You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti: http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TOFAUTI KUBWA YA MISHAHARA SERIKALINI KUKOMA

Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeagizwa kufanya


utafiti wa kina utakaowezesha kuwa na uwiano sawa wa malipo ya mishahara
na masilahi ya watumishi wote serikalini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala


Bora, Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo
wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika
Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mkuchika amesema kuna baadhi ya taasisi/Idara za Serikali zinalipa


watumishi wake mishahara mikubwa tofauti na taasisi nyingine jambo ambalo
limekuwa likisababisha watumishi kutotulia sehemu moja na kutafuta masilahi
bora zaidi sehemu nyingine.

Hii haiwezekani, mmesoma darasa moja, fani moja na mko cheo kimoja, lakini
mnalipwa mishahara tofauti wakati serikali ni moja, ni lazima mlifanyie utafiti
wa kina suala hili. Masilahi ya watumishi wa umma lazima yawe sawa Waziri
Mkuchika amesisitiza na kuongeza kuwa kumekuwa na malalamiko mengi
serikalini kuhusu tofauti kubwa ya mishahara miongoni mwa watumishi wa
Serikali Kuu na baadhi ya taasisi za serikali.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka watumishi wa Bodi hiyo kuwa wabunifu na


kupendekeza mambo ambayo yatawavutia Watumishi wa Umma kufanya kazi
Serikalini kwa dhati kwa kuzingatia taaluma zao na mgawanyo wa majukumu.

Kila mtumishi ana taaluma yake na mgawanyo wa majukumu aliyopewa


wakati anaanza kazi, hivyo ni vema kila mtu akazingatia hayo ili kuwa na
utendaji bora serikalini, Mhe. Mkuchika amesema.

Mhe. Mkuchika, ameendelea na ziara ya kikazi ya kujitambulisha na kujifunza


kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake, ambapo leo
ametembelea Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bodi ya
Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa.

Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ni matokeo ya Tume


ya Rais ya Malipo ya Mishahara ya mwaka 2006 iliyopewa jukumu la kuishauri
Serikali namna ya kuboresha malipo ya mishahara na motisha nyingine katika
Utumishi wa Umma.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI


OFISI YA RAIS-MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA
TAREHE 18 OKTOBA, 2017

You might also like