You are on page 1of 3

JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA

(ALAT)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


KUZINDUA MCHAKATO WA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA
MIAKA 30 YA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA
Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) ilianzishwa rasmi tarehe 13
Disemba 1984 kufuatia kuanzishwa upya kwa mfumo wa Serikali za Mitaa
mwaka 1982.Kwa kuzingatia umuhimu na maendeleo yaliyofikiwa katika
sekta ya Serikali za Mitaa nchini Mkutano mkuu wa 30 wa Jumuiya uliofanyika
jijini Tanga uliazimia kufanya maadhimisho ya kitaifa ya sherehe za miaka 30
ya ALAT na Serikali za Mitaa.
Katika kipindi cha miaka 30 Jumuiya pamoja na Serikali za Mitaa nchini
zimepata mafanikio mengi ya kujivunia na hivyo wakati tunafikisha miaka 30
kuna kila sababu ya kujivunia, kuonyesha na kuwaeleza wananchi juu ya
mafanikio hayo.
Baadhi ya mafanikio yanayostahili kutajwa ni pamoja na Kushawishi na
kufanikisha utungaji wa Sera ya Kupeleka Madaraka kwa wananchi The
Policy Paper on Decentralization by Devolution, Kushawishi na kufanikisha
kupandishwa mishahara na marupurupu ya Wakurugenzi na watendaji
wengine wa halmashauri ili kulingana watendaji wengine wa Serikali;
Kuandaa kitabu cha Kiada cha madiwani (councillors Handbook) na kutoa
mafunzo ya madiwani kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani
na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI; Kushawishi na kutungwa kwa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya Serikali za Mitaa Na. 6 ya Mwaka 1999,Uanzishwaji
wa kada ya Maafisa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa na kuondokana na
Makatibu Watendaji wa Vijiji/Kata, Uanzishwaji wa Sherehe ya Wiki ya
Maadhimisho ya Serikali za Mitaa, Kubuni mbinu za kufadhili Mikutano Mikuu
ya ALAT Taifa, Kupitisha hatua mbalimbali za Mpango wa Kuijengea Uwezo
Jumuiya uofadhiliwa na Ubalozi wa SIDA (ALAT institutional Strengthening
Project).

Kubuni na kusimamia Mradi wa Ushirikiano wa miji katika kujenga uchumi


jamii (Municipal Partnership for Local Economic Development- MPED) n.k.
Leo tunazindua mchakato wa maadhimisho ya za miaka thelathini ya ALAT
na Serikali za Mitaa mchakato ambao utaenda sambamba na utekelezaji wa
shughuli mbalimbali zifuatazo zitakazotufikisha katika kilele cha sherehe hizo
mwezi April 2014; moja ni shughuli ya kutangaza mafanikio ya ALAT na
Serikali za Mitaa kupitia mkanda wa sinema (CD) iliyoandaliwa ili jamii
ifahamu mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 30 ili kuendelea
kujenga hoja kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuzitumia Serikali zao za
Mitaa katika kuwaletea maendeleo kupitia mipango mbalimbali ikiwa ni
pamoja na uimarishaji uchumi kwa jamii (local Economic development).
Pili, kuendelea kukusanya taarifa kutoka kwa wanachama juu ya utekelezaji
wa mkakati wetu wa kuondoa tatizo la madawati shuleni. Tatu, kufanya
maandalizi ya mpango wa kumzawadia meya/ mwenyekiti wa Halmashauri
aliyefanya vizuri katika halmashauri yake (mayors Award). Mpango huu
utakuwa
hatua
zifuatazo;
uombaji
(nomination),
kutangaza
(announcements), kuwapigia kura wenyeviti/mameya wa Halmashauri na
utoaji wa zawadi utakaofanyika wakati wa kilelele cha maadhimisho ya
miaka 30 ya ALAT na Serikali za mitaa. Nne; kuendelea kufanya maandalizi
ya sherehe za miaka 30 ya ALAT na Serikali za mitaa nchini pamoja na
maandalizi ya Mkutano Mkuu.
Napenda kuchukua fursa hii kuziomba taasisi, mashirika, wabia wa
maendeleo na wadau wa Serikali za Mitaa nchini kujitokeza na kuchukua
fursa mbalimbali za kufadhili sherehe hizi zitakazofanyika sambamba na
Mkutano Mkuu wa Jumuiya pamoja na mpango wa kuwazawadia
Mameya/wenyeviti wa Halmashauri.
Nawashukuruni sana kwa kunisikiliza na sasa natoa fursa ya kuuliza maswali.
Mwisho

Mwenyeki wa ALAT Taifa na Meya Wa Jiji la Dar es Salaam


13 Disemba 2014

You might also like