You are on page 1of 2

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MFUKO WA


HIFADHI YA JAMII KWA WATUMISHI WA UMMA, 2017(THE PUBLIC
SERVICE SOCIAL SECURITY FUND ACT, 2017), KUHUSIANA NA
MASUALA YA KODI, MAFAO YA MAJAJI NA MAFAO
YATAKAYOTOLEWA KWA WATEGEMEZI

Kumekuwa na tafsiri potofu kuhusu Muswada wa Sheria ya Mfuko wa


Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (The Public Service Social
Security Fund Act, 2017), inayotolewa aidha kwa bahati mbaya au kwa
lengo la kupotosha maudhui ya Muswada huo kuwa unakusudia kutoza
kodi mafao ya Wastaafu, kubagua Wajane na kuathiri mafao ya Majaji.
Tunapenda kuutaarifu Umma na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya
Jamii kwa ujumla kwamba tafsiri hiyo siyo sahihi na ni upotoshaji
mkubwa na kwa misingi hiyo tunapenda kutoa taarifa na ufafanuzi kama
ifuatavyo:
1.0. Serikali haijawahi na wala haikusudii kutoza kodi Mafao ya
Wanachama na wala si malengo ya kifungu cha 56 cha Muswada
huu. Ni vema ifahamike kwamba hata katika Sheria za sasa za
Mifuko ya Pensheni na Sheria za Kodi, mafao ya wanachama
hayatozwi kodi, rejea kifungu cha 47(3) cha Sheria ya Mfuko
PSPF, kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Mfuko wa GEPF, kifungu
cha 90(2) cha Sheria ya Mfuko wa NSSF na kifungu cha 54 cha
Sheria ya Mfuko wa PPF. Aidha, masharti na maudhui ya kifungu
cha 56 cha Muswada yanafanana kabisa na masharti ya vifungu
tajwa hapo juu vikisomwa pamoja na sheria za kodi ambazo ndiyo
misingi wa misamaha yote ya kodi nchini.
2.0. Masharti kuhusu mafao ya Majaji yamechukuliwa kutoka kwenye
Sheria ya Mfuko wa PSPF ambako ni vifungu vya 21 na 22 vya
Sheria Hiyo. Hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwenye
maudhui ya vifungu hivyo zaidi ya kuboreshwa kwa kutenganisha
masharti ya Pensheni na stahili nyingine. Hivyo taarifa
zinazotolewa kwenye vyombo vya habari kuhusu mafao ya Majaji
ni upotoshaji wa makusudi unaolenga kujenga taswira potofu
mbele ya macho ya Jamii.

3.0. Eneo la mafao ya Wajane na warithi katika Muswada ni moja ya


maeneo ambayo yameboreshwa kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa
na masharti yalivyo kwenye Sheria za sasa. Muswada
umebainisha kwa uwazi stahili za Wajane na Warithi pale
mwanachama au mstaafu anapofariki.

Tunawashauri na kuwaasa wananchi na Taasisi nyingine kuepuka kutoa


maoni ambayo yanalenga kupotosha nia njema ya Serikali katika
Muswada huu.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam
22/1/2018

You might also like