You are on page 1of 3

MAONYESHO YA CHAKULA, KAHAWA NA CHOCOLATE YAFANYIKA SAUDI ARABIA

Maonyesho ya chakula, kahawa na chocolate yamefanyika mjini Riyadh, Saudi


Arabia. Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ulishiriki kwa kuwaalika baadhi ya
wafanyabiashara kutoka Tanzania na wafanyabiashara raia wa Tanzania wanaoishi
Saudi Arabia.

Katika maonyesho hayo bidhaa za kahawa ya kijani (green beans) zilionyeshwa na


kuvutia wanunuzi wengi wa Saudi Arabia ambao waliweka miadi ‘order’ za kuagiza.
Bidhaa zingine zilizowekewa miadi ya kuagizwa ni pamoja na korosho, chai,
karafuu, hiliki na viungo. Pia watu walitembelea banda la Tanzania walipata fursa
ya kuuliza maswali na kupokea taarifa kuhusu uagizaji wa bidhaa na mazao ya
kilimo kutoka Tanzania.

Kampuni mbili za Saudi Arabia ambazo zilipata taarifa za kahawa kutoka Tanzania
katika maonyesho yaliyotangulia ya mwaka 2016 na 2017 zilishiriki na kuuza
kahawa iliyokaangwa (roasted) kutoka Tanzania kwa wingi. Kampuni hizo ni
Roasting House ambayo kahawa yao huipata kutoka Ruvuma, kampuni nyingine ya
pili ni Filter Coffee Roasters ambayo kahawa yao huipata kutoka Songwe. Watu
wengi walifurika katika mabanda ya makampuni hayo mawili ya Saudi Arabia
kununua kahawa ya kutoka Tanzania kwa kuwa ina ubora wa hali ya juu
ukilinganisha na kahawa za kutoka maeneo mengine ambayo zilikuwa ikiuzwa.

Taarifa zaidi na video zinapatikana kwenye YouTube ya Prince EddyCool.

Watu mbalimbali wakiwa katika banda la Tanzania kupata maelezo ya bidhaa za


Tanzania.
Sehemu nyingine ya watu waliofurika katika banda la Tanzania katika maonyesho
ya chakula, kahawa, chai na chocolate mjini Riyadh, Saudi Arabia.

Wateja wakiwa wamefurika katika banda la kampuni ya Saudi Arabia iitwayo


Roasting House ambayo inauza kahawa iliyoakaangwa kutoka Ruvuma, Tanzania.
Watu waliotembelea banda la Tanzania mjini Riyadh wakionja chai na kahawa ya
Tanzania ikiwa ni pamoja na kupata vipeperushi vinavyolelezea kuhusu mazao ya
Tanzania.

Mmojawapo ya wafanyabiashara mwanamama kutoka Tanzania akipanga bidhaa


zake za asali kahawa na chai katika banda la Tanzania mjini Riyadh, Saudi Arabia.

You might also like