You are on page 1of 4

MAOMBI YA KUOMBEA KIBALI KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YAKO.

Bwana YESU apewe sifa.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU na kisha tuombe maombi ya ushindi mkuu.

Katika somo la leo linahusu maombi ya kibali kitakachokuwezesha kuwa mshindi katika maisha yako
yote.

Kibali ni nini?

Kibali ni idhini anayopata mtu ili kupata vitu fulani avitakavyo.

Kibali ni kukubaliwa kufanya jambo jema unalolitaka kulifanya.

Kibali ni ruhusa inayovisukuma nje vizuizi vyote.

Kibali ni ridhaa ya kutenda unachotaka kutenda.

Sasa nisikilize kwa maandishi haya itakusaidia.

1 Samweli 2:26 ''Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia.''

Samweli alikuwa mteule wa MUNGU kama ulivyo wewe ulieokolewa na Bwana YESU.

Samweli alikuwa na kibali kwa MUNGU na kwa wanadamu.

Kibali kilikuwa kimemtangulia Samweli katika maisha yake, ndio maana alisema naye mara kwa mara.

Kibali kilifanya Samweli awe mtawala wa waisraeli wote bila kuchaguliwa na watu wala kuteuliwa,
alikuwa mwamuzi wa mwisho kabla ya mfumo wa ufalme haujaanza katika Israeli.

Biblia inasema watu walikuwa wanamfuata ili awaamue na kuwafundisha na kuwaelekeza, Kwa
sababu ya nini?

Ni kwa sababu ya kibali.

Baadae Waisraeli walitaka mfalme ndipo MUNGU akasema na Samweli na kwa kupitia Samweli, Sauli
akawa mfalme. Lakini jambo la ajabu ni kwamba Samweli alikuwa na nguvu wakati mwingine kuliko
Mfalme maana hata Mfalme alihitaji Msaada kwa Samweli mwenye kibali kwa MUNGU na wanadamu.

Pia, Ukisoma habari za Yusufu, hasa ukianzia pale alipofungwa gerezani Mwanzo 39:20-23

Eleza namna kibali a

Kibali kina nguvu sana sana.

Ukishindana na mtu mwenye kibali itakusumbua sana kumshinda.


Nilichojifunza ni kwamba kila eneo la maisha yako unahitaji kibali cha MUNGU ndipo utafanikiwa na
kustawi.

Sio waliosoma wote na kazi nzuri, wenye vibali haijalishi wana elimu ndogo wana kazi.

Hebu ngoja nikufundishe kazi za kibali ili upate msukumo wa kuombea kibali chako.

1. Kibali kinafungua macho ya watu kukuona na kukutendea mema.

2. Kibali kinaamrisha watu kukukubali na kukutendea mema, hata kama huna sifa za kukubaliwa

3. Kibali kinawafanya watu kukuheshimu na kukuthamini.

4. Kibali kinawafanya watu kukupenda na kukufanyia mema, hata kama huna sifa za kupendwa.

5. Kibali kinawafanya watu wakufuate katika unayoyasema na kuyafanya.(Utiisho)

6. Kibali kinakutengeneza ili ufae, hata kama hufai.

7. Kibali kinaleta upendeleo kwako, hata kama hustahili kupendelewa.(Uuze nini kisinunulike, hata
upange mawe barabarani yatanunulika tu)

Zaburi 106:4- '' Ee BWANA, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa
wokovu wako, Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu
pamoja na watu wako.''

Hujawahi kumuona mtu ambaye watu wengi sana wanamkubali sana sana hata kama hana sifa yeyote
njema, huyo mtu ana kibali.

Dalili za mtu ambaye kibali chake shetani amekiharibu.

1. Hafanikiwa hata kama ana sifa zote za kufanikiwa.

2. Kutumia nguvu nyingi sana hata pale ambapo asingetumia nguvu nyingi akiwa na kibali.

3. Kukataliwa bila sababu, kuonewa bila sababu bila kosa na kupuuzwa bila sababu za msingi zozote.

4. Kutokufikia lengo la mafanikio yaliyokusudiwa.

Omba MUNGU akuletee watu wanaokiona kibali chako kutoka kwa MUNGU na kukithamini.

Jambo kubwa tu kumbuka tuliumbiwa matendo mema ili tuyaishi hivyo kibali alichokupa MUNGU ni
kwa mema na sio mabaya.

Endelea kujifunza somo hili itakusaidia.


JE NI SABABU GANI ZINAZOSABABISHA UKOSE KIBALI MACHONI PA MUNGU NA KATIKA
MAISHA YAKO.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha ukose kibali. Baadhi ya sababu hizo ni kama
ifuatavyo;

01.Dhambi unayoendelea kufanya.

Ikiwa utadumu katika kufanya dhambi,basi ujue unajitenga na Mungu,na kitendo cha kukaa mbali na
Mungu kinakunyima nafasi ya kukubalika mbele za Mungu na hapo hujikuta umekosa kibali kabisa.
Kumbuka kwamba ; mwenye kutoa kibali ni Mungu tu katika Kristo Yesu. Sasa ikiwa upo mbali naye
itakuwa na maana upo karibu na shetani. Maovu pamoja na dhambi zako zinauficha uso wa Mungu (
Isaya 59:2). Unapofikia hatua ya kuipenda dhambi fulani,basi ujue huwezi kuwa na kibali machoni pa
Mungu.

02. Kukamatwa na roho ya kukataliwa.

Inawezekana ikawa unajitihada nyingi kwa Mungu wako,na ikawa unajitahidi kumlingana Mungu lakini
unajikuta bado unkataliwa katika mambo mengi uyafanyayo. Ikiwa ni hivyo basi ujue kuna roho ya
kukataliwa inayokusumbua. Sasa,roho hii inaweza ikawa na vyanzo vingi tu. Mojawapo ya chanzo cha
roho ya kukataliwa yenye kukuondolea kibali ni

1. roho mbaya za kurithi.~ unaweza kurithi tabia,magonjwa,hata roho ya kukosa kibali. Unjikuta
huna mvuto wa kitu chochote kile. Inawezekana ukawa umezaliwa katika ukoo ambao kuna
roho ya kukataliwa inayosumbua. Unahitaji Mungu akufungue katika maombezi.

2. Majina ya kupewa/matamko/maimbilizio ya kimaneno.~ Kwa sehemu kubwa majina


yanachangia sana katika kukuondolea kibali ( 1 Samweli 25:25).Au maneno yaliyotamkwa kwa
waganga na wachawi kabla ya ufahamu wako ulio nao sasa,ikiwa kama hayajashughulikiwa
ipadavyo unaweza ukajikuta unakosa kukubalika katika yale uyafanyayo

03. Kujiinua/kujikweza

Kujiinua ni tabia ya shetani ya kutaka kupewa sifa anazo stahili Mungu. Au ni hali ya kutaka kupewa
sifa ambazo hustahili kabisa. Hivyo kila anayejiinua Bwana atamshusha tu ( 1 Petro 5:5-6) Lakini soma
pia yule Farisayo alivyojikinai katika Luka 18:9-14.

Ukiwa na tabia ya kiburi basi ujue huwezi kuwa na kibali machoni p Bwana hata mbele za watu. Mfano
mdogo; ukiwa mtu wa kujiinua utaona hata watu hakupendi kiivyo kwa sababu ya tabia yako
hiyo,tena inawezekana ukawa unataka kusema ujumbe mzuri tu,lakini kule kujisifia sana
kunakupotezea kibali cha kufikisha ujumbe huo.

Je kibali kinapatikanaje?

01. Kwa kumcha Bwana.


Kumcha Bwana ni mchakato wa maisha ya kiibada. Kumcha Bwana ni kitendo cha kuwa na roho ya
kicho;Hivyo kumcha Bwana ni hatua ya msingi ya kuvikwa kibali cha Bwana. Kabla ya yote,ukimuamini
Yesu na kumpokea awe Bwana na mwojozi wa maisha yako,basi uwe na uhakika atakupa uwezo wa
kufanyika mtoto wa Mungu (Yoh.1:12)Kile kitendo cha kupewa uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu
kinakupa nguvu ya Mungu katika yale uyatendayo.

02. Kuwa mwaminifu - Ukiwa mwaminifu katika nyanja zote za wokovu wakovu wako basi ujue
kibali kitakuwa ni sehemu yako.

Tunaweza kujifunza kwa Yusufu mtoto wa Yakobo. Yusufu alikuwa amekaza kwa Bwana na mtu
mwaminifu kiasi kwamba alipolazimishwa alale na mke wa Potifa alikataa akaona hawezi kumkosa
Mungu kwa dhambi hiyo ya kutembea na mke wa boss wake ( Mwanzo 39:9). Tazama jinsi Yusufu
alivyotembea katika kibali cha Mungu katika maisha yake. Kila alipoingia mahali,Bwana alikuwa
pamoja naye;angalia kaingia katika nyumba ya Potifa,gafula nyumba nzima ikabarikiwa,kaingia tena
gerezani Bwana akamuinua kutoka huko mpaka akawa waziri mkuu wa nchi ya Misri.

Haikuwa ni jambo la kawaida tu,bali Mkono wa Mungu ulimtangulia na ndio kibali chenyewe
tunachojifunza leo. Unahitaji kibali kama hicho,basi ukubali kulipa gharama ya kuwa mwaminifu. Ifike
wakati uikimbie dhambi ujitunze katika kifungo cha uaminifu.

03. Neno lijae kwa wingi ndani yako.

Ukiwa na neno kwa wingi ndani yako ni sawa na kusema umembeba Yesu ndani yako kwa maana
Yeye Yesu ndio Neno mwenyewe. Na ikiwa utakuwa umekaa ndani ya Yesu na Yesu ndani yako, hapo
uwe na uhakika utakuwa na kibali machoni pa Mungu kwa maana yale uyatendayo hayatakuwa yako
bali yatakuwa yametoka kwa Mungu.

Labda jifunze kwa kumuangalia yule mwana-punda aliyembeba Yesu katika LUKA 19:33-37. Utaona
kwamba mwana-punda akikubalika na kundi kubwa la watu kiasi kwamba ilimbidi atembee juu ya
nguo na matawi waliyoyatandaza watu,kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani kwake isipokuwa kwa
kumbeba Yesu tu,naye akapata heshima ya juu.

You might also like