesha na kulea? Anafikiri nchi hii itaendelea bila
viongozi,hususan mawaziri,kuzisaidia taasisi ambazo ziko chini ya sekta zao kujiendesha
na kupata kazi za kufanya? Je anajua maana ya ulezi na uwezeshaji?
8. Nijuavyo mimi,hadi sasa kwa hiari yake,kiwanda kimetoa fedha za kuwezesha
uhamishaji wa wanachi kutoka chasimba kama ifuatavyo:
a. Shs 250 milioni zilitolewa kwa halmashauri ya kinondoni kuhamisha wananchi
kwenda mlandizi jambo ambalo halikufanikiwa ;
b. Shs 50 milioni kwa halmashauri ya kinondoni kwenda mabwepande,jambo
ambalo halikufanikiwa;
c. Shs milioni 150 kwa wizara ya ardhi kupuma na kuthamini kazi ya
chasimba,ambayo inaendelea na
d. Shs takribani 80 milioni kwa shirika la TAWLAT kwa kazi mbali mbali kadri
inavyohitajika hasa katika elimu kwa viongozi kukabiliana na fitna na vikundi
hasi kama vile mungiki vinavyotishia zoezi zima pamoja na kuzua migogoro
mipya na upotoshwaji na kuwasumbua viongozi wa wanachi. (kwa mfano
wakati wa zoezi la kubadilisha benki accounts,wanachi Fulani waliharibu gari la
diwani wa bungu mhe.sharif majisafi (CCM)na nikaitaka TAWLAT kumkodishia
gari wakati gari lake lilinafanyiwa matengenezo polisi wakikamilisha
uchunguzi.katika dynamics za urban recocations,kama huna uwezo wa
kuhudumia dharura kama hizi katika muda kwa hiyo ndiyo maana unakuwa na
taasisi zenye uwezo huo!mhe mdee anaingilia kazi ambayo haielewi kwa ndoto
za kufikiri fedha hutolewa ili viongozi wa CCM wajinufaishe.(it is an obsession
on her part). Mimi ninarudia sina haja ya kupata fedha kutoka TAWLAT
nilizonazo zinatoshereza mahitaji yangu madogo ya kawaida.maisha yangu
hayana makuu!
Mheshimwa spika pia nifafanue kwamba malipo haya ya awali ni hiari kutoka
kwenye kiwanda cha saruji,na wala siyo sehemu ya bajeti ya kiselikari
inayozungumziwa katika barua yangu. Kwa kuwa wizara ilikua haina bajeti ya
kufanya kazi hiyo, nilikiomba kiwanda kutoa fedha kwa wizara kama vile nilivyofany
kwa TAWLAT, kama sehemu ya cor porate social responsibility ya kiwanda. Nikatoa
taarifa kwa WM kwamba takriban sh.300 million zimetolewa ( Nikimaanisha kwa
wizara na TAWLAT) na shs. Million 300 na Halmashauri ya kinondoni kama
anavyodai ukurasa wa 27. Aonyeshe kwanini anasema uongo kupotosha umma
kwamba Taasisi ambayoanadai ninamahusiano nayo tayari imelipwa sh. Million 600
(300+300) na kiwanda na halmashauri?
9. Alete ushahidi kama pendekezo langu kwamba kiwanda kisimamie ulipaji wa fedha
kurahisisha procurement kilishakubaliwa bila kuweka taratibu zinazostahili na mamlaka
husika ambayo ni hazina na TRA na kama matumizi hayo yasingewasilishwa? Aonyeshe
madai yake kwamba hiyo deal nilikua ninaipeleka ki usiri kwa waziri mkuu na si
kushirikisha mamlaka zote husika ili nazo zitoe ushauri wake ili sheria, taratibu na kanuni
zifuatwe wakati tunatekeleza kazi kwa kuzingatia muda
10. Aeleze kama waziri sina wajibu kupendekeza kwa waziri mkuu mawazo yangu na kwa
mamlaka nyingine husika? Je ni kosa gani kuwa mbunifu katika utendaji kazi katika zoezi
kama la chasimba? Aoneshe kwanini si uongo na upotoshwaji kugeuza mapendekezo
yaonekane kama njama ya kupindisha sheria na kuiibia serikali?
11. Aoneshe kuna kosa gan kuwashauri na kuwashawishi na kuwaelimisha wananchi wa
chasimba kufungua benki accounts CRDB, NMB, na NBC ambazo zina matawi huko
chasimba? Kati ya wananchi 4,096 waliothaminiwa tayari wananchi 3360 wameitikia
zoezi na wamefungua benki account zao ili malipo yao yapitie benki? Mhe Mdee
aoneshe jinsi gani tungeliweza kuwaburuza wananchi hao benki kufungua account bila
kufanikiwa kuwashawishi wakafanya jambo hili kwa hiari? Aoneshe kwanii anataka
kuwapotosha wananchi wabaki kwenye umasikini? Kwanini anapinga maendeleo na
kutaka kukwamisha mradi kwa propaganda chafu. Anahujumu kazi yangu baada ya
kuwa ameonesha ushirikiano wakati Fulani, ni kigeu geu kwa maslahi gani?
12. Aoneshe kwanini anazungumzia TAKUKURU kufanya uchunguzi kama uongo na
propaganda ili aandikwe kwenye magazeti. Kwakuwa tayari kaiba barua za serikali kama
sio hila ya kisiasa kwanini basi , kwakuwa amemkamata mwizi na fisadi, hajapeleka suala
hili TAKUKURU ili wafanye kazi yao kimya kimya? Na je anafikiri vyombo vya serikali
kama vile TAKUKURU vimelala usingizi vikimsubiri Mhe Mdee katika suala linalo
shugulikiwa kiushirikishwaji na idara mbali mbali za serikali?

Mheshimiwa Spika, suala la tatu linahusu uongo na hila katika kile anachodai ni harufu ya
ufisadi katika utafiti ili kunichafua katika kazi ngumu tena tuliyofanya kwa hoja zake za
kiuchochezi.
(C)
TATHMINI YA WIZARA JUU YA WAMILIKI WAKUBWA WA ARDHI:
13. Mhe Mdee alete ushahidi wa jinsi kama waziri wa ardhi nilivyoweza kuingiza jamaa
zangu kwa kuwataja katika utafiti uliokuwa unafanywa na mtaalamu mwelekezi
aliyepewa tenda ya kufanya kazi hii ambaye ni idara ya uchumi ya chuo kikuu cha Dar es
salaam. Aoneshe jamaa zangu walioingizwa katika utafiti huo ni akina nani na tuna
uhusiano gani. Aoneshe jinsi nilivyoweza kushinikiza mtaalam mwelekezi ambaye ni
chuo kikuu cha Dar es salaam kuwaajiri wataalam nje ya matakwa ya mkataba waliosaini
kwa hiari. Chuo kikuu cha DSM kinaweza kulazimishwa kusaini mkataba wa kifisadi?
Hata heshima ya kawaida kama siyo kwangu angalao itolewe kwa taasisi ya elimu
kongwe kama UDSM na wataalam wake?

14. Alete ushahidi wa kiasi kikubwa cha fedha kilichonirudia mimi kama waziri akionesha
linikililipwa kwangu na nani alinilipa?
15. Alete ushahidi kwamba wataalamu walinisusia na nikalazimika kujifungia na wasaidizi
wangukukamilisha kazi ?ni wataalamu gani walionisusia ,awataje kwa majina?je
anamaanisha kuwa mtaalamu mwelekezi alishindwa kazi?ni kweli kwamba baada ya
kupokea ripoti nilitaka marekebisho na tukayajadili kwa kina.je kama waziri ambaye ni
mtaalam wa suala lilokuwa linatafitiwa sina haki na wajibu wa kusoma andiko na
kumwelekeza mtaalam mwelekezi aboreshe andiko lake lifikie viwango ambavyo
vilitakiwa ?je watendaji wa wizara ya ardhi baada ya kupokea andiko walikuwa hawana
haki na wajibu kufanya editing andiko likae vizuri na kukidhi vigezo vya kiserikali kabla
halijakabidhiwa bungeni?alete ushahidi wa madai yake au aeleze kwa nini analeta hila
na fitna kuchafua jina langu katika kazi ambayo tayari alitulazimisha tufanye katika
dharura.kumbe hoja yake ililetwa kwa hila mbaya.

16. Alete usahidi kwamba hakuna mchakato wowote wa manunuzi uliofanyika kumpata
mtaalam mwelekezi wa kufanya kazi ya uhakiki wa mashamba makubwa zaidi ya eka
50.njia iliyotumika ni ya ununuzi wa dharura(emergency procurement under single
source method).ununuzi huu uliwezeshwa chini ya kifungu cha sheria ya ununuzi wa
ummaya 2004 Na.59(2)(b)(c)na kanuni Na 95(1)GN Na98 ya 2005.sababu ya ununuzi wa
dharura ulitokana na hoja binafsi aliyoitoa yeyemwenyewe mhe mdee akitaka kusitisha
shughuli zote za ugawaji wa ardhi mpaka mashmba makubwa yathaminiwe,akidai ,ati
ardhi yote imeuzwa kwa wawekezaji? mhe mbowe ,kiongozi wa kambi rasmi ya
upinzani ndiye alipendekeza na bunge (la novemba 2012)likaridhia na kuazimia kwamba
shughuli za ugawaji ardhi zisitishwe lakini tathmini ifanyike na kuletwa katika bunge la
april,2013,yaani katika kipindi cha miezi 4.kwa hiyo ilikuwa dharura na mchakato
ukaanza januari 2013 kwa kumteua chuo kikuu cha dare s salaam idara ya uchumi
kufanya kazi hiyo .bodi ya wazamini ya wizara (mimi siyo mjumbe)ilimpitisha mtaalam
mwelekezi katika kikao chake cha tarehe 7 januari,2013.mhe mdee aoneshe kwamba
haya hayakutokea la sivyo alisema uongo.
(D)
TUHUMA ZA KUMILIKI ARDHI KIFISADI
17. Athibitishe jinsi nilivyomiliki eneo la ha 800 kiujanja huko kyamyorwa,wilaya ya muleba
,nikitumia nafasi yangu kama mkurugenzi wa UN-HABITAT,na kuwahamisha wamiliki
halali kutoka katika eneo hilo .awalete wamiliki halali niliowadhulumu ,lini
niliwadhulumu na UNHABITAT ilihusika vp?

18. Athibitishe eneo kubwa ninalomiliki huko kigamboni .liko wapi,nililipata je,nililipora
kutoka kwa nani na lini?alete walalamikaji niliopora eneo lao.

19. Athibitishe eneo la ekari 100 ninazomiliki bukoba mjini ,ziko wapi,nimezipora au
kuzipata kutoka kwa nani na nani mlalamikaji.

(E)
TUHUMA ZA KUTOSHIRIKIANA NA KATIBU MKUU(uk 62)

20. Alete ushahidi kuthibitisha kwamba katibu mkuu wa wizara hakushiriki kama
inavyopaswa katika shughuli za kazi za wizara zote ambazo yeye mdee amezishambulia
ikiwemo chasimba na kigamboni?athibitishe kama katibu mkuu amelalamikia
hashirikishwi.

(F)
UTENDAJI DHAIFU UMOJA WA MATAIFA
Nimalizie kwa kufafanua suala la utendaji wangu UN ambalo nalo mhe mdee anataka kulipotosha
,kunifanya sifai,eti kiongozi dhaifu.
Kuhusu utendaji wangu UNHABITAT na UN kwa ujumla mhe mdee hata akinibeza ni kazi bure.labda
nichukue nafasi kulieleza bunge lako tukufu jambo hili lieleweke,for the record.
Ninabakia kuwa mwanamke mwafrika wa kwanza na mpaka sasa wa pekee aliyechaguliwa kwa kupigiwa
kura na baraza la umoja wa mataifa (UN general assembly)(tena mara mbili,2001 na 2005)kuongoza
mojawapo ya mashirika yake,UNHABITAT.kazi yangu ya msingi ,UNHABITATilikuwa ya kuchaguliwa siyo
kuteuliwa kwa hiyo issue ya kuwa demoted kutoka nafasi hiyo haipo kama anavyodai mhe mdee
akisoma gazeti la daily nation la Kenya la mwaka 2009,bila kufanya utafiti.

Kilichojiri pale nikwamba mimi nilikuwa na kofia mbili. Kwanza ni nafasi yangu ya kuchaguliwa kama UN
undersecretary general and executive director wa UNHABITAT. Pili ni kuteuliwa mwaka 2006 na kofi
annan kuwa mkurugenzi mtendaji wa makao makuu Nairobi(Director General of the UN Office at
NairobiUNON) baada ya mjerumani aliyekuwa katika nafasi hiyo kustaafu kutoka ukurugenzi wa unep
(Dr. Klaus Toepfer).
Kwa kuwa makao makuu ya Nairobi yana mashirika mawili tu, uneo na UNHABITAT, basi the senior most
UndersecretaryGeneral katika kituo ndiye alikuwa anakuwa Director General wa UNON. Hata hivyo 2009
katibu Mkuu mpya Ban Ki-Moon, baada ya kuielewa UN, alikuja kugundua kwamba alikuwa kimsingi ana
wanawake wawili watanzania katika ngazi za juu
Kabisa za un. Hii noi kwasababu alimteua mtanzania dr. asha rose migiro kama naibu wake.
Baadhi ya mataifa ya ulaya yakamshinikiza atoe nafasi ya Nairobi kwa mwenzao aliyekuwa ameshika
nafasi unep (dr. achim steiner), wakidai sasa ana watanzania wawili katika nafasi moja?
Moja kwa vipi? Kwa sababu nafsi ya naibu katibu Mkuu wa umoja wa mataifa, ni nafasi amabayo
kimuundo wa un, zamani ilikuwa inaitwa Director General at headquarters kabla ya mataifa makubwa
hayohayo kumshinikiza kofi annan alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu kuibadilisha hiyo nafasi kuipa hadhi
ya deputy un secretary general na akamteua Canadian louise frochette katika nafasi iyo. Un ina makao
makuu 4 yaani New York, Geneva, Vienna na Nairobi. Na wawakilishi wa vituo hivi huitwa Director
Generals.
Kwa hiyo Ban Ki-Moon, march 20009 akaniondoa katika nafasi yangu ya Director General of unon
pamoja na kwamba nilibaki the senior most undersecretary general at Nairobi. Kwa kuwa taratibu za
umoja wa mataifa zilikuwa haziruhusu, uamuzi huo ukazua upinzani mkubwa hasa kwa wafanyakazi wa
magazeti yakaandika sana. Opia wanawake walipinga na hata kuandamana. Waliokuwa kwenye kampeni
hiyo chafu kuniengua mimi mwafrika ili wamsimike mjerumani ndio walikuwa wanaandika mambo hayo
kwenye magazeti, kwa mfano mafisadi niliokuwa ninawashughulikia hapo Nairobi nikiwa mkurugenzi wa
unon. Mhe mdee anakiri kwamba sikuhusika katika hizo multimillion dollars scandals ingawaje sasa
anapiga propaganda kwamaba nilikuwa dhaifu? Kwa taarufu mimi ndiye niliitisha audit iliyoonesha
ufisadi huo, na waliobanwa walikuwa sehemu ya kampeni ya kuniondoa UNON lakin
wasigeliwezaKuniondoa unihahbitat maana hapo nimechaguliwa.
Kitendo cha Katibu Mkuu Ban Ki-Moon kuniondoa katika ukurugenzi tendaji wa unon kilizua tafran
kubwa. Mataifa mengi, ikiwemo marekani na African group, yaliona nimeonewa na kudhalilishwa. Kwa
kuwa nilikubalika sana kama shupavu baraza la umoja wa mataifa, desemba 2009, lilisitisha uteuzi wa
achim steiner wa unep na kumuagiza Katibu Mkuu Ban Ki-Moon kumwondoa katika nafasi hiyo, na
badala yake wakaunda nafasi nyingine ya UndersecretaryGeneral of the un office at Nairobi, ambayo
Katibu Mkuu aliagizwa aijazae na Mwafrika. Hivi sasa imekaliwa na mwanamke kutoka Ethopia. Hiyo
ndiyo record yangu ya utendaji UN. Mhe Mdee hawezi kuniondosha kwa kueneza propaganda za
mafisadi niliowashughulikia kutoka gazeti la Kenya na kuisambaza mbele ya umma wa watanzania bila
ufafanuzi.

You might also like