You are on page 1of 2

WITO WA WANANCHI KUHUSU TOZO/ KODI YA LAINI YA SIMU YAFIKA BUNGENI

Wito wa maelfu ya watanzania uliokusanywa na jukwaa la Change Tanzania kupitia mtandao na mikoa mbalimbali nchini imepokelewa na mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye hivi sasa ameshaanza kufanya kazi ya kuandika muswada binafsi wa kupendekeza tozo hili lifutwe. Hivi karibuni bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha muswada wa sheria ya fedha iliyosainiwa na rais Jakaya Kikwete na kuanza kutumika kama sheria kuanzia Julai mosi. Sheria hii imetaja chanzo kimojawapo cha mapato kama tozo ya shilingi 1,000 kwa kila laini ya simu (sim card). Kama mwitikio wa sheria hii, wananchi wengi kwenye mitandao ya kijamii walilipinga tozo hili na kwa kupitia jukwaa la Change Tanzania, juhudi zilianza za kukusanya maoni ya wananchi kwa njia mbili: kwa njia ya mtandao online petition na kwa njia ya kukusanya sahihi za wananchi mitaani kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha, Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Morogoro, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Singida, Songea, Zanzibar na mikoa mingine. Pamoja na matamko mbalimbali ya serikali kuhusu kusitishwa kwa tozo hili hata hivyo sheria inayohalalisha ukusanyaji wa tozo hili haijafutwa na ni Bunge la Jamhuri ya Muungano pekee yenye uwezo wa kufuta tozo hili kandamizi inayomkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini kwani 67% ya wananchi wanaishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs 2,000) kwa siku. Takwimu zilizotolewa na makampuni ya simu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Ni wajibu wa kila mbunge kusikiliza sauti za wananchi wao waliowatuma bungeni na wito huu ni sauti za wananchi wakihimiza Bunge na wabunge kuchukua hatua mara moja kuhakikisha kuwa kisheria tozo hili linafutwa. Change Tanzania inampongeza mbunge Halima Mdee kwa usikivu wake na kwa kuchukua hatua mara moja na inawahimiza wabunge wengine bila kujali itikadi kuungana na mbunge huyu kufanikisha kufutwa kwa kodi hii. Kuhusu Change Tanzania: Change Tanzania ilianza mwaka 2012 kama mwamko wa wananchi waliopo katika mtandao yaani social networks kwa maana ya Twitter na Facebook ya kutaka kujadili masuala yanayohusu nchi yetu kama wananchi bila itikadi ya kisiasa na kwa kuzingatia umuhimu wa kuwajibisha viongozi wa ngazi zote na hivyo kuleta mabadaliko chanya katika jamii yetu kwa njia ya mjadala. Baada ya kupata wanachama zaidi ya elfu 20

(20,000) ndani ya mwezi moja, baadhi ya waanzilishi wa kikundi hiki cha mtandao waliisajili kama kampuni isiyo na hisa yaani isiyotengeneza faida (not for profit company). Leo hii ChangeTanzania ina wanachama zaidi ya elfu 30 Facebook, na wafuasi zaidi ya elfu 6 (6,000) Twitter. Pia tuna blog na ukurasa wetu wa internet (website) www.changetanzania.org. Change Tanzania haipokei msaada wowote wa kifedha au udhamini kutoka mashirika mengine, vyama au taasisi bali hutegemea michango ya wanachama wake tu. Maria Sarungi Tsehai MRATIBU Simu: +255 784 235215 Barua pepe: sarungim@gmail.com

P.O. Box 105133, Dar es Salaam, TANZANIA +255 22 2182405 | +255 784235215 info@changetanzania.org | www.changetanzania.org

You might also like