You are on page 1of 4

Kichwa cha somo: UPENDO WA BWANA

Wimbo :No:199 .UPENDO NI FURAHA

Fungu kuu: Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu

kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

*Tunapozungumzia upendo tunamzungumzi Bwana mungu maana yeye ni Upengo siyo tu


kwamba upendo ni tabia ya Mungu bali ni asili yake mandiko matakatifu yanatuweka
wazi :

1YOHANA 4:8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.16.
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo,
naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

*Tunapaswa kutambuwa kwa kuwa upendo ndiyo asili ya Mungu kila anachofanya ni
upendo, hata sheria yake ni upendo hata ghadhabu yake na hukumu zake ni upendo.

MATHAYO 22:36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?


37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa akili zako zote.38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.39 Na ya pili
yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.40 Katika amri hizi mbili
hutegemea torati yote na manabii.

CHIMBUKO LA WOKOVU WETU NI KATIKA UPENDO WA MUNGU:

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

WAEFESO 2: 4 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu
aliyotupenda;5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha
pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

TITO 3: 3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi,
tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu
na husuda, tukichukiza na kuchukiana.4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na
upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;

Watu wengi wanachanganyikiwa wanaposikia neno Wokovu, inakuaje Mungu Mwenye


uwezo Muumba wa vyote asitumie nguvu au mamlaka yake kuwaokoa wanadamu?

ROHO YA UNABII :The Desire of Ages / Tumaini la Vizazi Vyote ; Page 6 Chap : God with
us / Mungu pamoja na si

" The earth was dark through misapprehension of God. That the gloomy shadows might be
lightened, that the world might be brought back to God, Satan's deceiptive power was to
be broken. This could not be done by force. the exercise of force is contrary to the
principles of God's Government; He desires only the service of love; and love can not be
commanded; it can not be worn by force or authority; Only Love is Love awakened
" Kwa kuwa ulimwengu haukumjua Mungu, giza nene liliifunika dunia, ili kulimulika na
kuliondoa giza nene na kuirudisha dunia mikononi mwa Bwana, ilibidi kuzivunja hila za
mwovu shetani.
Jambo hilo halikuhitaji matumizi ya nguvu, kwa maana matumizi ya nguvu ni kinyume na
kanuni za serekali ya Mungu; Mungu huridhia huduma ya upendo; na upendo
haushurutishwi; na haupatikani kwa matumisi ya nguvu wala mamlaka; Upendo pekee
huamsha Upendo"

kanuni za Serekali ya Mungu upendo ndio mkuu kuliko kitu chochote sio kama serekali za
dunia zenye kuacha majeraha makubwa na visasi katika mioyo ya wanadamu. Ndiyo
maana japo tupo katika dunia serekali yetu nambari moja inapaswa kuwa ya Mbinguni na
kanuni hiyo ndiyo tuifuate

MATHAYO:20:25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa


huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
26 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na
awe mtumishi wenu; 27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe
mtumwa wenu.

Upendo wa Mungu ni tofauti sana na upendo wa Mwanadamu, muimbaji moja aliandika na


kusema " Hata Bahali zote na maziwa vijapo kuwa wino na majani yote yawe kalamu na
mbingu ziwe karatasi havitoshe kuandika maelezo kuhusu upendo wa Mungu"

Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa
ajili ya rafiki zake.

Upendo wetu sisi una mapungufu sana" Kisa cha Mwanamume aliedai kumpenda mke
wake na kuitangazia dunia nzima, upendo wake ulipojaribiwa kwa kutoa figo yake
kumuokoa mke wake huyo, akashindwa."

Kitabu kiitwacho " Beyonde Beliefs by Jack Sequaira, page 10


"human love is self-seeking. Since we are by nature egocentric, everything we do or
think, in and of ourselves, is polluted with self-love or selfishness. Socially, politically,
academically, materially, economically, even religiously, we are all slaves to our
own way
Upendo wa kibinadamu ni wa ubinafsi. kwa kuwa tuna u mimi kiasili, kila tunalofanya au
kuwaza ndani na kwa ajili yetu sisi, kimeathiliwa na kujipenda wenyewe pamoja na
ubinafsi, yawe ni mahusiano yetu na jamii, siasa, elimu, mali, uchumi, hata katika mambo
ya dini, sisi sote ni watumwa wa njia zetu wenyewe."
ISAYA 53: 6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake
mwenyewe...
WAFILIPI 2: 21 Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.
Neno upendo limegawanyika katika sehemu kuu nne kama lugha ya kiyunani (kigiriki
inavyoelezea) neno upendo kwa kingeleza lina msamiati moja "Love" na hili hutumika
katika kueleza kila utitili wa aina ya upendo, lakini kwa Kiyunani amabayo ni lugha ya
agano jipya tunaweza kuelewa aina ya upendo ili tuweze kutofautisha upendo wa Mungu
kwetu na upendo wa wanadamu.
Storge:Huu ni upendo wa kifamilia kumpenda mtu wa damu yako
Philos: Upendo wa kirafiki
Eros : Ni upendo wa kimahaba
Pendo hizi zote zimejengwa juu ya maslahi na sababu fulani fulani huo na mara nyingi hizi
huwa zina dosali na zina eksipaya (expire).
AGAPE: Upendo wa kweli (genuine and pure love) yani huu ni upendo usiochanganywa
(undiluted ) usiochakachuliwa, Usio wa kawaida huu ndiyo upendo wa Mungu.
A. Upendo wa Mwanadamu una Masharti lakini Agape(Upendo wa Mungu) hauna
masharti
MATHAYO 5:44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni
wanaowaudhi,45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye
huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

B.Upendo wa mwanadamu una Kigeugeu lakini Agape hauna kigeugeu

YEREMIA 31: 3 Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa
milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.

C.Upendo wa Mwandamu ni wa Kujipendeza nafsi Agape ni wa Kujikana nafsi.

WAFILIPI 2: 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule
kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa
wanadamu;8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa
mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.\

UDHIHILISHO WA UPENDO WA MUNGU

Upendo wa Mungu (AGAPE) usio na masharti, usio na kigeugeu na wakujikana nafsi


ulidhihilishwa pale msalabani Mwana wa Mungu na Bwana Wetu Yesu Kristo alipokubali
kufa na kuangamia pale msalabani katika mauti ya Pili iliokuwa ikitukabili kwa sababu ya
dhambi zetu.

RUMI 5: 8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo
alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

WEBRANIA 2: 9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani,
Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa
neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.

Yesu alipokufa pale msalabani haikuwa mauti hii ya usingizi tunayopatwa nayo sisi, kwa
sababu mauti hii ya kwanza haiwezi kuihukumu dhambi, mauti ya pili ndio Mwisho wa
dhambi na wadhambi na hii ndio iliokuwa mauti ya Msalaba Yesu alikua tayari kuangamia
na asiwepo milele ili mimi na wewe tuishi milele!

Ufunuo wa Yohana 2:11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia
makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Ufunuo wa Yohana 20:6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na
sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa
makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.

Upendo ndiyo siri ya wokovu wetu, bila upendo isingewezekana kutuokoa dunia imefika
pabaya kwa sababu upendo hatuna upendo.

ROHO YA UNABII INASEMA; Desire of Ages/Tumaini la vizazi vyote, pg444 chapter ; It is


Finished / Imekwisha.

"God could have destroyed Satan and his sympathizers as easly as one can cast a pebble
to the earth; but he did not do this, rebellion was not be overcome by force. Compelling
power is found only under Satan's government. The lord principles are not of this order.
His Authority rests upon goodness, mercy, and love; and the presentation of this principles
is the means to be used. God government is moral, and truth and love are to be the
prevailing power.

"Mungu angeweza kumuangamiza shetani na wafuasi wake kirahisi kama kubwaga


uchafu chini: lakini hakufanya hivyo kwa maana uasi huu usingekomeshwa kwa matumizi
ya nguvu, matumizi ya nguvu ni jambo ambalo linatumika chini ya utawala wa Shetani.
Kanuni za Mungu ni kinyume na utaratibu huo. Mamlaka ya Mungu msingi wake ni Wema,
Rehema na Upengo. namna Alioitumia ilikua ni kudhihilisha kanuni hizo. Serekali ya
Mungu ni Adili, Ukweli na Upendo ndio nguvu yake ya Ushindi.

1WAKORINTHO 13:13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na
katika hayo lililo kuu ni upendo.

Upendo wetu umepoa : MATHAYO 24:12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo
wa wengi utapoa.

Nasi tunaweza kuwa na upendo wa kweli tukilijua hili

1WAKORITHO 13: 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo


hautakabari; haujivuni;5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu;
hauhesabu mabaya;6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;7 huvumilia yote;
huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo
lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
1YOHANA 4:20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni
mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda
Mungu ambaye hakumwona.21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye
ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.

WITO : Ni wangapi wanasema ewee Bwana Yesu kaa ndani yangu ili uniambukize
upendo wa agape, kama ulivyonipenda mimi nami nimpende Mungu kwa moyo wangu
wote na kwa akili zangu zote na jirani yangu kama nafsi yangu, uniwezeshe kutoa mali
zangu na muda wangu kwa mguso wa upendo wa agape ili kuwasiadia wahitaji.

Yuko mtu ambaye ni kama mimi ambaye anasema nimeusaliti upendo wa Bwana kiasi cha
kufanya maovu yasiyoelezeka, na nataka nizaliwe upya kwa maji (ubatizo) na kwa Roho
(Utakaso) ili nife kwa ubinafsi nifufuke kwa upendo wa Agape, Tembea uungane nami
tusimame mbele za Bwana tumulilie atuokoe.
Bwana Awe nanyi Daima.

You might also like