Bank Tanzania imezindua mikopo ya nyumba ya masharti nafuu ikiwemo muda wa miaka 20 kulipa. Mikopo hii italeta faraja kubwa kwa mamilioni ya Watanzania wenye ndoto za kumiliki nyumba. Meneja wa mauzo wa First National Bank Tanzania, Emmanuel Mongella akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya FNB Home loans leo jijini Dar es salaam alisema kuwa benki hiyo sasa imeanza kutoa mikopo ya nyumba kwa riba nafuu ambazo zinapangwa kutokana na uhusiano wa mteja na benki na vilevile uwezo wa kukopesheka. Wateja wetu watafurahia huduma ya haraka na kupatiwa mikopo katika muda wa siku tatu. Na katika miezi mitatu ya kwanza tangu uzinduzi, wateja wetu hawatalipia gharama za huduma katika mchakato wa kupata mikopo, alisema. FNB inaamini kwamba huduma hii itakuwa ni suluhisho kwa wale wote wanaotafuta mikopo ya muda mrefu ili kununua nyumba na kukarabati nyumba. Mikopo hii ya FNB inaweza kulipwa taratibu kwa kipindi cha miaka 20 Mshauri wa Mikopo ya Nyumba wa FNB, Patricia Nguma alisema mikopo hiyo itagawanyika katika
makundi manne ambayo ni; Mkopo wa kununua
nyumba (home Purchase loan) Mkopo wa kumalizia nyumba (Home completion loan), mkopo wa kuwekeza nyumba na kupata fedha (Home equity loan) na kuhamisha mkopo toka benki nyingine (Home switch loan). Mikopo ya nyumba ya FNB imelenga kuwapa faraja linapokuja suala la kujenga na kumiliki nyumba na vilevile kufanya ukarabati wa nyumba. Watu kutoka maeneo yote ya jamii wanaweza kuomba mikopo hii, alisema. FNB ni benki iliyosambaa barani Afrika iliyoanza kutoa huduma kusini mwa jangwa la Sahara tangu mwaka 1874. Hivi sasa FNB inapatikana Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zambia, Mozambique, Lesotho, Swaziland na Tanzania. Benki hii imedhamiria kuwa taasisi bora zaidi ya kifedha barani Afrika. FNB Tanzania ilifungua milango yake rasmi nchini Tanzania mnamo Julai 27, 2011. Sinza na Mbagala ni tawi la 6 na 7 jijini Dar es Salaam; mengine ni tawi la posta, tawi la maeneo ya viwanda, tawi la Peninsula, tawi la Kariakoo na tawi la Kimweri. FNB ina dhumuni kubwa la kuwa mdau muhimu katika maendeleo ya sekta ya fedha na imepanga kuendelea kuanzisha huduma zenye ubunifu na utaalamu wa
hali ya juu hapa nchini na hakika FNB inazingatia
kauli mbiu yake isemayo Tukusaidiaje? Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu www.fnbtanzania.co.tz au tuma barua pepe kwenda info@fnb.co.tz