You are on page 1of 1

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

10 SEPTEMBA 2017

MAKUSANYO YA KODI MWEZI JULAI SEPTEMBA 2017


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa taarifa ya makusanyo ya mapato ya kipindi
cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi
Septemba 2017, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.65.

Makusanyo haya ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama
hicho kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Katika kipindi hicho cha miezi mitatu, makusanyo ya kila mwezi yalikuwa kama ifuatavyo;-

Julai, 2017 Shilingi 1,101,193,417,551.91

Agosti, 2017 Shilingi 1,205,008,256,053.51

Septemba, 2017 Shilingi 1,345, 339,916,757.65

Kwa makusanyo haya, Mamlaka ya Mapato Tanzania, inapenda kuwashukuru wafanyabiashara


na wananchi wote kwa ujumla kwa kuendelea kulipa kodi na kuiwezesha serikali kutimiza
majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, Mamlaka inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki kwa
kila mauzo na kudai risiti kwa kila manunuzi kwani ni njia pekee ya kupata mauzo sahihi
yanayoiwezesha TRA kukokotoa kodi sahihi na kwa haki.

Napenda kuwakumbusha wananchi wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wa tarehe
na kiasi walicholipa na bidhaa waliyonunua kabla ya kuondoka na risiti hiyo. Endapo
utaona haina vigezo tafadhali ripoti kwenye ofisi ya TRA iliyokaribu nawe au piga simu
kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba 0800750075 au 0800780078. anasisitiza
Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

Vile vile, Mamlaka inawakumbusha wamiliki wa majengo nchini kulipa kodi ya majengo mapema
badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka wa fedha ili kuepuka misongamano na usumbufu usio
wa lazima.

Pia, wafanyabiashara wa michezo ya kubahatisha wanapewa wito wa kulipakodi zao kwa mujibu
wa sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41.

Pamoja Tunajenga Taifa Letu

You might also like